Kamati ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama yatembelea Kiwanda cha Maji Mgulani kuona mitambo mipya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mwenyekiti Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Victor Kawawa amesema wameridhishwa na jinsi SUMA JKT walivyotekeleza maelekezo yao kwa kukifanya kiwanda cha maji ya Uhuru kuongeza kasi ya uzalishaji.

Ameyasema hayo kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa ziara kwenye kiwanda hicho cha Suma JKT Bottling Co. LTD kilichopo Mgulani JKT Jijini Dar es Salaam.

Baada ya ukaguzi wa kiwanda amesema awali walitoa maagizo kiwanda hicho kuongeza kasi ya uzalishaji ili kwenda na adhima ya Serikali kutaka mashirika na taasisi zake kutoa kipaumbele kutumia maji ya kiwanda hicho katika shughuli mbalimbali.
photo_2023-11-14_22-33-58.jpg

photo_2023-11-14_22-33-52.jpg

photo_2023-11-14_22-32-53.jpg

Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Victor Kawawa

Mwenyekiti huyo amesema SUMA JKT imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6 kukifanya kiwanda kuongeza uzalishaji zaidi, ambapo kiwango cha uzalishaji kimeelezwa kuongezeka karibia mara tatu.
photo_2023-11-14_22-33-45.jpg

"Walikuwa wanazalisha maji Kita 3,250 kwa saa lakini sasa hivi baada ya kufunga mitambo mipya yenye uwezo mkubwa wanazalisha Lita 10,000 kwa saa na pia wamebadilisha mwonekano wa chupa mbalimbali na aina za chupa katika soko zinazotakiwa, wameongeza ufanisi mkubwa.”

Ameongeza kuwa "Tunashauri yale masoko yaliyokuwa yanasuasua sasa warudi tena maji yapo na yazalishwa kwa wingi.

"Sisi rai yetu Kamati ya Ulinzi na Usalama kwamba Mashirika, Wizara, Taasisi za Serikali zinunue Maji ya Uhuru ili kuendeleza adhima ya Shirikishi hili kuendelea kwenye soko."

Amesema kwa sasa kiwanda hicho kina kazi kubwa ya kutengeneza soko la uhakika ili kiweze kupata faida kwa kuwa kinafanya biashara, hivyo amewasii kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha wanafanikiwa katika hilo.

Pia Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele ameshukuru Kamati hiyo ambayo amedai wamekuwa ikiwashauri katika miradi yao mingi hususani iliyoko chini ya SUMA JKT.

"Mawazo ya kupanua kiwanda hiki japo tulikuwa nayo lakini yalishinikizwa zaidi na Kamati hii kuhakikisha kwamba tunapanua hiki kiwanda," amesema Meja Jenerali Rajabu

Amesema lengo la kuongeza ufanisi pamoja na uzalishaji kwenye kiwanda hicho ni kutanua wigo wa kibiashara pamoja na kukuza soko hasa kwenye maeneo ambayo bidhaa hiyo imekuwa haipatikani.
photo_2023-11-14_22-33-20.jpg

photo_2023-11-14_22-32-48.jpg

"Niwathibitishie Watanzania tuna dhamira ya kufanya biashara hii ya maji, kwanza maji yaliyo salama lakini imekuwa ikizungumzwa kuwa maji haya kuna mikoa yamekuwa hayafiki niwaambie mpango wetu ni kufikia mikoa yote ya Tanzania," amesema Meja Jenerali Rajabu.

Amesema kwa sasa hivi mikoa yote ambayo reli ya kati inapita tayari wameweka mkataba na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambao watakuwa na jukumu la kusafirisha maji hayo, ambapo amesema kuwa bei ya kushusha maji hayo kwenye mikoa ya karibu haitakuwa na utofauti wa kushusha kwenye mikoa ya mbali akitolea mfano Morogoro na Kigoma.

"Tupo kwenye mpango wa kununua magari zaidi ambayo yataenda zaidi Mikoani, sasa niwahakikishie Watanzania kwamba maji haya yatapatikana kwa wingi Nchi nzima," amesema Meja Jenerali Rajabu.

Viongozi wengine walioshiriki katika ziara hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni pamoja na maofisa wa Serikali na Jeshi Kujenga Taifa (JKT) ambapo wamepata fursa ya kuona namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi kupitia mitambo mbalimbali na watendaji walioko ndani ya kiwanda hicho.
 
Hata kuonyesha maji yenu mmeshindwa?

Hata design ya chupa hola?

Basi, kutaja tu jina la maji mnayozalisha ni changamoto?

Pathetic!..
 
Hizi kamati hizi ndyo zinazotengeneza mianya ya rushwa kwenye baadhi ya sekta za kiserikali.

Siajua mantiki hasa ya hizi kamati ni nini
 
Nilikuwa ofisi za SumaJKT Guard mlalakuwa,Kawe ,nilipewa haya maji.Kwa kweli yana quality nzuri sana!
 
Hizi kamati hizi ndyo zinazotengeneza mianya ya rushwa kwenye baadhi ya sekta za kiserikali.

Siajua mantiki hasa ya hizi kamati ni nini
posho, unafikiri hayo maekalu wanayojenga na kushindana kusomesha watoto shule za bei hela zinatoka wapi
 
Back
Top Bottom