Serikali kujenga nyumba za wafanyakazi Hospitali za Wilaya Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kwa kipindi kifupi kijacho Serikali itaanza kuweka mawe ya msingi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika hospitali za Wilaya ikiwemo Kinyasini ya Wilaya ya Wete, Vitongoji Wilaya ya Chakechake, Micheweni Wilaya ya Micheweni kwa upande wa Pemba.

Pia upande wa Unguja kwa Hospitali ya Kitogani Wilaya ya Kusini Unguja, Pongwe Wilaya ya Kati, Pangatupu Wilaya ya Kaskazini B na Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipoweka Jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa nyumba za Wafanyakazi katika Hospitali ya Abdulla Mzee Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe: 03 Januari, 2024.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa matayarisho ya ujenzi wa nyumba hizo yameanza ili kuendeleza mafanikio ya sekta ya afya nchini kwa kuondoa tatizo la kukosekana kwa Daktari au wafanyakazi wengine wa sekta ya Afya wanapohitajika kutoa huduma katika hospitali hasa wakati wa dharura.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amefarijika kushuhudia kwa vitendo ahadi iliyotolewa na Serikali ya China kutimia kufanikisha mradi wa ujenzi wa nyumba za Wafanyakazi katika Hospitali ya Abdulla Mzee .

Vilevile amesema mradi huo utawapunguzia masafa Wafanyakazi na kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni vipaumbele vya Serikali ilivyoelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025.
FB_IMG_1704306303083.jpg
View attachment 2861210
FB_IMG_1704306311115.jpg
View attachment 2861212View attachment 2861213
IMG-20240103-WA0177.jpg
IMG-20240103-WA0179.jpg
IMG-20240103-WA0176.jpg
 
Back
Top Bottom