Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kitendo cha Rais Magufuli kuwateua Nape NNAUYE, DK HARRISON MWAKYEMBE na Prof SOSPETER MUHONGO kuwa Mawaziri kiliwaumiza sana mafisadi wakiongozwa na fisadi Mkuu Edward Lowasa. Kutokana na hali hiyo, mafisadi hao waliweka mikakati ya kuwashughulikia mawaziri hao huku wakiamini kuwa ikiwa watafanikiwa lengo lao la kuwashughulikia, watakuwa wamelipa kisasi.
Mtakumbuka kuwa Harrison Mwakyembe ndiye aliyeshindilia msumari wa mwisho siku chache kabla ya uchaguzi na Watanzania hawakufanya ajizi. Wakamtosa fisadi Lowasa. Nape Nnauye alisimamia chama wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM. Siku zote Nape alisimama kidete na kukemea matendo yamkifisadi aliyokuwa anafanya Lowasa ili tu ateuliwe kuwa Mgombea Urais. Ilifikia hatua mpaka akapachikwa jina la Vuvuzela kwani wakati wote alikuwa anasema bila woga.
Prof Sospeter Muhongo ana mgogoro mkubwa na Reginald Mengi ambaye ni mfadhili wa fisadi Lowasa katika harakati zake za kwenda Ikulu. Mgogoro huo ulikuja baada ya Prof Muhongo kusimama kidete kuhakikisha kuwa madalali hawapati nafasi na hawakabidhiwi rasilimali za nchi hususan vitalu vya gesi, mafuta na madini.
Kutokana na hali hiyo, mafisadi walijipanga kisawa sawa kuhakikisha kuwa mawaziri hao wanayumba. Mkakati upo namna hii. Baadhi ya wabunge wameteuliwa ambao jukumu lao litakuwa kuibua mijadala itakayohusu wizara hizo na hatimaye wabunge wengine wa upinzani kuendelea kukandamiza mpaka ionekane kuwa mawaziri hao hawamudu. Kila Waziri ametengenezewa skendo zaidi ya moja. Prof Muhongo ameandaliwa sakata lile lile la ESCROW na aliyekabidhiwa jukumu la kumhenyesha Muhongo hi Zitto Kabwe. Wengine ni Jesca Kishoa, mke wa David Kafulila ambaye ndiye aliyekabidhiwa mikoba na Reginald Mengi kumshambulia Muhongo. Pia Prof Muhongo anaundiwa zengwe kuwa kuna makampuni binafsi anafanya nayo deal ya kuzalisha umeme ili yeye apate ten per cent. Pia Prof Muhongo anaundiwa zengwe kuwa miradi ya kufua umeme ya Kinyerezi ina ufisadi mkubwa na kwamba yeye kama Waziri, ameshiriki kwenye ufisadi huo. Yapo mengi ila kwa leo nadokeza haya tu.
DK Mwakyembe anabebeshwa zigo la Mabehewa feki. Walioandaa mkakati huo walikuwa wanataka kutumia mwanya wamkusimamishwa kazi kwa watendaji wa Mamlaka ya Reli ili kumhusisha Waziri kwenye Sakata hilo. Hata hivyo, inaonekana wamebugi from the Beginning. Jesca Kishoa aliyekabidhiwa jukumu hilo hana uwezo wa kujenga hoja badala yake amejikuta akiwasilisha hoja ambazo zinamkaanga yeye mwenyewe.
Nape Nnauye ameundiwa zengwe kuwa hana uwezo wa kufanya kazi kwenye wizara husika. Wapinzani na hasa wale waandishi makanjanja wanamuogopa sana Nape kwa vile ana uwezo mkubwa wa kuchukua hatua pindi anapogundua kuwa mambo hayajaenda sawa.
Hata hivyo, inaonekana kuwa mikakati yao yote imefeli. Na kwa vile tayari imegundulika, Mafisadi kwa sasa wanahaha kuhakikisha kuwa hawaendelei kuumbuka.
Tutaheshimiana tu.