Zitto afanye haya kurudisha umaarufu wake

.
Nasikia mkuu Passco ni kiranja kwa wale wa zile ...... Za khaki. Yana ukweli haya?
.

Kama ndio pasco mayala huyu ni mwandishi habari uchwara tu hivi unapata wapi ubongo wa kumsifia zitto kama sio mchumia tumbo?
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi Chadema ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.

Umaarufu wa Zitto uko mfukoni,si wengi wanaomfahamu Zitto kama inavyooneka.Hana ability yoyote-sababu akashindwa kuyataja majina ya mafisadi wenzake.
Angekuwa na ability angesimamia vyema kauli zake za ubadhilifu kwenye madini,angetaja na kuomba msaada wa ujumla(wananchi) kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika n.k
Ayafanyo Zitto,kila mtu anaweza kuyafanya...Zitto ni wa kawaida na nafasi yake,uwepo wake waweza zibwa na wengi-ambao ni zaidi yake.
 
Unaarufu upi?
Bila kazi iliyofanywa na TINDU kwa miaaka zaidi ya kumi huko migodini na yeye kupewa desa aliwasilishe bungeni angekuwa hapo?

Bila kazi iliyofanywa na wanachadema kigoma yeye akiwa mwanafunzi, kumbuka ile makala ya kibanda kuwa alitoka shule na kukuta network ya chadema ipo na yeye kupata ungunge kiulaini, angekuwa wapi leo?

mkuu hakuna aliyekuwa anafahamu utendaji wake kwani hakuwepo Kigoma muda mrefu alikuja tu na kugombea baada ya kutoka nje kama sio kazi kubwa iliyofanywa na wanachadema kigoma kama waliokuwa madiwani wa chadema kipindi hicho leo hii Zitto asingekuwa mbunge.
 
hii pumba jf haiwez present watanzania wafanya maamuzi angalia hzo thread za vijana wa chadema wanao rumbana utakuta kuna post 1500 kumbuka mtu moja ana post comment had 20 na ukiangalia hzo comment 1500 hazizid watu 100 so kwa akili yako watu 100 wana present watanzania mbaya zaidi unaona watu wenyewe ni washabiki wa mlengwa gan
 
Umaarufu wa Zitto uko mfukoni,si wengi wanaomfahamu Zitto kama inavyooneka.Hana ability yoyote-sababu akashindwa kuyataja majina ya mafisadi wenzake.
Angekuwa na ability angesimamia vyema kauli zake za ubadhilifu kwenye madini,angetaja na kuomba msaada wa ujumla(wananchi) kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika n.k
Ayafanyo Zitto,kila mtu anaweza kuyafanya...Zitto ni wa kawaida na nafasi yake,uwepo wake waweza zibwa na wengi-ambao ni zaidi yake.
Waingereza walitutajia mpaka jina la yule mzee wa vijisenti, tulimfanya nini?. Anachofanya ZZK sio tuu kutaja majina ya wenye fedha Uswiss, kama ni fedha tuu, wengi sana wameweka huko kwa sababu ndio safe ila sio wameficha.

Kuwa na fedha uswiss sio kosa kisheria kosa ni fedha hizo zimepatikanaje?, ndio maana mzee wa vijisenti baada ya kukutwa na tule tujisenti alihojiwa, wakaridhika mpaka leo mzee anatesa na tujisenti twake!.

Anachofanya ZZK sio issue ya majina tuu, kama ni majina tunayo mpaka humu jf yameishawekwa, kazi ni hizo fedha zimetokea wapi mpaka zikatua uswiss?. Watu hawabebi fedha kwenye magunia kwenda ku bank cash kama vijana wa Bhahresa, fedha hizo za Uswisi zimepatikana kwenye deal fulani na zikapigwa huko juu kwa juu, jee ni deal gani hizo?, hapo ndipo ZZK amejitolea kuisaidia serikali ya Tanzania kujua kama ni kweli serikali inayo nia ya dhadi ya kujua kwa sababu sehemu ya wenye fedha hizo ni waserikali!.
P.
 
