Zanzibar 2020 Zanzibar: Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 toka maeneo mbalimbali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
871
1,000
Wakuu,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia kutoka Zanzibar. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.


ORODHA RASMI YA WAGOMBEA WANAOWANIA URAIS KWA MUJIBU WA ZEC
ORODHA RASMI YA WAGOMBEA WANAOWANIA UBUNGE KWA MUJIBU WA ZEC

MKOA WA KASKAZINI UNGUJA - MAJIMBO 8


Wilaya ya Kaskazini A

Chaani -
Kijini -
Mkwajuni -
Tumbatu -
Nungwi -

Wilaya ya Kaskazini B
Donge -
Mahonda -
Bumbwini -


MKOA WA KUSINI UNGUJA - MAJIMBO 5

Wilaya ya Kati

Chwaka
Uzini
Tunguu

Wilaya ya Kusini
Makunduchi
Paje


MKOA WA MJINI MAGHARIBI - MAJIMBO 19

Wilaya ya Magharibi A

Mtoni -
Bububu -
Mfenesini -
Welezo -
Mwera -

Wilaya ya Magharibi B
Dimani -
Fuoni -
Kiembesamaki -
Mwanakwerekwe -
Pangawe -

Wilaya ya Mjini
Kwahani
Amani
Magomeni
Shaurimoyo
Malindi
Kikwajuni
Chumbuni
Jang'ombe
Mpendae


MKOA WA KASKAZINI PEMBA - MAJIMBO 9

Wilaya ya Micheweni

Micheweni -
Tumbe -
Wingwi -
Konde -

Wilaya ya Wete
Mtambwe -
Pandani -
Gando -
Kojani -
Wete -


MKOA WA KUSINI PEMBA - MAJIMBO 9

Wilaya ya Chake Chake

Chake Chake -
Wawi -
Ziwani -
Chonga -
Ole -

Wilaya ya Mkoani
Mkoani -
Mtambile -
Kiwani -
Chambani -

UPDATE

MAALIM SEIF APIGA KURA
Seif.jpg
Amefika ktk Kituo cha Garagara, Jimbo la Mwera na kupiga kura mapema leo. Asema ametiwa moyo na watu wengi kujitokeza kupigia kura ila Wananchi wengi wana malalamiko ya kutokuona majina yao kwenye vituo

------
DKT. HUSSEIN MWINYI APIGA KURA
Mwinyi.jpg

Mgombea Urais Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi akipiga kura. Ahimiza wananchi Zanzibar kujitokeza kupiga kura​

UPDATE
SAMIA SULUHU ATIMIZA HAKI YA KIKATIBA KWA KUPIGA KURA
Mama Samia amepiga kura katika Kituo cha SOS Mombasa Zanzibar. Amewasihi Watu waliopo nyumbani na wanahofia usalama wao wajitokeze kupiga kura kwasababu kila kitu kipo vizuri na zoezi linakwenda haraka.

2604023_Samia.jpg

UPDATE
DKT. SHEIN APIGA KURA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amepiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Unguja. Dkt. Shein ambaye ameongoza Zanzibar tangu mwaka 2010 anamaliza muda wake

Shein.jpg


UPDATE
SALUM MWALIMU APIGA KURA
Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Mhe. Salum Mwalimu akishiriki zoezi la Upigaji wa kura katika Kituo cha Kisiwandui chumba namba 3 kilichopo katika Jimbo la Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Mwalimu.jpg


UPDATE
HAMAD RASHID APIGA KURA

Mgombea Urais Zanzibar kupitia chama cha ADC, Hamad Rashid akipiga kura katika kituo cha Shule ya Fidel Castro kisiwani Pemba ambapo amesema zoezi hilo limeenda vizuri

Hamad.jpg
 

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
871
1,000
UPDATES:

12:30pm

Idadi kubwa ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Polisi wameonekana wakiranda maeneo mengi ya Jiji la Zanzibar tangu alfajiri, ikiwa ni siku ya kupiga kura.

Wakiwa ndani ya magari na wengine kutembea barabarani kwa makundi, wameonekana wamebeba silaha huku wengine wakifunika nyuso zao kwa soksi-uso nyeusi.

Pamoja na kuwepo kwa hali ya utulivu, lakini hali hiyo inaelezwa kuogofya baadhi ya wapigakura, hasa katika majimbo yenye idadi kubwa ya wanachama na mashabiki wa vyama vya upinzani, hasa ACT-Wazalendo.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous Faina amesema kwamba kuwepo askari wa usalama siku ya kupiga kura siyo kosa kwani "wanalinda haki na kuhakikisha kila mtu anakuwa huru kuchagua kiongozi anayemtaka bila kushurutishwa."

