Zitto amkaribisha Kafulila CHADEMA

Zitto amkaribisha Kafulila CHADEMA

Msajili wa vyama vya siasa angalau angekuwa na kauli au mamlaka flani hivi kisheria inayomruhusu kuamua kama mtu aliyefukuzwa uanachama wa chama fulani taratibu, haki zimefuatwa. Huyu wetu anasimamia RUZUKU tu na kusajili. Msajili pia angeangalia kama fukuzafukuza hii ina maslahi kwa Taifa au inalinda tu maslahi ya wakubwa ndani ya vyama hivi.
Tendwa, peleka marekebisho ya sheria iliyounda ofisi yako ili tusihangaishwe na wenye vyama hivi.
 
tatizo la yule dogo ni mpenda vyeo na msemaji mno.
He is too young to be wise........RR.
 
Mbaya sana kufukuza mtu eti kwa sababu ya kutofautiana na Mh mwenyekiti, na si kwa utendaji mbaya, je wabunge wake wote wakitofautiana naye atawatimua wote? kwa mitndo huu vyama vya upinzani havitafika popote, nawasifu CCM wanavyomaliza tofatui zao bila kufukuzana, wako makini sana kwa hilo, huwa hawakurupuki, kwa hili la kafulila hapa Mbatia amekurupuka, wangeweza kuelewana na kupeana hatua zingine za kinidhamu na si kumfukuza mbunge dishonorably!

Ulishawahi kusikia neno "Nidhamu" ukitofautiana na viongozi wenzako ndani ya Chama huendi kupayuka payuka kwenye vyombo vya Habari. Vyama vina katiba zao na hizo katiba zimeweka utaratibu wa kufikisha malalamiko kunakohusika. Nccr ilivurugika wakati ule waMrema kwa kuwa Nidhamu ilitoweka kila mtu anasema lake
 
ulimi ni kiungo kidogo sana ila kinaweza kikakuinua au kukushusha, kinaweza kikakupa faraja au kikakupatia fedheha, ndimi hizi tuzichunge jamani, chanzo cha mafarakano ni ndimi na sivinginevyo.
 
Kwani katiba ya CDM inasemaje? Kafulila anaweza kujiunga na CDM Kama mwanachama tu. CDM isimpe uongozi wa aina yeyote hata ujumbe wa kitongoji. He proved not to be a leader but a power monger. Mtu wa hivyo is dangerous popote atakapoenda. Mtakumbuka alijiunga na Cuf kuikandamiza CDM ili tu awekwe kwenye kamati za bunge!
Zito Hana mamlaka ya kutoa mualiko. Mbinu yake kumtumia Kafulila ili akamsafishie njia ya kuuchukua nccr imeshindwa vibaya.

Cdm haimpi mwanachama uongozi wanachama ndowanao chaguwa viongozi
 
Daaaaah! Nna hofu acje akaharbu na uku kwetu inabd tujifunze kupitia kwa shibuda mana hawakawii hao muac na muac tu
 
Msajili,
Chunguza pia KATIBA za hivi vyama ulivyosajili. Maamuzi kama haya ya kumfukuza mtu uanachama si madogo kiivyo. YanaVURUGA mfumo mzima wa maisha ya mtu, familia yake na wote wanaomtegemea. Haina tofauti na kufukuzwa kazi au kufiwa na mke. Halafu BUNGE letu limekaa kimya tu. Kafulila ni mwajiriwa pale. Bila shaka wataomba maelezo ya kina toka NCCR-MAGEUZI. Mbona polisi sheria inawataka wapewe taarifa tu juu ya maandamano na mikutano lakini kuna wanayoizuia isifanyike?
 
Kama cdm alitimuliwa na sasa Nccr katimuliwa inaonyesha dhahiri yeye ndn ana matatizo na sio vyama na kwa sasa vyama vinavyomfaa ni ccm na cuf ambao wamepoteza mwelekeo kama yeye
 
shibuda ni kirusi cha UKIMWI!

Kweli Shibuda nikirusi ndani ya CDM, Lakini kumbuka kuwa kuna wakati mwingine unaoa mwanamke na baadaye unagundua ana kasoro za kitabia au hata ile shughuli ya bibi ana bore..vyote hivyo havihalalishi kumwacha bali is better to ignore her and find substitute to fill the gape, so Kafulila na Shibuda wanaweza kubaki CDM bila athali sawa tu na Zitto anavyolelewa na wazee wa CDM otherwise Zitto naye angeshamwagwa zamani kama sio busara za wazee akina Mtei
 
Nimegundua hawa wabunge wengi vijana waliopata umaarufu gafla wameanza kupoteza mwelekeo. Ukiwaangalia wanapoteza muda mwingi kupanga strategies za kuzidi kuwa maarufu. Sio vibaya mwanasiasa kupanga njia za kuwa mwanasiasa zaidi , tatizo ni pale wanaposahau kabisa kuwatumikia wapiga kura wao. Wanadhani wapiga kura ni mbumbumbu ambao muda wote wataaungamkono.

