CCM Yamteua Bahati Keneth Ndingo kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Mbarali, Mbeya

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekutana katika kikao chake maalum, kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, leo Alhamis, Agosti 17, 2023.

Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Ndugu Bahati Keneth Ndingo kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CM katika Jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliopangwa kufanyika tarehe 19 Septemba 2023, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Ndugu Francis Leonard Mega, aliyefariki dunia tarehe 1 Julai, 2023.

Aidha, Kamati Kuu ya CCM, imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan na Seriali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Dkt. Hussen Ali Mwinyi, kwa namna zinavyoendelea kuwatumikia wananchi kwa vitendo kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.

F3vRoM7bwAABjnf.jpeg


Bahati.jpeg
 
Ameshapita Tayari maana kwa CCM hii imara , madhubuti na shupavu haiwezi kushindana na vyama dhaifu kama chadema katika sanduku la kura.Hapo kinachosubiriwa ni kuapishwa tu
 
Ameshapita Tayari maana kwa CCM hii imara , madhubuti na shupavu haiwezi kushindana na vyama dhaifu kama chadema katika sanduku la kura.Hapo kinachosubiriwa ni kuapishwa tu
Nafasi hiyo ungeenda wewe

Au umeridhika kuwa mpiga debe tu

Ova
 
Ndugu Bahath Ndingo ameteuliwa kugombea ubunge wilayani mbarali kupitia tiketi ya ccm,Twaombeni wasifu wake wakuu
Screenshot_20230817-201008.jpg
 
Ninachopendea CCM ni kuwa haijawahi kuwa na mechi ya kirafiki linapokuja suala la uchaguzi. Huo uchaguzi mdogo utaona viongozi wote wakubwa wa chama wametia timu. Hakunaga shughuli ndogo. Ninaishauri CHADEMA isisimamishe mgombea ili kuokoa gharama kwasababu kushindwa ni lazima. Kidumu CCM
 
As long as ni CCM it doesn't matter wasifu wake ni lazima tu atatangazwa hata wasipopiga kura. Ni mzigo mwingine tu unaoenda kupiga kura ya ndiyo kwenye Kila azimio la bunge
 
Mbunge wa Viti Maalum mh Bahati ameteuliwa na CCM kugombea Ubunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya

Uchaguzi hii unafanyika baada ya Mbunge wa jimbo hilo kufariki katika Ajali ya iliyohusisha Pikipiki na Trekta

Jumaa kareem 😀

cc: Mshana jr Ufipa st
 
Back
Top Bottom