Ziara za Deng Xiaoping baada ya kupokea kijiti cha Mao. Hivi viongozi wetu huwa wanaenda kuzurura tu huko nje ?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,017
12,310
Hebu mtazame hapa huyu mwamba Deng Xiaoping katika ziara zake baada ya kuipokea China iliyokuwa imechoka vibaya katika miaka ya mwisho ya Mao.

Deng alifanya ziara muhimu kwa wakati ule kwa majirani zake waliokuwa wamewaacha China mbali sana kama Thailand, Singapore, Japan, Malaysia

tazama maeneo aliyo tembelea na sikiliza kwa makini anavyo jibu swali aliyo ulizwa.

Hivi hawa viongozi wetu huwa wanaenda kutalii tu huko nje na kuishia mahotelini na kusaini mikataba ya kilaghai ya kutuuza ?

Sisi tumelaaniwa au ? Mbona hawa viongozi wetu hawana hata uchungu nasi na vizazi vyetu vijavyo ?

Wakina Mangungo waliuza baba na bibi zetu wa kale kwa vipande vya fedha nao hawa wanatuuza nasi na vizazi vyetu vyote tena.

Sisi watu weusi tumelaaniwa au ? Mbona kama hatuna akili timamu hivi mpaka leo ?

Hii video inatia hasira sana ukitazama hawa wanao onekana wenzetu namna wanavyowaza juu ya jamii zao tofauti na sisi.

Ukimsikiliza kwa makini majibu ya Deng Xiaoping namna alivyokuwa anaiwazia mema China baada tu ya kupanda Train ya kijapan ilimpa wivu na uchungu na kuona wachina wapo nyuma sana tofauti na wenzao wa Asia kwa wakati ule leo hii China inaongoza kwa km za reli duniani nzima ukijumlisha nchi zote na nchi ya pili kwa uchumi duniani ikifukuzia nafasi ya kwanza.
 
Hivi sisi na hawa wenzetu tuna fikiria sawa kweli juu ya hii dunia au kwetu bora liende
 
Back
Top Bottom