Mkuu umeuliza vema, ukweli ni kwamba kwa sasa hamna hatua tunayoweza chukua lakini itoshe tu kusema mbali na uwezo tuliojaliwa wana Chadema, tunapata kuungwa mkono zaidi pale panya CCM wanapofichuliwa. Na hatua kubwa itakuwa kuwaondoa madarakani 2015.

ZZK should be fired
 
Matokeo halali ni yale tuu yanayotangazwa na Tume, na mshindi ndio anakuwa mshindi halali kwa utaratibu wa "the end justifies the means!".
P.

Pasco acha utani Tume yenyewe ni ya CCM mbona kusiwe na tume huru? Ni kweli unayoyasema kuwa mshindi ni yule anayetangazwa na Tume. Hebu tutafakari are the "means" you are referring even in line with the documented CCM ideology? yaani wewe unahalalisha matumizi ya mbinu chafu ili mradi ushindi upatikane ni sawa tu mkuu? Hakika Tume ingekuwa si chombo cha serikali ya CCM wengi wangekuwa na imani na kazi yake.
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi Chadema ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.

Nikikuita mchumia tumbo nitakuwa nakutusi ,si vyema kufanya hivyo. Jitafutie jina sahihi mwenyewe.
Wachambuzi wa siasa wanajua fika umaarufu wa Zitto umetokana na yeye kufukuzwa bungeni na Sitta alipokuwa spika, uma wa Watanzania ukafunguka macho kutokana na uonevu ule. Hapo ndipo Zitto alipopata umaarufu .

Suala la ability unalosema wewe ni nadharia zaidi,Zitto ni kigeugeu sana amepingana na mambo mengi sana kuhusu chama chake hadharani kwa maslahi binafsi. Mchambuzi gani makini asiyejua kwamba hoja ya fedha za uswiss Zitto alikuwa anapewa data na B. Membe .Alikuwa anatumika kwa maslahi ya Membe na kundi lake ili kwachafua kiina EL!

Navyojua watu kama Mnyika,Lissu,Nyerere(MP) ,Mdee na wengine wachache wanapata umaarufu kwa ability sio kwa kufukuzwa bungeni kama Zitto na kujiona yeye ni maarufu kuliko wananchi tunaom-support.

Zitto mara zote anajenga hoja kwa minajili ya kujinufaisha yeye akibeba kivuli cha maslahi ya umma. Alivyopiga kelel kuhusu madini ,kampunii za madini zilidivert misaada akapelekewa yeye jimboni kwake. Huu ni ukigoma na sio ability jipange upya mkuu Pasco
 
Last edited by a moderator:
CK zote kuni ikijitenga na ingine itazimika na nguzo ya umeme ikiwa mbali na ingine waya utalegea tu. namshauri ZITTO atubu ndipo arudi kundini
 
CK zote kuni ikijitenga na ingine itazimika na nguzo ya umeme ikiwa mbali na ingine waya utalegea tu. namshauri ZITTO atubu ndipo arudi kundini

Mkuu una busara kweli. Lugha hii ya picha inatosha kumtoa PASCO kimasomaso.
 
Pasco acha utani Tume yenyewe ni ya CCM mbona kusiwe na tume huru? Ni kweli unayoyasema kuwa mshindi ni yule anayetangazwa na Tume. Hebu tutafakari are the "means" you are referring even in line with the documented CCM ideology? yaani wewe unahalalisha matumizi ya mbinu chafu ili mradi ushindi upatikane ni sawa tu mkuu? Hakika Tume ingekuwa si chombo cha serikali ya CCM wengi wangekuwa na imani na kazi yake.
Mkuu Makundi, hakuna ubishi "the playing field is not level"!, mnagombea kisu mmoja ameshika kwenye mpini na mwingine kwenye makali!. Ila kabla ya mchezo, wote mlikubaliana kuhusu rules of the game, na kutian saini kukubali matokeo yoyote hivyo kipenga kikapulizwa na game ikaanza!, baada ya kujua umeshindwa, kwa sababu the playing ground is not level and rules of the game zilipindishwa kumfavour opponent wako, siku ya kutangazwa matokeo ulitakiwa ujitokeze to tell it infront of their faces tha "it was not a fair game!", wewe ulioshindwa ndio kwanza unanuna, unasusa!.

