Imekuwaje Kenya iliyosimamishwa na FIFA kujihusisha na shughuli za kimichezo imetoa muamuzi wa kisimamia mechi ya CAF CC ya Simba Vs Orlando Pirates?

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
242
450
Habari wana jukwaa. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada yangu, Mnamo tarehe 22/02/2022 shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) lilizipiga marufuku nchi za Kenya na Zimbabwe kujihusisha na shughuli zozote za soka kutokana na Serikali zao kuingilia mashirikisho ya soka ya nchi hiyo kitu ambacho ni kinyume na kanuni za FIFA na mpira kwa Ujumla.

Naomba ninukuu baadhi ya maneno ya Raisi wa FIFA akisoma hukumu hiyo alisema;
"Bila ya kuathiri uchunguzi wowote wa mamlaka ya kitaifa au vyombo vingine vya mahakama, Baraza la Fifa pia liliamua kusimamisha Shirikisho la Soka la Kenya na Chama cha Soka cha Zimbabwe mara moja kutokana na kuingiliwa isivyofaa na serikali ," Infantino alisema.

Ila katika hali iliyonikanganya leo CAF (Shirikisho la Soka barani Africa) kupitia shirikisho la soka nchini, TFF, limetoa orodha ya masimamizi na waamuzi wa mchezo wa robo fainali kati ya Simba Vs Orlando Pirates utakaopigwa tarehe 17/4 na kuonesha jina la Mkenya David Mwangi ambaye ndiye atakuwa kamishina wa huo mchezo.

Hapo ndipo sijaelewa inakuwaje FIFA imeifungia Kenya kujihusisha na shughuli zozote za soka ila CAF inamteua Mtu kutoka Kenya awe kamishina wa mechi kubwa ya robo fainali? Au hukumu ya FIFA imepotezewa na CAF? Au imekaaje hii Wadau maana mpaka leo sijaona hukumu ya kutengua katazo la kujihusisha na soka kwa nchi za Kenya na Zimbabwe.

Wasalaam

20220408_162534.jpg
 
View attachment 2180624
Subiri kidogo ninaandaa nondo za kujibu swali lako.
 
Back
Top Bottom