So bidii wanaweka katika kupanga majungu ya kuenguana na kueneza fitina. Na wanadhani wao ni wakubwa kukliko vyama vyao na wapiga kura wao. Mfano Kafulila alidai yeye ni mkubwa kuliko Mbatia kwakuwa alishinda ubunge na Mbatia akashindwa sasa alikuwa anampigia magoti na kumlilia ili iweje? Ina maana Kafulila hajui umuhimu wa chama. Sasa ataujua.

Nawashaulil wafanye kazi kwa bidii wawatumikie wananchi then wananchi ndo wataamua wawe wakubwa zaidi au la.
 
Walicheza na vyombo vya habari wakidhani vitawafikisha huko kwenye malengo yao ya kisiasa. Kafulila ameanza kufukuzwa toka NCCR na vyombo vya habari ikiwemo maoni ya baadhi yetu humu JF. Ule mkutano wa Mbatia na genge lake umethibitisha tu hukumu ile.
 
ZITO asijichanganye,huwasipendi watu wasio kuwa na misimamo. naamini zito ni makini na kwa umakini huo ya NCCR AACHANE NAYO.
 
Upo sahihi ,huwa najiuliza kwa nini Zitto huwa anapenda kutoa taarifa/habari bila kujua/kutafakari kuwa watu/wafuasi wake wataichukuliaje hiyo habari?!!!.Huyu bwana ana hulka ya kupenda kuenekana kuwa yeye huwa hakosei na ndio kitakachomtafuna taaratibu
Huyu Zitto nae anatafuta umaarufu wa kisiasa na migogo na viongozi wenzake.

Ni wazi Kafulila akishawika na ombi la Zitto la kurudi, Chadema watampa masharti kuweka mambo sawa jinsi alivyoondoka nani wazi Kafulila hatakataa na uwezekano mkubwa Zitto atamwunga mkono kurudi bila masharti. Kafulila ataamia Cuf au chama kingine, atagombea tena kutetea kiti chake na atashinda.Zitto atakimbilia facebook kuandika message ya kujisifia kuhusu ombi lake like it was a rocket science na kuponda uhamuzi wa chama.
 
Kafulila ni kama pigo la Knock Out! Ngumi moja hiyohiyo ndiyo iliyompeleka chini, hakuna kujitetea, kujiuliza, kujifikiria wala kuonywa!!
Kweli mkuu adhabu za kuviziana hizo yaani kwamba alikuwa anatafutiwa kona ya kummaliza, ndyo maana hakuna cha onyo wala kujitetea, this was their only chance, maisha yangekuwa kwa staili hiyo ktk nyanja zote, sijui kama kungekuwa na amani.
 
Msajili wa vyama vya siasa angalau angekuwa na kauli au mamlaka flani hivi kisheria inayomruhusu kuamua kama mtu aliyefukuzwa uanachama wa chama fulani taratibu, haki zimefuatwa. Huyu wetu anasimamia RUZUKU tu na kusajili. Msajili pia angeangalia kama fukuzafukuza hii ina maslahi kwa Taifa au inalinda tu maslahi ya wakubwa ndani ya vyama hivi.
Tendwa, peleka marekebisho ya sheria iliyounda ofisi yako ili tusihangaishwe na wenye vyama hivi.

Hapa ninaungana nawe sana Mkuu. Lakini sidhani kama hili ni jukumu la Mzee (wa) Tend(w)a, bali udhaifu wa Sheria zetu, ikiwemo sheria vya vya siasa na uanachama katika vyama hivyo. Pamoja na hilo la kuhamahama vyama, nadhani sheria zetu zingekuwa na kiwango cha idadi ya vyama vya siasa. Leo hii sijui tuna vyama vingapi (13, 15, 17?) Ya nini utitiri wa vyama vyote hivi? Kwa nini hawaundi NGO's za kikanda?
:focus:Wazo langu ni kama lako, ikiwa mtu ametimuliwa chama kimoja asiruhusiwe kwenda chama chengine, au angalau mtu asiruhusiwe kurudi chama alichohama. Hivi ni sawa na kukokota wafu.
 
Good Idea kama kweli hakufukuzwa CDM!KFLL should then be double careful in what he talk. Plain Talking at times has its own costs. Be bold and stand firm.
 
Back
Top Bottom