Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Hii ni sawa na kumwambia Mungu unataka kuacha uzinzi lakini wanawake wote waondoe duniani wasikupe tamaa ya zinaa. Mimi ninachojua ili upate thawabu lazima ushinde vishawishi wakati wa kufunga. Inakuaje unaogopa watu wasile kwa sababu yya njaa zako? Hapo hakuna funga.
Kuna migahawa na baadhi ya hoteli ambazo ziko maeneo ya wazi ina maana nazo itabidi zifungwe maana watu huwa wakula wakionekana mahala pa wazi

Kwa miktadha wa tangazo/agizo la naibu Waziri hii ni hatari kwa wajasiriamali wadogo wadogo

Hii ni sawa na kumwambia Mungu unataka kuacha uzinzi lakini wanawake wote waondoe duniani wasikupe tamaa ya zinaa. Mimi ninachojua ili upate thawabu lazima ushinde vishawishi wakati wa kufunga. Inakuaje unaogopa watu wasile kwa sababu yya njaa zako? Hapo hakuna funga.
Kuna migahawa na baadhi ya hoteli ambazo ziko maeneo ya wazi ina maana nazo itabidi zifungwe maana watu huwa wakula wakionekana mahala pa wazi

Kwa miktadha wa tangazo/agizo la naibu
 
Huu ni upuuZi kabisa !! Kwani hakuna wakrosto Zanzibar???
Hichi ni cha mtoto kwa ubaguzi unaotokea dhidi ya Wakristo na Wabara Zanzibar, hapa mjini vikitolewa vyandarua au madawa ya malaria misaada ya watu wa Marekani nyumba za Wabara na Wakristo hazipati hata taarifa.
 
Ni sawa kabisa,lakini lazima ufahamu,Zanzibar ina serikali yake,na juu ya kwamba,juu ya kwamba kuna serikali ya muungano,lakini kuna mambo mengi ya zanzibar ambayo serikali ya muungano haina haki ya kuyaingilia,mathalani suala la uchaguzi kule,unaedeshwa na wao wenyewe na unaamuliwa na wao wenyewe,Kwa hiyo litizame hata hilo,ambalo ni suala la haki zaidi,ambalo hata linakiuka haki za kibinaadamu na sheria,serikali ya muungano hailiingilii,najua umekuja zaidi katika Imani ya kidini,Ni dhahiri limekugusa katka Ustashi wako wa kiimani,lakini ukweli utabaki pale pale,kwamba zanzibar ina haki hata ya kujitoa katika muungano,ikiwa raia zake wataamuwa hivyo,usichukulie kama unavyiona hivi sasa,lakini Miaka 20 tu nyuma,zanzibar ilikuwa na asilimia 99.9 wakiwa waisilamu,Kwa hiyo hiyo inaonesha wazi uislamu Ni dini ya asili ya zanzibar,tukitaka tusitake,Kwa hiyo suala la kutaka tuwanyime haki ya kufuata sheria za utamaduni wao,hiyo itakuwa Ni kinyume na haki za kibinaadamu.
Wewe hujui haya mambo, kumbe hujui kuwa tume ya uchaguzi ya Zanzibar ni tawi dogo la tume ya uchaguzi ya Taifa? Hivi unadhani anaoendesha tume ya uchaguzi ni Lubuva na sio makamu mwenyekiti Mzanzibar Mahmoud Hamid?
 
Isis ni taasisi iliyoanzishwa na marekani kama ilivyokuwa kwa alqaeda na wengineo lengo kubwa kuuchafua uislam kwa maslahi yao tamko la wawakilishi wa waislamu duniani limezipinga taasisi hizo na kutamka wazi kuwa uislam hausapoti ugaidi wala mauaji yoyote bila ya haki na fahamu kua gaidi ni mtu wala sio dini vit endo viovu ni vya wanadamu ila mungu no mwema
kuran inasema
"rafiki wa mwislam n mwislam
"kulipa kisasi n suna" kwa hali hii nitaachaje kuamini kuwa isis ndo nyie walewale?
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
utamaduni ni wao kwa nini tuwaingilie
 
Dini yakwenu wenyewe sie wakiristo twahusika vipi?ndio maana ma al shabaab wengi fungeni nyie sie twala popote sio nchi ya kiisilamu
 
Hata kama ikitokea watu kumi tu zanzibar ndiyo wakawa si waislamu bado hawastahili kubanwa kiasi hicho kisa imani ya mtu mwingine.Imani hailazimishwi waislamu jitafakarini sana ktk taarifa hiyo.
Uhuru ni utajiri, kuna watu mnawalazimisha kufunga hawana mpango wa kufunga hivyo mnatenda dhambi kwa kuwakosesha uhuru.

Mkuu hujakatazwa kula
Umeambiwa usile hadharani
Kiswahili pia Shida kwako
 
Kwaresma ni mfungo usioruhusu mtu kuamka asubuhi na mapema saa kumi kubugia daku kisha tena unakula saa 12

Hiyo si kufunga bali ni kubadilisha tu muda wa kula

Umeona eeh...!

bado hujajibu swali

ni vitu gani ukifanya vinabatilisha mfungo wako wa kwaresma,

kwaresma unafunga masaa mangapi
 
Wewe hujui haya mambo, kumbe hujui kuwa tume ya uchaguzi ya Zanzibar ni tawi dogo la tume ya uchaguzi ya Taifa? Hivi unadhani anaoendesha tume ya uchaguzi ni Lubuva na sio makamu mwenyekiti Mzanzibar Mahmoud Hamid?
Kama huwezi kuishi huko,rudi kwenu shinyanga na mwanza,acha kutengeneza ubaya,utakurejea mwenyewe,waachieni wazanzibari wajiongozi,Nani alotoka zanzibari akaja kuongoza shinyanga na mwanza?.
 
Mungu hayupo. Acheni kujidanganya.
Kaka unaanzisha ugomvi na aliyekuumba,nikuambie jambo moja,nimeshakutana na watu kama wewe,na wengi wanaishia vibaya sana,najua kinachokunbua Ni hizi pumzi zako,lakini nakuasa kabla ya upepo haujabalika,nikwambie jambo Moja experience yangu katika ulimwengu Huu Ni kubwa,nabahatisha haraka sana,Kwa kusema wewe Ni kijana ,kutokana na kauli zako,tafuta watu wenye busara ukae nao,mimi binafsi nimezunguka ulimwengu mzima,baada ya hapo nimezidi kumuogopa M Mungu,kutokana na hatua uliyofikia namuomba Muumba akuudhihirishie,lakini nakwambia jambo moja,hayo unayoyasema unajitengenezea jambo baya,kama umewahi kusikia neno linaloitwa laana,basi ujue wewe unaitengeneza Kwa kauli zako,nadhani hili neon linaloitwa uhuru wa kuabudu limekuathiri.
 
Thibitisha kwamba Mungu yupo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom