Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
ALIYEKUWA Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Jahazi Asilia, Mussa Abdallah Kitole, amekataliwa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa madai kuwa hana kitambulisho cha Mzanzibari mkazi.
Tukio hilo lilitokea juzi katika Kituo cha Shule ya Gamba, katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambako Kitole alikwenda kujiandikisha kama mpigakura.
Hata hivyo maafisa waandikishaji walimwambia kuwa hawezi kuandikishwa kwa sababu hana sifa.
Msimamizi wa Uandikishaji katika Wilaya ya Kaskazini Unguja A, Murshid Khamis, alisema Kitole hana kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi na kwa hiyo hawezi kuandikishwa.
"Sheria ni msumeno, hakuna aliyekuwa juu ya sheria," alisisitiza Khamis.
Kwa sasa Kitole ni Katibu Mkuu wa Jahazi, chama hicho ambacho kimejijengea ngome kubwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Kassim Bakari Ali, alielezea kusikitishwa kwake na kwamba hizo ni njama za kukwamisha wapinzani wa kisiasa.
Alisema "Kitole ni mzaliwa halisi wa Zanzibar, kitendo cha kumkatalia kujiandikisha ni cha kumdhalilisha kiongozi huyo."
Hata hivyo alisema chama chake kimeamua kufanya mkutano mkubwa mwishoni mwa wiki hii kuelezea udhalilishwaji huo katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.
SOURCE: MWANANCHI.