ZEC Yakataa Kumuandikisha Aliyekuwa Mgombea Urais Zanzibar

Sheria za uchaguzi wa Zanzibar zinasenma ili uandikishwe kuwa mpiga kura ni lazima uwe Mzanzibari Mkaazi katika jimbo unalojiandikisha. Ukijadili tafadhali zingatia hilo. Huu ni utawala wa sheria Bwana!!!. Usiwakandie ZEC tu. Hata hao uliowasema0- kama hawana Zan Id hawatoandikishwa katika uchaguzi wa 2010.

Wakati anagombea katika ngazi hiyo ya urais alikuwa mkazi wa wapi? Mambo mengine si lazima uende darasani.
 
Kwa zanzibar hilo si la kustaajabu. Alikataliwa mgombea urais wa zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kule mtoni kisa yeye akitangaziwa kifo wanasema akiwa popote pale. Hivyo sheha wa shehia ya mtoni alimkataa sio mkazi wa mtoni.

Kuna mengi zanzibar. lakini tunamuomba Mungu ayaepushe.
Hawa nao wapuuzi, yaani mtangazaji wa redio ndiye anayejuwa anakoishi mtu......... Hii nayo kali. Yule m'bongo fleva alikosea kusema uswahilini kuna vituko, angesema Zanzibar kuna vituko.....

Kwa mchezo huu hawezi kuwa mkazi wa Zanzibar maana hakuna mahali panapoitwa POPOTE PALE...
 
Hii inanikumbusha mkasa mmoja wa sheha wa shehia moja maarufu kwa kupandikiza wapiga kura kutoka bara kule visiwani, alimkataa mkaazi wake asiandikishwe eti hamtambuwi...ukweli ni kuwa mkaazi huyo alikuwa ni mwanachama wa chama cha upinzani na baraza ya nyumbani kwake ndio kama "masikani" ya mazungumzo na wanachama na wapenzi wa chama chake, siku ya uandikishaji kuelekea uchaguzi wa 2000, jamaa alikataliwa na sheha wake, hakufanya tabu alirudi nyumbani kwake kimya, uchaguzi ukafanyika na yaliyotokea yakatokea. Cha ajabu sasa, zikaja dawa za matende na mabusha, zikawa zinagaiwa kila nyumba katika kila shehia na masheha wakatakiwa wawahamasishe wakaazi wa shehia zao kuchukuwa dawa hizo, sheha yule yule, kiguu na njia katika vijumba vya wakaazi wake, akiwataka kushirikiana na watoa dawa...alipofika katika nyumba ya yule jamaa aliyemnyima kuandikishwa siku ya uchaguzi... kwa mbwembwe za ukubwa wa kuongoza mtaa tu..alianza upuuzi wake...si anajuwa kuwa jamaa ni mpinzani "...hodi.." aliita bw.sheha kwa kelele. Bahati jamaa alikuwapo, mlango ulipofunguliwa tu,sheha hakusubiri, alitoa ilani kwanza. "...nimekuja makusudi kwa habari za dawa za matende maana nasikia mnakataza watu wasichukuwe eti zinaharibu uzazi..uwongo mtupu..." alin'gaka sheha. Kwani aliwahi kumaliza, mke wa yule jamaa kama alipangwa vile alivurumisha dishi la maji ya mavumba,yananuka vibaya sijuwi yalivumbikwa siku ngapi, na jamaa baada ya kumtaka radhi sheha, aliporomosha matusi na kumfukuza "..nenda kashitaki popote ww si mkubwa, alaaa...kwenye kura hunitambuwi...kwenye madawa haya hata sijuwi yanatoka wapi...huko unanitambua...mm sina haja ya dawa bana...pelekeni hospitali huko...hata panadolo hakuna..eboo..." alimalizia kwa msonyo na kufunga mlango wake. Mbona uchaguzi uliofuata aliandikishwa.
 
Anakataa dawa ambazo zingesaidia kwa sababu alikataa kuandikishwa! Na wewe unamuona mwerevu! Huko Zanzibar basi kuna kazi.

Amandla.......
 
Hapana, nimekumbuka tu huu mkasa lakini nilichotaka kuashiria ni jinsi hawa masheha wanavyoonyesha kuwa utendaji wa majukumu yao ni wa kisiasa siasa kwa kulinda maslahi ya waliowateua, kama huyu sheha mfano,system ingemuwezesha kufanya kazi kwa uwadilifu, matatizo kama haya ya kukosana na wakaazi wake katika mambo ya faida kama haya yasingelitokea na kila mtu angetekeleza wajibu wake kama inavyopasa. Hili pia dogo tu, yapo makubwa zaidi ya haya tena ya hatari tu, kuna sheha mwingine yeye alikataa kutoa barua ya utambulisho kwa mkaazi wake ili apatiwe kibali cha ujenzi na manispaa, sheha kwa sababu kama hizi akamuhangaisha jamaa wee, yaliishia kupigana matofali na mapande ya mawe na kuumizana bure, sasa haya yote ya nini. Haya matatizo si kama nafurahia mm watu wangu hawa wananiuma siyo!
 
Back
Top Bottom