Zanzibar kunyimwa uanachama wa FIFA na CAF ni chuki kisiasa au kukosa vigezo?

Kibosho1 Tatizo ni kuwa Tanzania Bara au Tanganyika wamejiunga ndani ya FIFA kwa kupitia mlango wa Tanzania. Walitakiwa wajisajili kama Tanzania Bara. Sasa Zanzibar ipo ndani ya Tanzania kwahiyo ni ngumu kupata uanachama kwa kuwa tayari wamo ndani ya fifa kwa kupitia mlango wa Tanzania.
Suluhisho la hili ni Tanzania Bara kubadili Jina lao na mipaka yao ndani ya Fifa kitu ambacho Serekali ya Bara haitaki kiroho mbaya tu.

Mbali na hivo TFF ikishirikiana na SMT licha ya kuwabania Zanzibar kupata uanachama pia wanagoma kuwapa Zanzibar mgao wowote unaotokana na FIFA. Kwa maana Si tu Hawataki wenzao wapate uanachama bali hata Mgao hawataki kuwapa.

Huu Muungano una madudu mengi sana
 
Na Somali nao, Djibout, Malawi, Eritrea, Mauritius, Seychelles, Burundi na nyengine mfano wa hizo ulizisikia zimefika wapi.

Shida ya Zanzibar ni moja tuu imekaliwa kimabavu na Jamhuri ya Tanganyika kiasi kwamba haiwezi kufanya ya kwake hata kwenye sekta ya michezo.

Na hii ni kaana hata kwa hiyo inayoitwa Taifa Stars ikiingua kwenye mashindano ya kimataifa huwa haifiki popote hubaki kuhamasishana tuu na kujipa moyo mnajifunza.
 
Bora uvunjike tu. Mbona China na Hong Kong wote wanachama wa fifa ?
 
Asante kwa jibu zuri
 
Sisi watanzania na Waafrika kwa ujumla tuna matatizo sana ya kiakili, yani mtu yupo tayari kuua cha nyumbani na wakati huo huo anatetea cha nje. Mtu na akili zake timamu hawezi kusema Zanzibar sio nchi.
Na ndo maana huko Ulaya tunabaguliwa maana sisi wenyewe hatujitambui
 
Afadhali ww umeandika cha maana kuliko hao wanaosema Zanzibar sio nchi.
 
Afadhali ww umeandika cha maana kuliko hao wanaosema Zanzibar sio nchi.
Kaandika vizuri sana lakini bado. Mfano Kosovo ni jimbo la Serbia na Serbia ni mwanachama wa fifa, mbona imepewa uanachama juzi juzi? Hong Kong nayo ni nchi?

Bado sijaona kigezo cha zbar kunyimwa huu uanachama eti kisa ipo Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…