Mwandishi wetu ametembea baadhi ya majimbo na kuona wanajeshi na askari wengine wakiwa wamebeba silaha ndani ya maeneo ya kupigia kura. Hatua hii inakatazwa na sheria kwani huenda ikaogofya wapigakura.

Katika Jimbo la Pangawe, Shehia ya Kijitoupele na kituo cha Shule ya Kijitoupele, wanajeshi sita wakiwa na silaha walionekana wakiwa ndani ya eneo la kituo cha kupigia kura. Jimbo hilo lina idadi kubwa ya mashabiki wa chama kikuu cha upinzani, AT-Wazalendo.

Aidha, imeshuhudiwa idadi kubwa ya askari katika Jimbo la Welezo, wakiranda kutoka kituo kimoja cha kupigia kura hadi kingine wakiwa na magari ya deraya, magari yenye maji ya kuwasha na magari mengine.

Katika majimbo ya Raha Leo, Mwanakwerekwe, Bububu na Chambani, hali ilikuwa tofauti, idadi ndogo ya askari walishuhudiwa wakizunguka vituo vya kupigia kura, wakiwa na virungu na wengi wa askari hao wakiwa wanawake.

Hadi mchana wa leo, hali ya usalama imekuwa shwari na hakuna taarifa za vurugu wala rabsha katika maeneo ya vituo vya kupigia kura au barabarani katika maeneo mengi ya Unguja.

UPDATE 2:
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,838
2,000
Kiti cha mbele, kabisa hapa sishuki Mchamba Wima wala Kibanda Maiti.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,860
2,000
Huu ni wakati sahihi wa kuchukua hatua za kidwanzi dhidi ya upuuzi wowote ule wenye sura ya dhuluma.
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
721
1,000
Aibu matokeo ya jana ya uchaguzi wa mapema Zanzibar,askari kibao wamepigia ACT Wazalendo, wanachofanya ZEC ni kuziharibu kwa kuongeza michoro.

Na hapa Tanganyika wazalendo wengi wamekasirika kwa kuonekana wanaothaminiwa ni walinzi wa kigeni kutoka nchi jirani ambao ndio hutoa ulinzi kwa misafara ya viongozi wa CCM.
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,765
2,000
Matumizi ya nguvu hayajawahi shinda nguvu ya umma. Laiti ccm ingetatua kero za muungano na kuwasikiliza waznz wanataka muungano wa aina gani yasingetokea haya.
 

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
579
1,000
Aibu matokeo ya jana ya uchaguzi wa mapema Zanzibar,askari kibao wamepigia ACT wazalendo,wanachofanya Zec ni kuziharibu kwa kuongeza michoro.
na hapa Tanganyika wazalendo wengi wamekasirika kwa kuonekana wanaothaminiwa ni walinzi wa kigeni kutoka nchi jirani ambao ndio hutoa ulinzi kwa misafara ya viongozi wa ccm
Labda hao ndio wazalendo
 

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,078
2,000
MWENYEKIT WANGU WACCM AMENIAIBISHA SANA KAMA ANAJIAMINI MIAKA MITANO AMEITENDEA HAKI KWANINI ANAHANGAIKA KUZIMA MITANDAo?
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,797
2,000
Mungu Baba ninatubu kwa dhambi zangu na taifa letu Tz, tuonee huruma, tujalie hekima na busara tukafanye wajibu wetu kupiga, kuhesabu, kutangaza matokeo kura itakayo leta HAKI na ustawi wa taifa letu.

Amina
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
721
1,000
Wananchi waPemba wazuia masanduku yaliokuwa na kura zilizokwishapigwa kuingizwa kwenye kituo cha kupigia kura ,polisi wametaka kutoa sapoti kwa nec na zek kuyapitisha masanduku hayo,hapo ndipo kindende kilipoanza.

Polisi ni nyinyi au watu wanatumia uniform zenu? Mabomu yameanza tena ,polisi hawachelewi kupoteza uvumilivu waPemba wameshajitolea kufa kupona kulinda haki yao.
 

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
15,968
2,000
Aibu matokeo ya jana ya uchaguzi wa mapema Zanzibar,askari kibao wamepigia ACT wazalendo,wanachofanya Zec ni kuziharibu kwa kuongeza michoro.

na hapa Tanganyika wazalendo wengi wamekasirika kwa kuonekana wanaothaminiwa ni walinzi wa kigeni kutoka nchi jirani ambao ndio hutoa ulinzi kwa misafara ya viongozi wa ccm
Uzuri wa kura ni siri
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom