#COVID19 Rais Mwinyi: Zanzibar kwa sasa haina wagonjwa wa COVID-19

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mwinyi.jpg

Picha: Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi
Serikali ya Zanzibar imeeleza kuwa hivi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ugonjwa wa Uviko19 (Covid-19) japokuwa hawawezi kuweka wazi kama ugonjwa huo umeisha moja kwa moja visiwani hapo.

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ameyazungumza hayo wakati wa mahojiano yake na waandishi wa habari, Ikulu Zanzibar, jana Februari 17, 2022.

Pamoja na mambo mengine alizungumzia kuanza kutumika kwa teknolojia mpya ya kupima Uviko19 kwa muda mfupi kwa kutumia simu ((EDE Covid Scanners) pamoja na kurejea kwa safari za ndege za ‘Fly Dubai’ kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Amesema hatua hiyo itapunguza matatizo ambayo wasafiri wanayapata na kusisitiza kwamba ni muhimu Serikali kufanya kila juhudia katika kurudisha watalii hapa Zanzibar ambapo ndege ya ‘Fly Dubai’ itakuwa inakuja mara mbili kwa siku na siyo muda mrefu ndege za Shirika la ndege la ETIHAD itaanza safari zake hapa Zanzibar.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya visiwani huo Nassor Mazrui amesema tangu Januari, mwaka huu Zanzibar haijaripoti kisa kipya cha Uviko-19 kwa wakazi wala wageni lakini haitoshi kusema kuwa ugonjwa huo umeisha.

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom