Uchaguzi 2020 Zijue sababu kuchelewa vikao Kamati Kuu ya CCM kupitisha Wagombea wa Ubunge

Ratiba za kichama hapa Makao Makuu Dodoma zinaonesha kuwa vikao vya Kamati Kuu wa CCM almaarufu kama CC vilipaswa kufanyika tarehe 7 na 8 ya mwezi huu. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichoketi hapa Dodoma au hata Dar es Salaam. Ajenda kuu ya kikao hicho ni kupitisha majina ya Wagombea wa Ubunge wa Majimbo wa CCM Tanzania Bara na Visiwani.

Zipo sababu mbili zilizochelewesha vikao vya Kamati Kuu. Kwanza, kuna tuhuma lukuki za rushwa kwenye mchakato wa kura za maoni majimboni. Taarifa zimemiminwa CCM kutoka TAKUKURU, waliogombea, makada hadi wananchi wa kawaida kuhusu vitendo vya rushwa kwenye kura za maoni chamani. Kamati ya Maadili ya chama imeelemewa na makabrasha ya tuhuma kutoka karibu kila mkoa wa Tanzania.

Katika hilo la rushwa, kuna wakubwa chamani wanataka itumike FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE katika kupata suluhu la jambo hilo. Yaani, rushwa isionekane kwenye macho ya wanaKamati Kuu na hivyo wagombea waangaliwe kwa vigezo vinginevyo kama kukubalika na si rushwa. Inapendeezwa kuonwa kuwa wagombea walizidiana dau wenyewe kwenye majimbo yao. Kuna mvutano mkubwa kwenye Kamati ya Maadili na hata baina ya viongozi waandamizi wa chama.

Sababu ya pili ni sauti za makada na wananchi kuhusu nani arudishwe wapi kugombea. Kuna waliokataliwa majimboni lakini wanatakiwa uongozini; kuna waliopita majimboni lakini hawatakiwi chamani na uongozini; kuna waliokataliwa lakini wanatakiwa huko huko majimboni. Kamati Kuu imetumia muda wa kutosha kutega masikio yake huko site ili kujiridhisha kabla ya kufanya uamuzi wake. Je, waliokatwa wataandikwa tena?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwa sasa jijini Dodoma)
CCM na rushwa ni mama na Baba
 
Nakubaliana na wewe kuwa kama serikali imeamua kupiga vita rushwa ni lazima ifanye hivyo kwa vitendo. Inapobainika kuwa mshindi wa kura za maoni alitoa rushwa na akawa wa kwanza na katika wale aliowashinda wako watu safi ambao hawakutoa rushwa uamuzi unakuwa rahisi kuwa yula aliyetoa rushwa anakatwa na yule ambae hakutoa ndiye anayeteuliwa kuwa mgombea.

So far so good, tatizo linatokea pale wagombea wote wametoa rushwa na hiyo imedhihilika isipokuwa wamezidiana kete katika viwango walivyotoa!! Sasa hapo utamteua yule aliye honga kidogo na kumuacha yule aliyetoa dau kubwa au utamteua yule aliyetoa dau kubwa na kushinda?

Nimkumbushe kidogo mzee wa mafaili kuwa katika Uchaguzi za ccm huko nyuma hali kama hii iliwahi kujitokeza katika majimbo fulani fulani hivyo kuna precedent kama wanataka kazi yao iwe rahisi. Uamuzi wa wakati ule ulikuwa, kwavile wagombea wate walijulikana Kuwa walihonga na tofauti Yao ni dau walilotoa basi yule aliye shinda kura za maoni ndiye aliyeteuliwa kuwa mgombea.
Hakuna kitu kama hicho, na wewe acha kupotosha..kama una mfano wa jimbo au kata ambapo wagombea wote walihonga wajumbe taja hapa ni jimbo gani au kata gani, tusiongee nadharia jamani mambo yote yanafahamika, katika kila jimbo na kata wapo wengi tu ambao hawakutoa hongo kabisa hata senti kwa mjumbe yeyote, wapo wengi tu! acheni kugeneralize
 
CCm kama wasemavyo ina wenyewe na wenyewe wanakuambia mkono mtupu haulambwi!! Ili uchaguliwe huko ccm ni lazima kuhonga hata JIWE analijua hilo na alihonga sana alipokuwa mbunge!! Hivi sasa anawahadaa watu tu!!! Ulizia wenyeji wa Chatto wakupe historia ya ubunge wake.
 
CCm kama wasemavyo ina wenyewe na wenyewe wanakuambiwa mkono mtupu haulambwi!! Ili uchaguliwe huko ccm ni lazima kuhonga hata JIWE analijua hilo na alihonga sana alipokuwa mbunge!! Hivi sasa anawahadaa watu tu!!! Ulizia wenyeji wa Chatto wakupe historia ya ubunge wake.
Tatizo lenu ni kutaka mabishano ambayo hayasaidii kitu chochote, tunaongea hapa kura za maoni mwaka huu wewe umerukia kitu kingine kabisa..point ni kwamba si wote walioshiriki kura za maoni CCM walihonga wajumbe!
 
