Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Mbona Waislam ni asilimia ndogo Marekani lakini wanadai wanataka haki zao

Uislam ni udicteta halisi
Mkuu unaizungumzia Marekani baba wa demokrasia ulimwenguni au America kusini hah hah all in all wengi wape na ndivyo ilivyozoeleka toka enzi na enzi!
 
Kwani mkuu serikali ina dini?? Au toka lini serikali inadhibiti mambo ya dini??? Nchi zetu ni huru hizi haya mambo toka lini kulazimishana?? Kila mtu awe na uhuru wake maana hii ni ibada na kila mtu ataulizwa siku ya kiama hivyo tusiingilie uhuru wa dini za wengine
Ni kweli nchi yetu haina dini lakini ndio utamaduni wa watu wa Zanzibar na wengi wape,kwa Zanzibar utamaduni wao dini ya kiislamu imepewa kipau mbele,na ndio maana serikali imesisitiza ila kutoleta uvunjivu wa amani ,hebu fikiria watu waanze kula hadharani halafu wakicharazwa bakora na zikatokea vurugu ,si ndio serikali itakuwa ya kwanza kulaumiwa kwa kushindwa kutoa tahadhali au kudhibiti hali hiyo ndio maana kuna usemi wa ya ngoswe tumwachie ngoswe,au ukienda Roma uishi kama Waroma,wakati mwingine uhauru na haki huleta vurugu
 
Kufunga kula ni imani ya dini wala hakuna madhara yoyote usipofunga kula.Si jambo zuri kulazimishana kuamini imani isiyoaminika kwa wengine.
 
Hivi wewe ukiwa umefunga nami nakula chakula changu hadharani inakuuma nini....!!?? Hivi ina maana wakristo huwa hatufungi?? Mbona tunaishi na nyie vizuri...
Hata kama mfanyakazi wako wa ndani kama siyo muislam mpe uhuru ale kwa muda wake... Wewe uliyefunga uko na Mungu wako... Kumnyima uhuru mwenzio kisa umefunga hain maana... Na mfungo wako ni batiri...
Kaka mimi sio mwislamu ni mkiristo haswa ,nilichokisema ni kuwa Zanzibar ,Uislamu ni utamaduni wao,na ndio taratibu za dini ya kiislamu ,kwa hiyo kula hadharani,narudia tena kula hadharani unakuwa unawakwaza waliofunga na kwa Zanzibar dini ya Kiislamu imepewa kipau mbele na hata serikali ,hiyo ndio hali halisi upende au usipende ,serikali imeamua kutangaza hivyo ili kutoa tahadhali ili vurugu zisije kutokea pale watu ambao hawajafunga (hata baadhi ya waislamu hawafungi)wasije wakacharazwa au kufanyawa vurugu na watu waliofunga ,je zikitokea vurugu si ndio hiyo hiyo serikali itawajibika ?Kwa Zanzibar haya mambo yapo kuanzia zamani na sio sasa tu.Kinachokatazwa si kula bali ni kula hadharani.Na kwa taarifa huko Zanzibar wakati wa mfungo hakuna hoteli au duka linalouza vinywaji au vyakula hadharani ,ukiondoa baadhi ya hoteli za kitalii na hizi za kawaida kama Maisara CCM na Ukumbi wa Magereza huko hata bia unazipata.
 
haya mambo buana....
basi tu wacha nipige kimya nisijechafua hali ya hewa...
 
Imani yako inakomaa kwa kukinzana na nafsi yako kujizuia kufanya mambo mabaya

Kuwazuia watu kufanya yale ambayo ni kipimo cha imani yako kwenye nafsi ni udhaifu wa imani yako kwenye nafsi yako.....

Kama wewe umefunga kutoka kwenye nafsi yako kwa imani yako kwanini uhangaishwe na mtu anayekula na kunywa.....!!??

Sasa unakuwa umefunga kwa imani au umejizuia....!!??

Kipimo cha imani ni kipi hali unazuia majaribu kwenye imani yako...,,!!?

