Swala la Kafulila linaonyesha jinsi gani sheria ya mgombea binafsi ni ya muhimu sana nchini kwetu. Sasa hivi jambo linaloonekana mbele yetu hapa ni la watu wawili waliogombea Ubunge katika majimbo yao; mmoja akashinda na mwingine akashindwa. Sasa yule aliyeshindwa akatokea kuwa ni mwenyekiti wa chama kilichowasimamisha wagombea hao wawili. Kutokana na uneyeyekiti wake, anaamua kumvua unachama mbunge aliyechaguliwa na wanachi kwa kujua kuwa hatua hiyo itamvua ubunge pia.
Kwa wenzetu kama Marekani, mtu unaweza kuchaguliwa kwa kupitia chama kimoja halafu ukaamua kuachana nacho na kuingia chama kingine kama vile alivyofanya Senator Arlen Spector alipohama kutoka Republican na kujiunga na Democrat. Utaratibu wetu unaonyesha jinsi gani wapiga kura wasivyokuwa na sauti kwani mgombea wao anaweza kuvuliwa kiti chake kirahisi tu kwa vile eti hakubaliani na mwenyekiti wa chama chake. Na hiyo ndiyo tabia mbaya tunayotaka ikomeshwe mara moja kusudi wabunge wetu wasitumike kama rubber stamp tu.
Kama Mbatia anaona kuwa hatua aliayochukua ni sawa, je atawakemea nini wabunge wa CCM wakiamua kukubalia kila upupu unaoletwa na serikali bungeni iluhali serikali hiyo inaongozwa na mwenyeketi wao ambaye akitumia madaraka yake kama Mbatia anaweza kuwafukuza wote kutoka ndani ya CCM na hivyo kupoteza ubunge wao?