Ratiba za kichama hapa Makao Makuu Dodoma zinaonesha kuwa vikao vya Kamati Kuu wa CCM almaarufu kama CC vilipaswa kufanyika tarehe 7 na 8 ya mwezi huu. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichoketi hapa Dodoma au hata Dar es Salaam. Ajenda kuu ya kikao hicho ni kupitisha majina ya Wagombea wa Ubunge wa Majimbo wa CCM Tanzania Bara na Visiwani.

Zipo sababu mbili zilizochelewesha vikao vya Kamati Kuu. Kwanza, kuna tuhuma lukuki za rushwa kwenye mchakato wa kura za maoni majimboni. Taarifa zimemiminwa CCM kutoka TAKUKURU, waliogombea, makada hadi wananchi wa kawaida kuhusu vitendo vya rushwa kwenye kura za maoni chamani. Kamati ya Maadili ya chama imeelemewa na makabrasha ya tuhuma kutoka karibu kila mkoa wa Tanzania.

Katika hilo la rushwa, kuna wakubwa chamani wanataka itumike FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE katika kupata suluhu la jambo hilo. Yaani, rushwa isionekane kwenye macho ya wanaKamati Kuu na hivyo wagombea waangaliwe kwa vigezo vinginevyo kama kukubalika na si rushwa. Inapendeezwa kuonwa kuwa wagombea walizidiana dau wenyewe kwenye majimbo yao. Kuna mvutano mkubwa kwenye Kamati ya Maadili na hata baina ya viongozi waandamizi wa chama.

Sababu ya pili ni sauti za makada na wananchi kuhusu nani arudishwe wapi kugombea. Kuna waliokataliwa majimboni lakini wanatakiwa uongozini; kuna waliopita majimboni lakini hawatakiwi chamani na uongozini; kuna waliokataliwa lakini wanatakiwa huko huko majimboni. Kamati Kuu imetumia muda wa kutosha kutega masikio yake huko site ili kujiridhisha kabla ya kufanya uamuzi wake. Je, waliokatwa wataandikwa tena?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwa sasa jijini Dodoma)
Ujenzi wa mnara wa Babel.
 
Tatizo lenu ni kutaka mabishano ambayo hayasaidii kitu chochote, tunaongea hapa kura za maoni mwaka huu wewe umerukia kitu kingine kabisa..point ni kwamba si wote walioshiriki kura za maoni CCM walihonga wajumbe!

Wewe huijui ccm!! ccm ina wemyewe sasa nyie wakuja mnajifanya mnakijua hicho chama zaidi kuliko wao ndio wanawaonesha sasa!! Tutaona mwisho wake.
 
Kosa la rushwa ni kwa anayetoa tu? Vipi kwa anayepokea?? 😀
Ukimkata mgombea kwa tuhuma za rushwa ukawaacha wajumbe waliopokea utakua umepunguza matawi tu na mti utakua tena baada ya mvua kunyesha. Kama ni kukomesha rushwa kata mti wote mzima(matawi+mizizi) kitu ambacho hakiwezi kutokea tena mpaka uchaguzi ujao kwasababu rushwa inakamatwa on the spot (mtoaji na mpokeaji papo kwa hapo)
Kwaiyo kigezo cha rushwa hakina mantiki yoyote🚮
Sauti inatosha? Au niongeze
 
Kwa mf. Jimbo la kawe hivi mnaamini kwamba kweli watanzania kwa sasa tunawaamini sana vijana au kigezo gani kimetuka pale?😂😂
 
Hata walioshindwa walitoa rushwa ila washindi walitoa zaidi. Labda Mashinji aliyepata kura 2!
Wakati wa kupiga kura mjumbe anabalance pesa uliyompa na mapenzi yake kwako so hata aliyeshindwa anaweza kuwa ndiye alyetoa mzigo mrefu zaidi
Mchawi mjumbe😂, tatizo liko hapa sijui kwanini tunajifanya hatuoni
 
Wawakate tu waliotoa rushwa wote na wafanye uamuzi based na advantage ya mtu utendaji wake. Ila CCM kwa rushwa kiboko hadi viti maalumu rushwa, hichi chama kwa kweli kijifikirie mtu anayetoa rushwa hafai maana ni adui wa haki.
Naapa watafunika kikombe mwanaharamu apite, maana tofauti na vyama vingine CCM karibu wote walioongoza kwa kura na wale waliowafuatia
wote wametoa rushwa! Chama kinanuka!
 
TAKUKURU wamerudisha mpira CCM!
Hapo nimeshindwa kuelewa, kwamba ni CCM ndo wameomba hiyo pass (warudishiwe) au ni TAKUKURU wenyewe wameamua kuitoa. Jambo lingine sijui sheria na taratibu zao za ufanyaji kazi zinavyowaongoza na hiyo namna walivyorudisha mpira kwa wahusika.
 
Back
Top Bottom