ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,950
- 6,981
Niliwahi kushauri kitu hiki katika moja wapo ya mitandao ya kijamii na leo narudia. Ningetamani kuona ibara hii katika katiba "IWAPO MBUNGE ATAJIUZURU KWA HIARI YAKE BASI CHAMA KILICHOMDHAMINI KICHANGIE ASILIMIA 50 YA BAJETI YA UCHAGUZI MDOGO NA GHARAMA ZOTE ZITAKAZOONGEZEKA NA IWAPO CHAMA KIKIMFUKUZA UANACHAMA MBUNGE WAKE BASI KICHANGIE 100% YA GHARAMA ZA UCHAGUZI MDOGO.
NA MCHANGO HUU WA UCHAGUZI UTAPUNGUZWA KATIKA RUZUKU YA CHAMA NDANI YA KIPINDI MAALUM"
Tungekuwa na hii kitu ktk katiba yetu ya Kafulila na gamba la Igunga tusingeyasikia na tungeokoa kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi wenye njaa,hawana mikopo ya elimu,hawana barabara,walimu wanaoidai serikali na mengine kibaooo, nawasilisha
wazo lako zuri sana, lakini nani wa kulitekeleza katika nchi hii ambapo watoa maoni hawaheshimiki? ukitoa maoni yako utaitwa mchochezi