Ni mtazamo tu
Aisee usitumie rai zako kwny dini za watu, ndio maana dini hakuna maoni ya watu mle kama binge la katiba. Aliyekwambia nani kwamba ili imani ipande ukakae na sehemu hatarishi.yaani ili uonekane unaimani inabidi unaenda clabu usiku unashinda baa au unalala chumba kimoja na makahaba halafu sasa ukiweza kuizuia nafsi yako humo kujiingiza kweny hayo majanga ndio imani yako iko juu? Amaa kweli hapo umewaza, dini sio fikra zako ni mwongozo kutoka kwa muumba mbingu na ardhi. Hujui, uliza utafahamishwa. Dini inakutaka usikaribie uovu ili usije ukatumbukia ndani yake. Usikaribie zinaa, sio uingie mpaka ndani halafu ndio ukishinda imani yako iko juu.
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Huwezi kuepuka hali halisi ya zanzibar. Ingawa Tanzania haina dini lakini kwa zanzibar karibu asilimia 95 ni waislamu. Kwa karne na karne wale ambao siyo waislamu wamekuwa wakiheshimu mwezi huu kwa kula faraghani na sioni sababu.
Mambo haya hayako zanzibar peke yake kwani hata saudia waislamu wengi huko nyuma walikuwa wanatoka nje ya nchi wakati wa kipindi hiki nao pia wanazuiwa kufanya hivyo.
 
Nimeulizwa kuhusu kujuzu au kutokujuzu kwa Mwislamu kuuza chakula ‎mkahawani (kwenye magenge) mchana wa mwezi wa Ramadhani, ‎NANUKUU:-‎
‎“assalaam alaykum mm nauliza jee ina faa muislamu kuuza chakula mwezi ‎waramadhani mchana hali ndo biashara yake hana nyengine” ‎

JIBU

BISMILLAH

Haijuzu. Haram! ‎
Sharia za Mwenyezi Mungu, khasa Sharia-mama ‎ألأصول‎ -si matawi ‎الفروع‎- ‎zinawahusu vile vile wasiokuwa Waislamu, isipokuwa wanatakiwa ‎KWANZA wasilimu kisha watii sharia. Sharia-mama ni kama Tawhidi, ‎Swaumu na Swala, hizi ni Sharia za msingi, nguzo za kufuatwa na ‎wanaadamu wote, isipokuwa wanatakiwa wasilimu kwanza: wawe Waislamu ‎kwanza.‎
Watu wa Peponi watawauliza makafiri, watu wa Motoni:‎
‎{ ‎مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ {42} قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ {43} وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ {44} وَكُنَّا ‏نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ {45} وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ {46‏‎}‎
‎“Ni kipi kilichokutokomezni kwenye kina cha Moto? Waseme: Hatukuwa ‎miongoni mwa wenye kuswali. Wala hatukuwa tunawapa chakula masikini. ‎Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katiika maovu. Na tulikuwa ‎tukikana Siku ya Kiyaa.” Al-Muddathir: 42-46. ‎

Hivyo, hata wanaokana kuwepo Siku ya Kiyama; makafiri, wanatakiwa ‎wawe miongoni mwa wenye kuswali, na wataadhibishwa kwa kutokuswali. ‎Vivyo hivyo, kwa kutokufunga na kadhalika. Hakuna khilafu miongoni ‎mwa wanazuoni kuyusu wasiokuwa Waislamu kuwajibika mbele ya sharia-‎mama. Kuna khilafu ndogo, tu, kuhusu kuwajibika au kutowaajibika mbele ‎ya matawi ya sharia, kama kutia nia ya kufunga, kutawadha kwa swala, ect., ‎ect. Ama sharia-mama hakuna khilafu.‎
Hivyo, haijuzu kumuuzia chakula mwislamu au asiyekuwa mwislamu, ‎mchana wa Ramadani. Haramu. Ni kumsaidia kuasi.‎

Kudai kwamba kuuza chakuka ndiyo kazi yake, na hana kazi nyengine, ni ‎madai ya kitoto, na hakumaanishi kuwa atakufa njaa iwapo hakuuza chakula ‎mchana, kwa muda wa michana 30. ‎

Na hakuzuwiwa kuuza usiku, au kuanzia magharibi hadi kabla ya alfajiri. ‎Kwanini iwe kutokuuza chakula kwa muda wa masaa kama 12, kwa michana ‎kama 30, katika mwaka mzima, kuwe kutamfilisisha au kumfanya awe ‎masikini au akose ajira? Je, alipoanzisha biashara hiyo alikuwa akiwauzia ‎wasiokuwa Waislamu tu, hadi adai, hii leo, kwamba kama hajauza mchana ‎atapata shida? Haijuzu, haramu!‎

