Tar 04 Nov 2009, nikiwa maeneo ya kituo cha daladala mwenge, na-endesha gari kuelekea Posta, nikitokea Sam Nujoma, mara napigwa mkono, na trafiki POLICE!. Kama kawaida yao, nikaambiwa niegeshe kushoto!.
Mama weeeee!!. Mara anakuja trafiki POLICE wa Kiume, kwa bahati mbaya , sikuchukua namba yake. Fuatilia mazungumzo yetu hapo:
POLICE TRAFIKI (PT): Sticker ya fire iko wapi?
SISIMIZI: Sina!
POLICE Trafiki: Ndiyo tunawataka, watu kama ninyi!
Sisimizi: Kivipi?
PT: Huoni gari hiyo STK (Landcruiser) iko kwenye operesheni hii?
Sisimizi: Ok!
PT: Haya nionyeshe fire extingusher (Kifaa cha zima moto)
Sisimizi: Hiki hapa!
PT: Ok! Una habari kwamba jeshi la zima moto limepiga marufuku aina hii ya kifaa cha zimamoto na unatakiwa ununue za Powder za Kilo moja ,1kg?
Sisimizi: Sina habari!
PT: Ok! Sasa wewe, umekumbwa na oparesheni!
Sisimizi: Ok!
PT: Unaelewa faini yake?
Sisimizi: Sielewi!
PT: Ni TZS 20,000 + 20,000 ya kununua kifaa kipya!
Sisimizi: Ok! Lakini kwa bahati mbaya sikutembea na pesa hiyo yote, siku ya leo!.
PT: Ndiyo maana ya Oparesheni!. Haya lete TZS 5,000 nikuachie uchomoke kabla sijakuchomekea kwa watu wa fire brigedi!!.
Sisimizi: Ndg, unamaanisha rushwa?
PT: Hapana, namaanisha senti ya maji ya kunywa!. Fanya haraka kabla sijakuchomekea kwa mama (Askari wa jeshi la zimamoto wa kike)!. Ukitia mguu kwake hautoki!
Sisimizi: Poa nichomekee tu!
PT: (Kwa sauti kubwa) Afande, njoo umsikie huyu raia!, (anamwita askari wa kike wa zimamoto).
Askari Zimamoto (Wa kike): Umeshindwa kumalizana naye??. Chukua fomu hii (napewa fomu ya kujaza). Nenda kalipie pale kwenye STK (Landcruiser)!.
Sisimizi: (Nachukua fomu kwenda kulipia TZS 20,000 ya sticker, nakurejea kuibandika kwenye gari).
PT: Yaani umeingia gharama 20k kwa ubahili wako!. mbona, haujanunua fire extingusher?
Sisimizi: Nimeelekezwa kwenye gari, ninunue ndani ya muda mfupi ujao!
PT: (Anaachana nami na kuendelea na kamatakamata!!)
WITO: PCCB wamlike oparesheni za jeshi la zimamoto! Limeanza kuzima moto wa kupambana na rushwa!