Zimamoto yatoa stika

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,971
3,827
Kama ilivyo kwa taasisi nyingine ambazo zinahusika na vyombo vya usafiri kuwa barabarani kati hali ya usalama na uhalali idara ya ZIMAMOTO maarufu kama FIRE nayo imetoa stika kwa ajili ya vyombo vya usafiri.

Kwa mikoa mingine tayari stika hizo zilikuwepo ila kwa DAR ndo sasa zimeanza kuonekana.
Tumeona taasisi kama TRA (mapato & road licence), SUMATRA, POLICE (nenda kwa usalama), BIMA, MANISPAA wakitoa vibandiko hivyo kwa gharama tofauti ZIMAMOTO nao wamejiunga na "riadha hii" (join the race).

KERO KUBWA NI NAMNA MSAKO NA UKAGUZI WA STIKA HIZI UNAVYOFANYWA ...... ! MAGARI YA ABIRIA KWA DAR NDIYO WAATHIRIKA WA MISAKO HII PEKEE....!

UTAWAKUTA KWA WINGI KWENYE VITUO VYA DALADALA...WHY...?
 
Hivi hizi stika hasa ni kwa ajili ya nini na watatungazia wamepata kiasi gani na wmezitumiaje?.
 
Kwakweli Nchi hii ni ya ajabu kweli! Kila kukicha unzuka usanii wa kutengeneza pesa (walianza na mikanda) speed gavana, sicker za usalam barabarani na sasa sticker za zimamoto!

Cha ajabu hawa watu wanalazimisha eti saloon car lazima iwe na mtungi wa lita moja! hivi wanataka kutuambia hao waliotengeneza magari na wakaweka fire extinguisher humo ndani ni wajinga?

Hapa huu ni mchongo wa kutengeneza pesa!

Na hizo sticker zinozongezeka kwenye vioo kila kukicha iatafika mahali kioo kitakuwa giza!
Hawa jamaa ni mara ngapi wanaitwa kuzima moto wanafika wamechelewa au gari halina maji? sasahivi wanashinda barabarani kukumata magari nakulazimisha kunua sticker! hivi nchi tetu inakwenda wapi?

Je ni sehemu ngapi muhimu ambazo zinazostahili kufanyiwa ukaguzi wa vifaa vya kuzimia moto na hawa waunwana hawajafika?
 
Hapa huu ni mchongo wa kutengeneza pesa! ?

Nakuunga mkono, hiyo ni michongo tu!! Bado kupaka Teksi Rangi, mara daladala ziwe na Rangi. Mwisho mtaambiwa nyumba za Temeke zote Zipakwe rangi Nyekundu, za Ilala Rangi ya Kijani na Kinondoni Rangi ya Bluu.
 
Sasa kama mmeamua kubana epa bot

hela za kampeni za ccm zitapatikana wapi???
 
tena unakuta wanapokamata wanakuelekeza pembeni yao ukanunue hiyo mitungi ya kilo moja ambayo HAIONYESHI IMETENGENEZWA WAPI.....! TUME YA USHINDANI MPO....?
 
Hizo stika ni muhimu sana...
Mnataka mpaka watu wangapi wafe kwa moto ndo muone umuhimu?
Unajua wabongo mmezowea kuendeshwa kwa matukio!
Nunueni bila kelele bana, ni kwaajili ya faida yenu wenyewe...eboo!
 
Kipi muhimu hapa? Stika au fire extinguisher? Hiyo stika itakusaidia vipi incase moto ukilipuka kny gari?

We naona huelewi kabisa nini kinaendelea! Hawa jamaa hata hawakagui magari, wanachofanya wanauza stika tu, so unaweza ukaacha hata gari lako home ukaenda fire wanakupa stika.....ss what is the use? just making money for nothing?
 
Hizo stika ni muhimu sana...
Mnataka mpaka watu wangapi wafe kwa moto ndo muone umuhimu?
Unajua wabongo mmezowea kuendeshwa kwa matukio!
Nunueni bila kelele bana, ni kwaajili ya faida yenu wenyewe...eboo!

PJ, hizi stika zinalipiwa Sh.20,000/- kwa lazima, halafu Fire Extinguisher unaenda kununua mwenyewe.... Sasa hiyo Sh.20,000/- ni ya nini???
 
Wenzetu mlioko huko nje je manadaiwa kuwa na hizi fire extinguishers kweneye magari? Mbona tunanunua magari toka ujapani na vitu vyote standard vinawekwa execept reflectors na hizi FE?Ni matukio managpi ya moto yametokea kuleta hii precedence?.
 
........ni majuzi tu nilipaki gari juani an kablam! fire extinguisher likalipuka an kunichania seat covers...
 
Hizi stika zinasaidia nini? Au ndo kuuchangia zima moto?
Zinafaida yoyote unapoweka kwenye kioo? Lengo haswa nini kuweka hizi stika?
 
Kama ilivyo kwa taasisi nyingine ambazo zinahusika na vyombo vya usafiri kuwa barabarani kati hali ya usalama na uhalali idara ya ZIMAMOTO maarufu kama FIRE nayo imetoa stika kwa ajili ya vyombo vya usafiri.
kwa mikoa mingine tayari stika hizo zilikuwepo ila kwa DAR ndo sasa zimeanza kuonekana.
tumeona taasisi kama TRA(mapato&road licence),SUMATRA,POLICE(nenda kwa usalama),BIMA,MANISPAA wakitoa vibandiko hivyo kwa gharama tofauti ZIMAMOTO nao wamejiunga na "riadha hii" (join the race)
KERO KUBWA NI NAMNA MSAKO NA UKAGUZI WA STIKA HIZI UNAVYOFANYWA ...... ! MAGARI YA ABIRIA KWA DAR NDIYO WAATHIRIKA WA MISAKO HII PEKEE....!
UTAWAKUTA KWA WINGI KWENYE VITUO VYA DALADALA...WHY...?

wiki iliyopita nilishuhudia hilo zoezi kwenye ofisi za hao zima moto, hamna kukagua gari wala nini. toa hela upewe stika na uchape mwendo. wanachojali wao ni pesa na si usalama kwani hawakagui gari wala nini.

Kabla ya kwenda huko nilitembelewa na jamaa aliedai katoka huko, hana kitambulisho wala nini, na hakuwa na uhakika na fee pia. nikakomaa nae tukaelewana. baadae kanipigia eti niongeze cha juu na tutagawana nikasema poa. (nikiwa na nia ya kumkomoa kwa kwenda kulipia ofisini na si vichochoroni). Mind you this guy never inspected hata kama nin FE....

nilikwenda kwa ajili ya kupata certificate kama hiyo kwa ajili ya food court. nikaambiwa subiri afu mara wakaulizana bei, mara wakanitafutia chumba niingie, mara subiri tena mara nikaitwa nje tukashuka ngazi na kuna sehemu kuna giza hivi, muhusika akaniambia nimwachie laki 3 niende afu nirudi baadae itakua tayari.

nikamwambia hapana nitarudi baadae when they are ready, nikamwomba mdosi wangu ajitose na yeye kwa kuwa sasa hata gharama halali sikuijua.

Mzee alipoenda na akaomba kuonana na mkuu na akachomekea hilo swali,akaambiwa aahh mbona hiyo ni 50,000 tu!!!!!!!!!!
 
Mimi nafikiri kuan umuhimu wa kuwa na chama cha wenye magari binafsui lol huu ni uonevu kabisa sasa uuziwe stika alfu 20 wakati ndani ya gari huna hiyo zimamoto stika ndo itazima moto ukitokea? hawa bwana naona ndio maana hawajazitangaza kama wanavyofanya wiki ya nenda kwa usalama ah mie ningegoma hadi wanipe maelekezo vizuri

Usiponunua faini yake ni ipi?
 
Kama vile si watanzania ninyi! kwani hamjui hizi 20 thou ni za nini! Si za kumlipa aliyepewa tenda ya kutengeneza stickers? ukiweka na 10% aliyekuja na wazo, 10% ya aliyetoa tenda, 10% watakaoendesha zoezi...hamuoni hata hiyo 20 thou inaweza isiwatoshe?! Nani kasema hii sticker ni kwa manufaa ya wenye magari? Si mnalalamika kodi nyingi? Zinatafutiwa majina mapya tu! Maisha bora kwa kila mdanganyika hayo.
 
Wenzetu mlioko huko nje je manadaiwa kuwa na hizi fire extinguishers kweneye magari? Mbona tunanunua magari toka ujapani na vitu vyote standard vinawekwa execept reflectors na hizi FE?Ni matukio managpi ya moto yametokea kuleta hii precedence?.

Wizi mtupu!!!!!

Tiba
 
Tatizo bongo kuanzia serikali mpaka wananchi kila mtu ni ujanja ujanja tu. Walianza na spidi gavana, baada ya kuona ajali nyingi, na ilitungiwa mpaka sheria matokeo yake ajali zimezidi na wamekaa kimya na hata spidi gavana hawaiongelei tena. Sasa hizi stika za zimamoto zina faida gani kwa nchi na wananchi?. Njia pekee ya kujustify vi-collection kama hivi ni kuboresha huduma za jamii, leo hii Magari mangapi yanaungua mpaka kuwa majivu mita 200 toka kituo cha zimamoto?.

Hii sasa ni lazima wananchi tuoneshe kuwa sisi si shamba la bibi. ni bora kuwa na wafanyakazi wachache serikalini walipwe vizuri na kuwa na huduma bora kuliko kuwa na group wa anandugu wanaoajiriwa kwa vi-memo huku hawana wanalolijua katika nchi zaid ya kusubiri mishahara
 
Hizo stika ni muhimu sana...
Mnataka mpaka watu wangapi wafe kwa moto ndo muone umuhimu?
Unajua wabongo mmezowea kuendeshwa kwa matukio!
Nunueni bila kelele bana, ni kwaajili ya faida yenu wenyewe...eboo!

Sikujua kama stickers ndo zinazima moto! Looh!
 
Back
Top Bottom