Baadhi ya wanazuoni wanasema hata kama ana mfanyakazi wa nyumbani, ‎ambaye si Mwislamu, na ambaye masharti ya kazi yake ni pamoja na kumpa ‎chakula cha mchana, basi bado hapaswi kumpa chakula mchana, katika ‎Ramadhani. Ampe chakula chake magharibi pale wanapokula wao, na ampe ‎vile vile cha mchana, kabla ya kuchomoza alfajiri- wanapokula daku wao, ili ‎kama anataka kujiwekea chakula chake hicho hadi mchana unaofuatia, basi ‎huo ni utashi wake mwenyewe, ajifnyie mwenyewe. Hatokufa njaa kwa ‎kutokula mchana. Mbona waajiri wao hawafi wala hawaumwi.‎

Kwa kweli, watu wengi, ambao si Waislamu na hawafugi, bado wanaheshimu ‎mchana wa Ramadhani na hawali mbele ya ndugu zao Waislamu. Ni baadhi ‎ya wanaojiita Waislamu tu, ndio wenye ukorofio huo wa kudai kuwa ‎anawauzia wasiokuwa Waislamu, kwa sababu kuuza chakula ndiyo kazi ‎yake, hana kazi nyengine!‎
‎ ‎
Hivyo, midhali hana sababu halali ya kutokufunga, na akawa mtu mzima wa ‎kuwajibika binafsi, basi hapaswi kupewa chakula mchana wa Ramadhani ‎mpaka magharibi. ‎
Kwa ufupi, haifai kwa Mwislamu kuuza chakula kilichokwisha pikwa kwa ‎walaji wa mchana, tena kwenye mkahawa wake. Wanaingia humu wauza ‎vyakula magengeni, vile vile. ‎

Usisaidie watu kuvunja sharia za Mwenyezi Mungu. Waache wavunje ‎wenyewe! ‎وتعاونوا على البر والتقوى ولا تعاونوا على ألإثم والعدوان‎ ‎
Naam, wagonjwa, wazee, wasafiri na kadhalika wanaweza kupewa chakula ‎mchana wa Ramadhani, maana hawana ulazima wa kufunga Ramadhani, ‎kwa muda wa kuwa na venye kuwaruhusu kula.‎
‎ ‎
والله أعلم

وبالله التوفيق

السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم‎ ‎

Imejbiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza ‎chchote, na kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye ‎Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

kcwajawema@gmail.com
 
Sasa mfano mwanamke ni mjamzito harafu ni mfanyakazi hashindi nyumbani atakula wapi iwapo magenge na maduka ya vinywaji na chakula hayauzi chakula? Nimewaza tu, maana mimi nikiwaga kwa hali hiyo kula hua ndo jambo la kubwa kwangu, kuna mtu anaweza nisaidia kujibu hili?
 
Aisee usitumie rai zako kwny dini za watu, ndio maana dini hakuna maoni ya watu mle kama binge la katiba. Aliyekwambia nani kwamba ili imani ipande ukakae na sehemu hatarishi.yaani ili uonekane unaimani inabidi unaenda clabu usiku unashinda baa au unalala chumba kimoja na makahaba halafu sasa ukiweza kuizuia nafsi yako humo kujiingiza kweny hayo majanga ndio imani yako iko juu? Amaa kweli hapo umewaza, dini sio fikra zako ni mwongozo kutoka kwa muumba mbingu na ardhi. Hujui, uliza utafahamishwa. Dini inakutaka usikaribie uovu ili usije ukatumbukia ndani yake. Usikaribie zinaa, sio uingie mpaka ndani halafu ndio ukishinda imani yako iko juu.
Samahani ndugu kama umekwazika na maoni yangu.....sikuwa na nia ya kukashifu au kuingilia imani za watu nilikuwa tu najaribu kutoa maoni yangu kama mwanajamii kwenye jamii ya watu wenye mchanganyiko wa imani mbali mbali.....

Hapo umezungumzia mtu wa imani kujiweka mbali na matendo maovu ambapo kwa mwezi ramadhani kula mchana ni moja ya matendo ovu....lakini pia bila ya kusahau tunaishi kwenye jamiii ya watu wenye mitazamo tofauti ya kiimani sasa kwanini wewe ambaye umefunga ukajiweka kando au ukajiepusha na maeneo ambayo watu wanapata chakula kuliko kuzuia watu wengine wasile kabisa...!!??

Kitabu cha imani yako kina semaje kwenye mwezi kama huu kuhusu watu wa imani nyingine ambao wanayafanya ambayo kwenu ni haramu likiwemo la kula mchana......!!?
 
Ndio maana ya Marekani ni Marekani na ya Zanzibar ni Zanzibar,mimi ni mla nguruwe kaka wala sio Muislamu ila najaribu kuelezea tu hali halisi ya jinsi ninavyoijua Zanzibar
Kama ndivyo kuna tatizo, maana ni double standard tayari! Ukiwa eneo la waislam wengi hakuna kitu kama minority rights lakini muislam akiwa eneo la waislam wachache minority rights ipo.
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Pole ndio unaona leo ... mbona ipo kitambo tu ...
 
Samahani ndugu kama umekwazika na maoni yangu.....sikuwa na nia ya kukashifu au kuingilia imani za watu nilikuwa tu najaribu kutoa maoni yangu kama mwanajamii kwenye jamii ya watu wenye mchanganyiko wa imani mbali mbali.....

Hapo umezungumzia mtu wa imani kujiweka mbali na matendo maovu ambapo kwa mwezi ramadhani kula mchana ni moja ya matendo ovu....lakini pia bila ya kusahau tunaishi kwenye jamiii ya watu wenye mitazamo tofauti ya kiimani sasa kwanini wewe ambaye umefunga ukajiweka kando au ukajiepusha na maeneo ambayo watu wanapata chakula kuliko kuzuia watu wengine wasile kabisa...!!??

Kitabu cha imani yako kina semaje kwenye mwezi kama huu kuhusu watu wa imani nyingine ambao wanayafanya ambayo kwenu ni haramu likiwemo la kula mchana......!!?
Nimejaribu kuleta fatua nzima IPO hapo juu, ya mwanchuoni wetu Wa tanzania , amejibu swali lako na Mimi nimenukuu, kwa sababu dini si maoni yetu Bali ni evidences. Yaani unapozungumza jambo yataka uwe na ushahidi nalo, si hulka jazba wala hamasa. Pitia hiyo kwanza kama hukutosheka niulize nikudadavulie, napenda watu wa sampuli yako wanapenda kuelewa upande mwingine unasemaje bila jazba wala mihemko. Dini ni kuelimishana kistaarabu.
 
Sasa mfano mwanamke ni mjamzito harafu ni mfanyakazi hashindi nyumbani atakula wapi iwapo magenge na maduka ya vinywaji na chakula hayauzi chakula? Nimewaza tu, maana mimi nikiwaga kwa hali hiyo kula hua ndo jambo la kubwa kwangu, kuna mtu anaweza nisaidia kujibu hili?
Vyakula vinaozwa muda wote wa Ramadhani na ndio maana watu wanafuturu. Vyakula ambavyo havijapikwa ni masaa 24 vipo ila vile ambavyo ni tayari kwa kuliwa haviuzwi mpaka ufike muda wa kufungua swaum, ama kwa mjamzito awe muislamu au si muislamu anayoruhusa ya kula mchana wa ramadhani; mradi kando na plate yake ale kwa raha zake, ama kuhusu chakula anaweza akaanda usiku asubuhi akaenda nacho kazini, au akipata kilicho ready ale kwa falagha. Na si kujifaragua na kujisosomola barabarani.
 
  • Thanks
Reactions: nao
serikali hiyo kiuhalisia ndio hivyo ni muungano tu ndio unawabana kuwa rasmi nchi yenye kufuata miongozo ya dini
ingekuwa si muungano ingekuwa inaitwa jamhuri ya kiislam ya watu wa zenjibar...
 
wakristo 90% hawafung kwa resma wala hawafatiliii dunia nzima n waislam peke yao wanoheshm mwez wao wa kufunga na utaona mamilion kwa mabilion ya watu wakijaaa misikitin zaidi hata ya kipindi cha kawaida.

uksema zanzibar harufu ya udini inanukia utakuwa huijui zanzibar ...zanzibar 99.5 % ni waislam tupu tena pure ivo serikali ya mapinduzi dini yake ni uislam sijui nyie msiokuwa na dini
 
Nina wanangu kama saba hivi Next month tumepanga kuja Zanzibar...Ntakunywa Juicy na Keki Darjani pale nione wa kunikamata [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom