Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Mm nipo huku 2 months sasa nataka nishuhudie hiyo kitu
Mm sipelekeshwi na hao vilaza.
Sijui nyerere aliwaza nn kufanya muungano na haa watu..
Nenda kwenu ambako hutapelekeshwa. Uharibifu wa funga mwisho bandarini.
 
Dini haiendeshwi kwa akili za MTU, kwamba Mimi nafikiri Bali ni sharia IPO katika vitabu vitukufu sisi ni kufuata tu. Hakuna andiko linalosema hivyo unavyofikiri Bali lipo linalosema anapata dhambi anaekula mchana Wa Ramadhani au kulisha bila dharura. Yule anaekula hadharani pia anapata dhambi kwa kumfanyia karaha mfungaji.
Asante sheikh
 
Kama ni ivyo hapo hakuna kufunga ni kulazimishana.Na hao wanaofunga wanashinda njaa tu bure au wanabadilisha ratiba ya kula mana kama kweli wewe umeamua kwa dhati kufunga kwa ajili ya Mungu wako sidhani kama utasumbuliwa na mambo mengine anayofanya jirani yako.
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu


Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.

Hivi zaa inzi bar ni taifa la kiislam? 5
Sisi wa upande wa pili shughuli zetu huwa haziwaathiri ambao si wa kwetu ila upande ule wanataka hadi wewe usio wa upande wao ufuate wanachotaka wao by power by force
 
Kwani huku kufunga ni imani ya mtu au ndio kulazimishana kutokula mchana? Hizi imani zingine za shuruti hizi...zipewe polisi wasimamie basi
Mbona mnapotosha.ni nani amekatazwa kula mchana? Watu bana mnaamua kujitoa ufahamu makusudi kabisa ili kuwachafua waislam.imesemwa usile hadharani siyo usile mchana. Eeeh
 
Yaaap.madhehebu yooooote.duniani.inafahamika labda uwe na dharura.sasa zanzibar wanashindwa kukataza kula hadharani kwenye kwaresma.kwa sababu si madhehebu yote ya wakristo wanaofunga.watawatesa madhehebu mengine.
Na siyo waislamu wote wanafunga
 
Hapo naipongeza wizara ya katiba,,,,maana Zanzibar ni nchi ya kiislamu,,,hivyo wasio waislamu wakitaka kuishi Zanzibar lazima wayaheshimu matukufu ya kiislamu
 
Hivi wewe ukiwa umefunga nami nakula chakula changu hadharani inakuuma nini....!!?? Hivi ina maana wakristo huwa hatufungi?? Mbona tunaishi na nyie vizuri...
Hata kama mfanyakazi wako wa ndani kama siyo muislam mpe uhuru ale kwa muda wake... Wewe uliyefunga uko na Mungu wako... Kumnyima uhuru mwenzio kisa umefunga hain maana... Na mfungo wako ni batiri...
Kabisa mkuu huwez kulazimisha mtu asile hadharani wakt si wa imani hiyo.
 
Mungu atakaye kusimamia wewe kuwachukulia hatua watu wa imani nyingine kwa kula hadharani huyo atakua ni Mungu wa zanzibar, Ukifunga ukashawishika kula kwa sababu mtu wa imani nyingine anakula basi utakua umefunga kwa sababu fulani sio za kidini, Tufuate sheria za nchi sio sharia za waarabu.
 
Kwanini tunakataza Watu kufirana wakati Nchi yetu haina dini na Upagani wa Nchi yetu haukatazi Watu kufirana na wakifanya hivyo wenyewe Hakuna athari kwa asiefanya?

Numekueleza kwa Mifano ili uelewe, Mavazi Mafupi (Mini skirts) kwny Ofisi za Serikali kwanini inakatazwa wakati ni Uhuru wa Mtu binafsi?

Umewahi kujiuliza kwanini huku Tanzania Bara tuna mapumziko ya sikukuu za Kiislam na Kikristo pekee kwanini huwa hatusherehekei Sikukuu za wengine Kama sikukuu za Kitaifa mfano Wahindu, Wabudha, Singasinga kwani Hawa hawapo?


Kajifunze maana ya neno utamaduni Wewe unachanganya Kati ya utamaduni na Uhuru!
  • Usitumie habari za ushoga kuhalalisha huo udini na hujuma zinazo fanyika hapo Zanzibar kwa wakristo
  • Kwa nini Wazanzibari wakristo (au wakristo kwa ujumla) wanapangiwa cha kufanya?
  • Si haki kuiamulia jamii ya wakristo (Agustino Ramadhani, Michael Hafidhi, Moudline Castico, Sylvester Mabumba, Augustine Ndeliakyama Shao, na nk.) cha kufanya
  • Wazanzibar wanaojigamba kwamba wanapenda haki kwenye chochote kile ikiwemo kwenye swala la Muungano mbona hiyo haki hawatendi kwa wakristo waliopo Zanzibar?
 
Sasa mtu kama unafunga bado unatamani chakula anachokula mwenzio, kuna haja gan ya kufunga? Si ule tu na wewe? Tatizo mnalazimishwa kufunga na mwezi tu. Na si kutika moyoni
 
  • Usitumie habari za ushoga kuhalalisha huo udini na hujuma zinazo fanyika hapo Zanzibar kwa wakristo
  • Kwa nini Wazanzibari wakristo (au wakristo kwa ujumla) wanapangiwa cha kufanya?
  • Si haki kuiamulia jamii ya wakristo (Agustino Ramadhani, Michael Hafidhi, Moudline Castico, Sylvester Mabumba, Augustine Ndeliakyama Shao, na nk.) cha kufanya
  • Wazanzibar wanaojigamba kwamba wanapenda haki kwenye chochote kile ikiwemo kwenye swala la Muungano mbona hiyo haki hawatendi kwa wakristo waliopo Zanzibar?

Tatizo ni kuwa Malalamiko hayo ya 'Wakristo wa Znz' yana tokea Tanganyika sio Znz
 
Kwa hiyo wakristo nao wajifiche ndani?
Kama hoteli wateja wake ni vijana wa kiislam kosa ni la nani? Ukiifunga hoteli ili isiuze chakula ndo kijana wa kiislam atafunga? Waulizeni vijana wenu kwa nini hawafungi? Hoteli ni mahali pa umma, na utalii ndo unapanda chati kipindi hiki. Imani zenu zisiwe kikwazo kwa maisha ya watu. Unless nchi ni ya kidini
 
Tatizo ni kuwa Malalamiko hayo ya 'Wakristo wa Znz' yana tokea Tanganyika sio Znz
  • Udini au Ubaguzi ni wakupingwa kutokea popote pale
  • Hata Trump alipoleta ubaguzi dhidi ya waislamu alipingwa na watu wa ndani na nje (wakiwemo na waislamu wa Zanzibar, Bara, Saudia, Iran, Indonesia na nk.)
 
kama ni uliokuwepo hata kabla ya mapindunzi kwa nini taifa liige mfumo kanda minzi kwa watu wa imani tofauti hawaoni huo kuwa ni unyanyasaji wa wale wasiofuata mfumo wa dini flani/
 
wanashangaa ya zanzibar wakati sasa hivi ofisi zote za serikali kama umevaa kimini, suruali ya kubana, jeans ya kuchanwa chanwa, mlegezo, kapelo, nguo inayoacha makwapa wazi, na mfanano wa hivyo.

Huruhusiwi kuingia ndani huoni kama hao nao wanaingilia uhuru wa mavazi?? mbona hamlalamiki.
Hizo ni taratibu za serikali na taratibu hizo ni lazima zifuatwe ama kutekelezwa na kila anayehusika (kwa case hii ni kwa watumishi tu na siyo kila raia). Kwa hivyo taratibu za dini fulani hazitakiwi kumhusu kila mtu kwa sababu si za lazima kufuatwa ama kuheshimiwa na kila mtu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom