DOKEZO Serikali mkoani Kagera fuatilieni madai ya Samaki wa kubanikwa kudaiwa kupuliziwa Dawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Waswahili usema ukistaajabu ya Musa utayaona ya Felauni. Ukielezwa unaweza usiamini lakini ndio hiko hivyo.

Wananchi wengi wa Kanda ya Ziwa waliozungukwa na Ziwa Victoria wengi wao utegemea samaki kwa ajili ya mboga, yaani Samaki ni mboga ambayo wanaweza kupata kwa haraka ukiachana na dagaa hasa kwenye maeneo yaliyopakana na shughuli za uvuvi.

Samaki hao ambao kwa zaidi upatikana kwenye Ziwa hilo ni aina ya Sato na Sangara, wakazi wengi wa Kanda ya Ziwa pamoja na wazaliwa wa maeneo hayo ambao wanaishi kwenye maeneo mbalimbali mijini upendelea samaki hao.

Licha ya samaki hao pendwa kupendelewa sana lakini kwa upande wa Mkoa wa Kagera baadhi ya watu walibuni mbinu kuwabanika ili kuwafanya wakae kwa muda mrefu bila kuharibika pia kuwafanya kuwa na radha tofauti tofauti.

HALI IPOJE KWA SASA
Baadhi ya wafanyabiashara katika Mkoa huo ambao ni wauzaji wa samaki baada ya kubaini samaki hao wa kubanika ni fursa kutokana na kupendwa na watu wengi wamekuwa wakitumia mbinu tofauti ambazo zinaweza kuwa zinahatarisha usalama wa afya za walaji.

Mbali na matumizi ya plastiki wakati wa kuwabanika hali ya kushangaza ni kuwa samaki hao wamekuwa wakipuliziwa dawa ili wakae kwa muda mrefu bila kuaribika na kuzuia nzi.

Samaki hao zaidi wanatengezwa kwenye visiwa vilivyopo Ziwa Victoria hasa Wilaya ya Bukoba vijijini maeneo ya Bugabo na ndani ya visiwa vilivyopo maeneo ya Muleba.
photo_2024-02-29_11-38-06 (2).jpg

photo_2024-02-29_11-38-09.jpg
Baadhi ya vyanzo vya siri vimedokeza kuwa Samaki hao wakishabanikwa wanapuliziwa Dawa maalum, ambapo inadaiwa lengo ni samaki wasiharibike haraka pamoja na kufanya inzi wasisogelea.

Wengi wanaotumia mbinu hiyo wanafanya katika mazingira ya siri ili kuepuka soko lao kutoharibika, wauzaji wengi wa samaki Bukoba na kwenye masoko hawafahamu vizuri samaki hao wanavyotengenezwa kwa kuwa nao utegemea kununua mzigo kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakijitahidi kuficha mbinu hiyo isibainike ili kulinda soko.

Chanzo cha siri ambacho kimeshudia wazi mbinu hiyo kinaeleza "Mbinu hii ni ya kificho sana kwanza ndio maana wanafanyia visiwani, hata vijana wanaozungusha samaki mjini (Bukoba Mjini/Mleba) hata wanaouza sokoni hawajui zinatengezwaje nao wanaletewa tu hawaelewi."

Samaki hao waliobanika usifika kwa kukaa muda mrefu na watu wengi wamekuwa wakipendelea kuwatumia hususani kuwasafirisha kwa kuwa sio rahisi kuharibika.

Ni muhimu mamlaka zikamulika kwa kina suala hili ili kubaini mbinu hii ikiwezekana kutafiti athari zake kwa watumiaji na pia kuwachukulia hatua wahusika sambamba na kutoa elimu zaidi.

Licha ya kutokuwepo kwa tafiti zinazobainisha wazi, lakini imekuwa ikinadaiwa mikoa ya Kanda ya Ziwa inakabiliwa na wagonjwa wengi wa saratani (kansa) ikilinganishwa na kanda zingine.

Ikumbukwe Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Phillip Mpango miezi kadhaa iliyopita akiwa Mwanza kwenye Hospitali ya Bugando alidai uwepo wa madai baadhi ya wafanyabiashara kutumia dawa ya kuhifadhia maiti katika kuhifadhia samaki.

Hata hivyo madai hayo yalifafanuliwa zaidi na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Hamis Ulega akijibu swali la Mbunge aliyetaka ufafanuzi wa Serikali kuhusu jambo hilo, Waziri Ulega alisema “Jambo hili halina uhakika ni kwamba watu wanahisi tu.”
 
Back
Top Bottom