Uchaguzi ni kama vita, kuna sheria za vita, suala la mbinu za ushindi zikiwemo tactics ni siri za jeshi lako lengo kuu likiwa ni kupatikana ushindi, kwa mbinu safi au chafu ikiwemo infiltration ndani ya kambi ya adui kisha kuwa piga surprise ambush!. Ukisha shinda ndio umeshinda, mbinu ulizotumia doesn't matter any more, kinachomatter ni ushindi tuu, ndio maana nikasema "The end justifies the means!". And The winner takes it all!" leaving the losser "Standing small!".

2015 tunaingia kwenye game nyingine, timu zile zile, watu wale wale ila this time manahodha watabadilika na tutaset new rules of the game ila uwanja ni ule ule na haujasawazishwa!. Once beaten twice shy!. Mpaka sasa wenzenu wako busy ku train, nyinyi mnacheza makida makida, kipenga cha 2015 kitapulizwa tena, mtaingia tena kwenye game, mtapigwa tena kwa kukosa maarifa!. Jee this time around mtalalamika tena au mtasusia tena?!.
P.
 
Nikikuita mchumia tumbo nitakuwa nakutusi ,si vyema kufanya hivyo. Jitafutie jina sahihi mwenyewe.
Wachambuzi wa siasa wanajua fika umaarufu wa Zitto umetokana na yeye kufukuzwa bungeni na Sitta alipokuwa spika, uma wa Watanzania ukafunguka macho kutokana na uonevu ule. Hapo ndipo Zitto alipopata umaarufu .

Suala la ability unalosema wewe ni nadharia zaidi,Zitto ni kigeugeu sana amepingana na mambo mengi sana kuhusu chama chake hadharani kwa maslahi binafsi. Mchambuzi gani makini asiyejua kwamba hoja ya fedha za uswiss Zitto alikuwa anapewa data na B. Membe .Alikuwa anatumika kwa maslahi ya Membe na kundi lake ili kwachafua kiina EL!

Navyojua watu kama Mnyika,Lissu,Nyerere(MP) ,Mdee na wengine wachache wanapata umaarufu kwa ability sio kwa kufukuzwa bungeni kama Zitto na kujiona yeye ni maarufu kuliko wananchi tunaom-support.

Zitto mara zote anajenga hoja kwa minajili ya kujinufaisha yeye akibeba kivuli cha maslahi ya umma. Alivyopiga kelel kuhusu madini ,kampunii za madini zilidivert misaada akapelekewa yeye jimboni kwake. Huu ni ukigoma na sio ability jipange upya mkuu Pasco
Mkuu Mwakalinga, uko sahihi, hujanitusi na hilo ni jina sahihi kwangu!. Thanks.
Pasco.
 
Mkuu una busara kweli. Lugha hii ya picha inatosha kumtoa PASCO kimasomaso.

Hivi Pasko akiulizwa kati ya ZZK na NASSARI nani zadi yani hapo hata LEMA anamzidi ZITTO AMECHOKA ANATAKIWA AJIPIME ATAFAKARI NA AJIREKEBISHE TOFAUTI NA HAPO HATA JIMBO LAKE ATALIPOTEZA
 
One cannot be a hero to everybody!.
Shujaa wa mimi ni bomu kwa mwingine!.
Hata alichokifanya Osama huku wengine wakimlaani lakini wengine ndiyo shujaa wao!.

Ukweli unabaki kuwa ZZK ni role model wa vijana kibao!.

Nimependa kuanza na maneno hayo hapo juu, na fikiri watu wa Kigoma Kaskazini humu Jf hawafiki hata 500, lakini kumbuka ni kura ngapia kijana huyu alipata huko kwao wakati wa uchaguzi uliopita?

So watanzania tuwe tunasimamia kwenye ukweli tusipende mambo ya kwenye migahawa kuna wakati fulani zkk alisha shambuliwa kwa kumuwajibisha waziri fulani watu walimshambulia sana humu jf, ila baada ya muda madam spika alikuja kumuumbua waziri huyo sikuona pongezi kwa kijana huyu hapa Jf.

