Zanzibar yatangaza wagonjwa wapya 23 wa COVID-19. Idadi ya maambukizi yafikia 58 na 170 kwa Tanzania ( 19.04.2020 )

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
WAGONJWA WA COVID-19 WAFIKIA 58 Z’BAR, VIFO VITATU

Idadi ya wagonjwa wa Covid-19 visiwani Zanzibar imeongezeka na kufikia 58 na idadi ya waliofariki kwa ugonjwa huo sasa ni watu watatu. Wizara ya Afya Visiwani humo imetangaza leo kuwa kati ya wagonjwa wapya 23, wagonjwa 21 ni Watanzania na wawili raia wa kigeni.

IMG_20200419_112345.jpg
 
Watanzania, msishangae ikitokea nchi yenu inakuwa kitovu cha corona duniani, wakati huo nchi zingine zikiwa zimefanikiwa kudhibiti maambukizi unless tunabadilika.

Swali: Huku bara hakuna wanaofia nyumbani kabla ya kuchukuliwa vipimo?

Majibu nadhani mnayo.

Tusubiri update za huku bara.
 
Tulikuwa wagumu sana kuchukua tahadhari mapema, madhara yake ndio tunayaona sasa, ila hatua madhubuti zikianza kuchukuliwa sasa.

Kuanzia ngazi ya mtu binafsi.(jiulize unachukua tahadhari gani kujikinga na huu ugonjwa) then itazame familia yako, ndugu, jamaa, na marafiki zako, tusisitiziane jinsi ya kujikinga, tusifanye utani, tutapunguza sana maambukizi siku za mbeleni.

Ukishajua uko vitani hakuna sababu ya kuziogopa taarifa mbaya, hizo zinatarajiwa, mwanajeshi akifia vitani sio mwisho wa vita, issue ni kuendeleza mapambano, never look back.

Better late than never.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi bado swali langu ni lile lile.. hivi inawezekanaje mtu akafia nyumbani kisa Corona? Kwamba wananchi hawana elimu kuhusu dalili za huu ugonjwa? Au watu wanaogopa kutoa taarifa sababu ya jinsi wanavyowatreat wagonjwa au suspects?

Maana cases zenji ziko 58 haiwezekani kwamba hospital zote zimejaa wagonjwa hadi wengine wafie nyumbani..

Hili jambo inabidi lijadiliwe ili tatizo lionekane.. either hakuna elimu kuhusu dalili au wananchi wanaogopa kutoa taarifa (kwanini?)
 
khaah! siipatii picha Tanzania bara ikitangaza matokeo ya corona kwa ujumla inaweza ikagonga 100 mana siku mbili hz bado hawajatangaza.

Mungu aturehemu
 
Hapa ndipo unapoona hatuna viongozi, na wapiga debe wao wanawatetea kwa kusema eti duniani kote viongozi wamefanya uzembe kwenye kudhibiti Corona.

Men hawa vichaa sijui wao wanakinga ya Corona! So sisi tumeiga uzembe kwa wenzetu badala ya kujirekebisha kwa uzembe wa wenzetu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom