Zitto amkaribisha Kafulila CHADEMA

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,719
1,440
Zitto Kabwe swahiba na mshirika wa karibu wa mbunge aliyetimuliwa kwenye chama chake Kafulila, ameweka wazi kutojihusisha na sakata la Kafulila kwa namna yoyote.

Akiweka maelezo kwenye ukarasa wake wa Facebook ameshindwa kujitetea kuhusu tuhuma za yeye kuwaita polisi.

Hata hivyo ameelezea kuwa huwa mara zote yuko upande wa mtu anayeonewa na mnyonge. Mwisho ameweka wazi Kafulila anakaribishwa CDM na kwamba hakufukuzwa hivyo katiba ya Chadema ipo wazi anakaribishwa

source FB
 
Heheheeeeee! CDM wasije wakafanya kosa kama ilo la kuingiza kirusi ndani ya chama chao. Aende zake mwanakwenda kwani alilewa sifa za kijinga na akajisahau kufikiri kama binadamu na badala yake akakubali mtu mwingine afikiri kwa niaba yake. matokeo yake amekua akikokotwa kama kondooo.
 
Anarudi kufanya nini wakati alisema CDM ni chama cha kikanda?faida ya kuropoka ndio hiyo.Kama alipiga magoti kwa Mbatia basi awapigie magoti wana CDM kwa maneno yake ya kebehi ili asamehewe.Bado yeye ni kijana mpambanaji ila tuu nidhamu ni ziro.
 
Kafulila fanya unachoona ni sahihi kutoka moyoni mwako. Ukishauriwa changanya na za kwako. Jaribu kuwa independent kimaamuzi itakusaidia kukwepa migongano isiyo lazima.
 
Zitto Kabwe swahiba na mshirika wa karibu wa mbunge aliyetimuliwa kwenye chama chake Kafulila,ameweka wazi kutojihusisha na sakata la kafulila kwa namna yoyote.Akiweka maelezo kwenye ukarasa wake wa Facebook ameshindwa kujitetea kuhusu tuhuma za yeye kuwaita polisi.Hata hivyo ameelezea kuwa huwa mara zote yuko upande wa mtu anayeonewa na mnyonge. Mwisho ameweka wazi Kafulila anakaribishwa CDM na kwamba hakufukuzwa hivyo katiba ya Chadema ipo wazi anakaribishwa source FB

Zile kasoro za CDM alizozikimbia awali zimekwisharekebishwa?
 
Anarudi kufanya nini wakati alisema CDM ni chama cha kikanda?faida ya kuropoka ndio hiyo.Kama alipiga magoti kwa Mbatia basi awapigie magoti wana CDM kwa maneno yake ya kebehi ili asamehewe.Bado yeye ni kijana mpambanaji ila tuu nidhamu ni ziro.

Hiyo inaitwa kunyea kambi!
 
Shibuda mwingine huyo!ya shibuda mmeshindwa kuyatatua na bado mnataka kuongeza kero ingine na matatizo?waungane na Hamad Rashid kuunda chama chao!cdm say no.
 
Zitto are you real great thinker?. umekosea sana kusema mapema hiyo mishe. sasa hapa umuongeza attention kwa wananchi, na kwa namna hiyo resistance ya kujoin CHADEMA itakuwa kubwa sana.

bora ungekaa kimya. Alafu unasibitisha kuwa mambo mengi unayofanya haya hayana strategies. na usipo angalia, watu wataku-group pamoja na akina nape.

kuna mambo unayafanya halafu baadaye unatumia nguvu nyingi sana kujitetea. usifikiri nguvu ya hoja hafanya kazi vizuri mara zote(long term strategies is needed na sio kama hivi unavyo fanya).

Halafu Kafulila akirudi CHADEMA ataonekana kuwa yeye anachokitaka maishani mwake ni ubunge na vyeo tuu.
 
Kafulila alishajea kambi kurudi cdm haina tofauti na wale wanyama wanaokula watoto wao kimsingi ni aanzishe chama
 
Siasa za bongo zinahitaji akina kafulila kama kumi ili kuweka sawa siasa za bongo
 
Back
Top Bottom