Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Kipindi cha kutafutiwa sababu za makusudi wakristo wafungiwe biashara zao, nakumbuka mmoja aliegongewa na kupelekwa polisi kisa harufu ya chakula. Huku ukienda sehemu za Waarabu kama kwa Raju vyakula vinauzwa kama kawaida kutwa na walaji 99% ni waislamu ila humo ndani kila mtu ana jina la Kikristo.
  • Ni kweli hata ukiwa mafichoni unafanya vyako (unajipikia ili ule) wale jamaa wengine wakisikia harufu bado ni nongwa
 
Mbona mnapotosha.ni nani amekatazwa kula mchana? Watu bana mnaamua kujitoa ufahamu makusudi kabisa ili kuwachafua waislam.imesemwa usile hadharani siyo usile mchana. Eeeh
Kwa hiyo watu wale wakiwa wamejificha? Dafu langu, nimenunua kwa hela yangu, unataka nikalie wapi?
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Sawa kabisa. Hata ukija nyumbani kwangu ukaanza kula punda au panya nitakufukuza. Wewe mmoja sisi 99 kwa nini tukuvumilie? Ningekuwa mimi ni serkali wala nisingehangaika: nawaachia tu wamnanchi wenye hasira. Kuna wasichana walivaa minidkirt Kariakoo 2008 wananchi wenye hasira wakavua skirt zite (tujue moja!); hawakurudia.

Idd mubarak ndugu zetu! Ramadhan kareem!
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Zanzibar ni kisiwa hatari Sana, siipendi ccm ila Kwa kuibana Zanzibar na kuikalia Kwa mabavu ipo sawa kabisa.
Leo hii Zanzibar ikiachwa kuwa taifa huru pasipo muungano na Tanganyika,Zanzibar haitakalika itakuwa Kituo cha magaidi.
 
amin amin nawaambia mara nying:-
Mzur halingi....wala
Mjuaji c muongeaji...wala
Mchokoz hana nguvu .
Ndo hawa wenzetu sasa Z'bar kwa Tngnyika Slam kw Kristo yaan sio km tukiamua wanatuweza ila wanatafta kupigwa waumie tu
Ni kuwapuuza tu
 
Zanzibar ni kisiwa hatari Sana, siipendi ccm ila Kwa kuibana Zanzibar na kuikalia Kwa mabavu ipo sawa kabisa.
Leo hii Zanzibar ikiachwa kuwa taifa huru pasipo muungano na Tanganyika,Zanzibar haitakalika itakuwa Kituo cha magaidi.
100%
 
Waznz mbali ya kwamba wengi ni waislam lkn mwezi wa ramadhani kwao ni tukio kubwa la kiimani na linabeba dhana ya utamaduni wa mzanzibari...kula hadharani mchana kweupe hata km wewe si mwislamu ni ukiukwaji wa maadili na taratibu za watu ukiwa uko kwao....kwa hiyo nampongeza waziri kwa kulisema hilo mapema na kwa uwazi...kama huwezi kufunga ukiwa zanzibar kale chakula chumbani kwako peke yako watu wasikuone.
 
Hii ni kawaida kwa Zanzibar tatizo tu hili limekuwa swala la kukuletea kidini na linalazimishwa kwa misingi ya dini.
Ukiwa pale mjini unaweza kwenda kula pale kanisani Mkunazini.
 
Wewe umefunga.... Mwenzio anakula inakuuma nini...?? Hivi hawa ndugu zetu kama wana wakristo wanaishi nao watawaruhusu kula kweli? Au ndio ukiajiliwa au kuishi na muislam lazima ufate matakwa yake ya kidini...

Mkuu hawa Watu(baadhi) wana matatizo sana na nnahisi ni kwa sababu wameuweka U-dini mbele kuliko 'Utu'.Nimeshuhudia baadhi ya Wasichana wa kazi wanao fanya kazi za ndani au ktk sehemu za biashara zao moja ya masharti yao ili wakupe kazi ni kuufuata Uislam bila ya kujali wewe ni Mkristo au Mpagani.

Utaenda Msikitini kama wao na ikifika kipindi cha kufunga utalazimika kufunga kama wao ,kama hautaki katafute kazi kwingine.Ni wabaguzi sana na hii tabia binafsi huwa inanikera na inatengeneza bomu mbele ya safari.

Hivi kuamini (Imani) ni mpaka ulazimishwe au inatakiwa kutoka Moyoni kwa Aaminie ?..Hata hiyo funga sidhani kama inahesabiwa rehema yoyote kwa Mola..
 
Zanzibar iko miaka nenda rudi.Hukatazwi kula kama ni mkristu Bali tunaambiwa usile hadharani.

Kwanza wanaweka onyo kwenye kila ofisi za serikali,public areas.Jamani hiyo IPO Zanzibar, tena ukishuka na ndege au boti hujavaa kitambaa wana kuomba ujifunge kitambaa kichwani.

Ninachokiona ni mila tu wala siyo issue ya udini nakumbuka waislamu ni 95%

Hakuna tofauti kati ya Mila na hizo Dini ,tofauti ipo katika vile mnavyo ziabudu.Wengine Msituni wengine kwenye Majumba makubwa wengine kwenye Milima nk.Unapoiweka Dini mbele kuliko 'Utu' unapoteza uhalali wa ule 'Ubinadamu'.
 
Kweni nchi hii inaamini dini mpaka wageuze watu wote qa Zanzibar wawe na imani moja?
 
Hichi kitu sio kigeni kwa Zanzibar kipo zamani. Ngoja uone watu humu watakavyorusha mapovu kwa sababu zao binafsi. Marufuku kula hadharani tu kwahio jaza tumbo kabla hujatoka home hakuna shida.
 
Kweni nchi hii inaamini dini mpaka wageuze watu wote qa Zanzibar wawe na imani moja?
Usipoteze muda kuwaza sehemu yenye watu milioni 1.35
Kama unaona ukiwa Zanzibar unakwazika, unakuja apa Dar es salaam Tanzania. Unakula nguruwe na bia, mwanzo mwisho akuna cha maswala ya dini, wala baba ake dini. Unakula Bata mpaka unakimbia wewe, apa tunaishi kwa katiba mwanzo mwisho.
Unajipatia protein nzuri ya nguruwe na bia yako
 
Hata kama ikitokea watu kumi tu zanzibar ndiyo wakawa si waislamu bado hawastahili kubanwa kiasi hicho kisa imani ya mtu mwingine.Imani hailazimishwi waislamu jitafakarini sana ktk taarifa hiyo.
Uhuru ni utajiri, kuna watu mnawalazimisha kufunga hawana mpango wa kufunga hivyo mnatenda dhambi kwa kuwakosesha uhuru.
Kwani wamelazimishwa kufunga au wameombwa au kutakiwa kutokula hadharani? Kumbuka kutokula hadharani wakati wa mchana haimzuii mtu kula nyumbani kwake au mahotel yatakayokuwa wazi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom