Hebu watanzania tufike mahala tufanye kufikiri kama ni janga linalokaribia kuangamiza utaifa wetu,matokeo yake ni kuzorota kwa uchumi,siasa na utamaduni.
Kuna watu wanamubeza Kafulila pasipo kufikiria juu ya mapana ya Demokrasia ya kweli na inayoonekana katika mihimili yake mikuu.
Kwa nini hatujiulizi kwamba kwa katiba iliyopo ina ufalme wa kichama kuamua kumfukuza uanachama mbunge wake kwa tofauti za mawazo kinyume na uhuru wa mtu kutoa mawazo yake na kuyaheshimu hata kama huyapendi.
Ina wanyima wananchi Fursa ya kumfukuza mbunge wao kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ya kibunge ila ina kipa mamlaka makubwa chama kumfukuza mbunge au kumtetea pale ambapo hakidhi matakwa ya wananchi.
Mamuzi ya chama hayapingwi na wananchi.
Chama ndicho Alfa na Omega.
Wananchi ambao katiba ya JAmhuri ya Muungano,ibara ya 9,inatamka wazi kwamba wananchi ndiyo Alfa na Omega kwa masuala yoyote yanayohusu Taifa.
Lakini contradiction yake Chama kinamfukuza mbunge hata kama wananchi wanamwitaji kuliko hitaji la chama!!!!!!!!!
watu tunashangilia kufukuzwa kwa kafulila katika mazingira ya demokrasia ya wakubwa!!!!!!!!!!!siyo ya wananchi!!!!!!!!
Kumbe Demokrasia kwa Tanzania ya kumchagua mwakilishi wao ni wakati wa uchaguzi tuu,wakimchagua hawana nguvu ya kumkataa kwa muda ule mpaka kipindi cha miaka mitano kiishe,Ila Chama kina demokrasia wakati wote wa kumuidhinisha na wa kumfukuza!!!!!!!!!!!
Vyama vina nguvu kuliko maelfu ya wananchi walio poteza masaa,wakikauka kwenye jua kumpigania mbunge wao!!!!!!!
Mbunge akigombana na wananchi wake hawana ubavu wa kumtoa!!!!! Ila akigombana na kiongozi wa kikundi cha chama ananyang'anywa ubunge wake mara moja!!!!!!!!!!.pasipo kuwasikiliza wananchi wake.Hii ndiyo tafsiri ya demokrasia kwa mnao shangilia badala ya kutafakariii?
Suala jingine ni kwamba Chama chochote cha siasa ni mali ya Ummah,ndiyo maana nguvu yake ni wananchi,lakini kikubwa zaidi haviendeshwi kwa pesa zake tuu bali kodi zetu sisi wananchi,vinahudumia wananchi wake kwa kuwasemea na kuwatetea,vina milango wazi kwa watanzania siyo warwanda au popote,Kafulila ni Mtanzania,anao uhuru wa kuhoji,anao uhuru wa kuchagua chama cha kujiunga nachama chochote kikatiba.
Naskitika watu wanaoshangiria uhalamia huu wa demokrasia hewa,kweli nimeamini suala lolote la kijinga,kipuuzi na kipumbavu,makao makuu yake ni Tanzania na siyo pengine,Kila jamii inastahili ya uongozi wake,kweli Mtanzania nimeamini hawezi kuongozwa na Jamii ya kenya na ya Kenya haiwezi kuongozwa na Mtanzania.
Ingekuwa ni jamii nyingine hapa duniani ingehoji nguvu ya Chama kuzidi ya wananchi waliomchagua!!!!!!!!!!
Ni wananchi wawe na mamlaka ya mwisho?au Vyama viwe na mamlaka ya mwisho kwa mstakabali wa taifa hili?Kafulila karibu Chadema,mapambano ni safari yenye mabonde ya furaha na milima ya uvuli wa mateso na umaiti.