Zito abadili dini

Zito abadili dini

Hongera Zitto kupata Mchumba, kama ni kweli unakaribia kuvuta jiko basi mchango wangu ni 500,000/. Haya ya dini its too personal tatizo la wa TZ hawana dogo sisi ndugu yangu tunataka kuserebuka tu.
 
Zitto hajui baba yake kama alikuwa Mkristo au Mwislamu. Anatumia majina ya ukoo wa mama. Nijuavyo mimi ndini ni kati ya Mtu na Mungu wake na sie wa pembeni hatupaswi kuropoka ovyo ya Mtu na Mungu wake.

Makubaliano ya Mtu na mke wake yanabaki kuwa yao na si vinginevyo. Asiyeamini hayo atwambiye yake na mke wake wanyofanya huko chumbani kila mtu ataumbuka.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Hatimaye mbunge machachari wa kutoka Kigoma, muheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ameamua kubadilisha dini yake kutoka kwenye uislamu kuelekea kwenye ukatoliki. Vyanzo vya karibu na muheshimiwa Zitto vimeeleza kwamba, sababu ya bwana Zitto kubadilisha dini ni sababu binafsi na wala siyo za kichama kama inavyodhaniwa na wengi. Inasemekana ndugu Zitto ana uhusiano wa kimapenzi na msichana wa kikatoliki ambaye ndiyo chanzo kikubwa cha muheshimiwa huyo kuachana na uislamu na kuwa miongoni mwa kondoo watakaookolewa na bwana yesu. Kama ambavyo bwana yesu alisema kwamba "mimi ndiyo njia ya kuelekea kwa baba", inasemekana kwamba muheshimiwa Zitto amekubaliana na mpenzi wake wamwabudu Mungu kwa kupitia njia hiyo. Ingawa kuna miongoni mwa wakereketwa wa chadema wamesikika wakinung'unika kwamba hii ni janja tuu ya bwana Zitto ili aweze kukwapua madaraka ya juu kabisa ya chamahicho. Chama hicho ambacho kina wafuasi lukuki katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kimekataa kukanusha au kuthibitisha habari hizi.

Sio kuwa ili uwe president wa CHADEMA lazma uwe Mkatolic? Kama ni kweli itakuwa unauvizia uenyekitiki, maana wakati ule alipotaka kugombea walimtoa nduki. wenye akili tulishajua sababu ndo maana hata maaskofu hawakulaani uvunjifu ule wa demokrasia!!!

Karibu Catholic Zitto!!!!!!
 
Zitto never was muslim and his conversion won't make difference to religion!
 
Hongera Zitto kupata Mchumba, kama ni kweli unakaribia kuvuta jiko basi mchango wangu ni 500,000/. Haya ya dini its too personal tatizo la wa TZ hawana dogo sisi ndugu yangu tunataka kuserebuka tu.

Watanzania malimbukeni kweli, yaani kwenye harusi ndo mnaona pa kuchangia kiasi kikubwa hivyo halafu kwenye maafa ndo mnatoa mia tano sijui aliyeyeturoga ni nani kwa kweli duh
 
huyo dada anapesa sana!ana NGO yake hivyo ZITTO ndiye anayelelewa kwa mahitaji ya kimaisha!hata hivyo ni aibu kwa mwanaume kulazimishwa kufuata dini ya mwanamke,mwanamke ndie anatakiwa afuate ya mwanaume maana anaenda kwenye ukoo wa KABWE!kwangu mie naona ZITTO HANA MSIMAMO BURE KABISA HUYU JAMAA

Bongolalaaaa!! Endelea kulaza ubongo baba!!
 
mambo mengine ni yake binafsi, abadili asibadili hayatuhusu, jambo la msingi aendelee kuwa mpiganaji wetu, na hilo ndilo jukumu lake,

iko siku mtu atakuja na mada yanye kichwa," ZITO KATOA SADAKA"

leteni mada za maendeleo
 
Huyu jamaa isije kua anataka pesa ya baba mkwe tuu , ni yule demu mtoto wa tajiri mkubwa hapa TZ nini ambaye jama alifanya ki intenshipu kwenye kampuni ya babaye?
 
uchi ni 1 ya sababu inayomfanya mtu abadili dini yake.sasa mwanamke tu anakupindisha.je? Tukikupa nchi c utaiuza.kama ni kweli yaani atakuwa bonge la zoba ila kama umefuata maslahi wewe tu imani yako ila mpaka kufikia hapa hatakuamini tena.
 
Kama Zito kaingia Ukatoliki sababu ya mwanamke, basi hakuwa na dhamira ya kweli ya kumfuata Yesu.

ndugu mie naomba kwenda kinyume na manenoyako kwakuwa mtu anaweza kufundishwa na mtu yeyote au kujuzwa na mtu yeyote ili afahamu jambo. zito inawezekana kabisa kupitia huyo ndiyo kaweza kumjuwa Yesu ya kuwa ni mwokozi wake!.

mtu anaweza kupotezwa na mwenza wake na asiende mbinguni kwa kushauriwa waishi kinyume na taratibu za imani furani, pia anaweza kwenda mbinguni kwa kushauriwa na kufundishwa na mwenza wake!

yote yanawezekana!
 
Amefuata dini rasmi ya Chama CDM!
Maana watu walikuwa hawana imani nae hapa wakimuona msaliti! Afadhali sasa wataweza kumwamini na pengine kumpa uenyekiti!

Hivi Ndesa au Mtei hawana binti wampe? ingerahisisha zaidi safari yake ya uenyekiti!

Mimi najitolea kukufundisha kinanda Mh. Zitto!
 
Amefuata dini rasmi ya Chama CDM!
Maana watu walikuwa hawana imani nae hapa wakimuona msaliti! Afadhali sasa wataweza kumwamini na pengine kumpa uenyekiti!
Hivi Ndesa au Mtei hawana binti wampe? ingerahisisha zaidi safari yake ya uenyekiti!!

Au yule Laizer anaweza kumpa yule binti yake wa Ngaramtoni maana sasa amekuwa Mchadema kamili
 
Hii hoja si ya kuichukulia kilaini. Mwandishi unaönekana syesyemu pyua, ili kuwahadaa watz kuwa CDM cha wakatoliki. Badilika.
 
Jamani msibadilishe JF jukwaa la udaku au kijiwe cha wahuni. Njooni na hoja madhubuti.

Mambo ya person ya nini humu! Tuchangie maendeleo wajameni
Kuna mada nyingi zakuongelea hapa mimi nawaombeni wandugu leteni mada za maendeleo ili watu wajenge hoja Tanzania isonge mbele!
 
Hizi habari zina walakini nazani ni zakutaka kujenga hoja kuwa chadema chama cha kidini hii si kweli zitto bado muislam swafiiiii
 
is vere personal issue, hivi Lipumba ameshambadilisha dini jojina? why yes and why not? kwa sababu dini is vere personal issue ya mtu. period!!
 
.....issshiiiiiii! kumbe udaku + Gossips......!
 
This has nothing to do with politics kama mleta hoja unavyotaka ieleweke watu tumeanza kubadili dini muda mrefu hata kabla ya CCM na CDM kuwepo, ikiwezekana omba Mods wabadili heading ya thread.

Thread ni kweli iwekwe vizuri kwani kutumia neno kusalimu amri haijakaa vema
 
Back
Top Bottom