Pili Jf si wapiga kura wa zkk kama jf ingekuwa na nguvu hizi na imani hata rais angekuwa ameshajiondoa kwenye madaraka yake hivi sasa, na fikiri kwa kuwa haya ni mawazo yako si vema kuyapinga ila tunayaboresha tuu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi hii, Jf kwanza tunahitaji kubadilika kwa kuwa siku hizi jf imekuwa kama kijiwe cha kahawa kwani mijadala inaindeshwa kutokana na kila watu wanacho kiona kwa wakati husika.

Ipo haja ya kunadilika kama tunahitaji jf kuwa chanzo cha mabadiliko na marekebisho ya nchi hii kwa wanachama wa mtandao huu kuwa makini katika kuandika hoja na kuchangia pia, kwani hivi sasa tunatumia muda mwingi sana kupiga soga kuliko kurekebisha matatizo katika taifa hili.

kuna mambo mengi sana yanatokea kila kukicha na kuna wezi wengi wanaiba kila kukicha na fikiri ni wakati wa jf kuweza kujadili kuhusu watawala na si watawaliwa, kwa kuwa hadi hivi sasa wananchi na chadema bado tupo chini ya utawala wa wanyonyaji wakuu ccm.

Ni vema kutumia muda wetu kuhakikisha ccm wanatupisha kwa kuwa muda wa utawala wao na kutuibia umetosha, lakini naona watu wa chadema wanapoteza muda kurushiana maneno na kusemana vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa hoja zinazo anzishwa na vibaraka wa ccm.

Sidhani kama zkk angekuwa ni tatizo hadi sasa chama kingekuwa kimetulia kama kilivyo, then kwa nini sisi washabiki na wanachama tupoteze muda, hebu tungojeni majibu kutoka kwenye chama kuhusu jambo hili, na sisi muda huu lazima tuhakikishe tunajadili na ku post mambo ya msingi kwa kuanzia hebu kuanzia leo tujaribu ku post mambo kama haya tuone nini kitakuwa ni majibu toka ccm kabla ya mwisho wa mwaka huu kwa kuwa na fahamu fika muheshimiwa msema hovyo wa chama tawala na katibu mwenezi wa chama tawala ni wanachama wa Jf wataweza angala kutupa majibu husika. Hivyo kama member wa Jf na penda kuona tunamaliza mwaka kwa kuhoji mambo ya msingi yenye tija ya taifa hili.

Kwa kuanzia hebu tujaribuni ku post na hata kurudisha zile post za kale zilizo kuwa zinahusika kwenye kashfa hizi hapa chini

1. Je twiga walipitishwa vipi pale Kilimanjaro airport na nini kimefanyika mpaka sasa kuhusu swala hili?

2.Je meremeta ili kuwa chini ya JWTZ kweli au kuna jambo limefichwa?

3.Kama watu walioa fanya uporaji na kule serengeti ilichukua siku 5 kuwa mikononi mwa dola vipi hawa walio kuwa wanatuibia pesa zetu watanzania hadi sasa wameshindikana huu mkono wa dola mbona umekuwa mfupi?

4. Maisha bora kwa kila mtanzania na hoja za mabadiliko ya uwongozi wa chama tawala ni kweli utaleta mabadiliko?

5.Barabara za mikopo je ni sahihi kuzitumia kama ndio sifa ya utawala wa miaka 51 ya uhuru wa nchi hii?

kama kuna mengine unaweza weka ila mimi naona mambo haya ndio tunapaswa kujadili sana humu ndani jf ili vidudumizi wakipita wakawape taarifa mabwanyenye wao.

Nawasilisha
 
P[B said:
asco;5310234]Matokeo halali ni yale tuu yanayotangazwa na Tume, na mshindi ndio anakuwa mshindi halali kwa utaratibu wa "the end justifies the means!".
P.
[/B]

Kama MATOKEO YA TUME NDIO HALALI basi Kafumu hakufumuliwa na Aeshi ni mbunge
 
kama ni rol modo je Lema ni nani Nasari je ni nani Mdee je Mnyika je T LISSU JE ACHA UZUSHI ZZK AMECHOKA HANA LOLOTE
 
Back
Top Bottom