Zipo faida na hasara za kutofungamana na upande wowote

mrdocumentor

Member
Nov 27, 2021
43
53
Toka tupate uhuru wa nchi yetu mwaka 1961 nchi yetu imekuwa na sera kuu ambayo inaendelezwa hadi sasa ambayo asili ya sera hiyo ni (NAM) Yaani Non Aligned Movement, sera hii ilikuwa imetawala Sehemu kubwa ya dunia hususan katika Bara letu la Afrika na nchi za mashariki ya kati

Kwa nchi kutofungamana na upande wowote wakati mwingine huonekana ni suala jema lakini pia upo wakati ambao suala hili huonekana kuwa na athari hasi na hali hiyo hutokea kutegemeana na ajenda yenyewe iliyoko mezani.

FAIDA
Kwa nchi kutofungamana na upande wowote kuna faida kubwa kulingana na hoja ambayo nchi inatakiwa kutoa msimamo wake Mfano pale ambapo Ukraine ilipoingia kwenye matatizo na Urusi yaani Urusi aliposhutumiwa kuvamia eneo ambalo Ukraine walikuwa wanadai ni la kwao na matokeo yake vita ilitokea. Tuliona nchi mbalimbali duniani zikitoa msimamo wake juu ya mwenendo wa hiyo vita na kuweka wazi wao wapo upande gani.
Mfano nchi za Afrika mashariki yaani Kenya na Uganda ziliweka wazi pia lakini Tanzania tuliendelea na sera ambayo kwa sasa ni kama mila ambayo tulirithishwa ya kutofungamana na upande wowote. Kwenye hili faida ipo kwa sababu kama nchi inatuweka mahali salama zaidi kwenye upande wa diplomasia kwani ushirikiano wetu utadumu kwa pande zote.

HASARA
Hakuna jambo lenye faida likakosa hasara kwenye macho na upeo wa kibinadamu. Hii hali ya nchi kutounga mkono au kukataa hoja iliyopo kwenye pande mbili tofauti inaweza kuwa na matokeo hasi kwenye baadhi ya hoja pia.

Mfano; Mkakati wa mapenzi ya jinsia moja ulianza zamani na hapo mwanzo ulikithiri zaidi maeneo ya nchi za magharibi Lakini kwa sasa hali imezidi kuwa mbaya kwa Afrika pia lakini hata hapa kwetu Tanzania mambo si mazuri hata kidogo. Katika ajenda Kama hii kama kiongozi Unaweza kutamani kukataza ili suala na kuanzisha kampeni za kupinga ili suala ikiwa tu nchi yako haina sera ya NAM Kwa sababu kama utafanya hivyo ni wazi utaonekana upo upande wa wale wanaopinga ndio maana umeona Rais wa kenya amelipinga hilo hadharani.

Vipi kuhusu sisi, na katika hili pia hatufungamani na upande wowote?

Kama ni hivyo tafsiri yake ni kwamba Hatuukubali ushoga lakini pia Hatuukatai Ushoga Si ndio?
 
Kuna Viongozi wakubwa sana hadi sasa hawaungi mkono wala kupinga mchakato wa kubinafsisha Bandari za Tanganyika …wao wanasubiria tu tamko la Bi Mkubwa watambae na biti
 
Kuna Viongozi wakubwa sana hadi sasa hawaungi mkono wala kupinga mchakato wa kubinafsisha Bandari za Tanganyika …wao wanasubiria tu tamko la Bi Mkubwa watambae na biti

Na tatizo ndio limeanzia hapa
 
Back
Top Bottom