Serikali 3 au 1 ni mwisho wa muungano. Zibaki 2, Zanzibar iwe na hadhi maalumu kama Hong-Kong

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,350
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.

Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati huo sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.

Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.

1. Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la sasa la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.

2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.

3. Zanzibar ipewe rasmi kikatiba 10% ya viti vya ubalozi.

4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.

5. Kuundwe bunge la seneti lenye wawakilishi 2 kutoka kila mkoa Tanzania bara na Zanzibar. Hili liwe linapitisha bajeti na maamuzi yote kutoka bunge la sasa kwenda kwa Rais wa Tanzania.
 
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.

Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.

Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.

1.Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.

2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.

3. Zanzibar ipewe 10% ya viti vya ubalozi.

4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.
Naunga mkono hoja
 
Kwani huo muungano usipokuwepo kutatokea shida gani? Na kwa nini tuulazimishe uendelee kuwepo, huku wananchi walio wengi wakiwa hawautaki?

Mbona hiyo Zanzibar ikiwa nchi kamili bado tutashirikiana nayo tu kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki(EAC)? Au inaweza kukataa kujiinga, na badala yake ikaamua kujiunga na Jumuiya ya Kiarabu ya watu Oman?
 
Wewe na wananchi walio wengi ambao hawautaki mmefanya, mtafanya au mnaweza kufanya nini ili usiwepo??

Hapo kwenye OIC hapo ... utashangaa mchungaji anatoka Mbeya anatishia maandamano...hili Taifa Lina wajinga wengi sana
 
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.

Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.

Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.

1. Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.

2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.

3. Zanzibar ipewe 10% ya viti vya ubalozi.

4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.

Hii set up yako nzuri sana
Tunaweza tazama pia Scotland na UK
Au Monaco na France...
Binafsi nafikiri umewwaza kizalendo Sana
 
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.

Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.

Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.

1.Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.

2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.

3. Zanzibar ipewe 10% ya viti vya ubalozi.

4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.
Serikali mbili au tatu hazitaweza kuimarisha muungano hata chembe.
Zanzibar yenye mamlaka yake kwenye mambo yanayoitwa yasiyo ya muungano itatamani kuwa na mamlaka kamili kwa mambo yote. Na hili linakwenda hatua kwa hatua. Linganisha mamlaka ya Zanzibar huko nyuma na sasa.
Tanganyika(Hii ipo kwa sababu Zanzibar ipo) kwa upande mwingine, kwa kadiri mamlaka ya Zanzibar yanavyozidi kujitanua, itaona kama yenyewe tu ndio iliyopoteza mamlaka yake tu.

Suluhisho ni serikali MOJA nchi MOJA TANZANIA.
Kiongozi akiwa katoka Zanzibar itakuwa sawa na aliyetoka Tabora tu maana ni Mtanzania. Hakutakuwa na Mzanzibari na Mzanzibara. Yaani mzanzibari amiliki ardhi nanjilinji sawasawa na muchari amiliki ardhi chakechake au matangatuani huko maana kote ni ardhi ya Tanzania.
 
tugawane , mbao mtu akiwa nje ya muungano ndio atajua faida na hasara. alitaka kuungana atakuwa na adabu.
hawastahili hata asilimia Moja ya vitu vya ubalozi kwani hawachangii hata senti Tano kuendesha nchi
Tatizo mnaotaka kugawana mbao hamna chochote mnachoweza kufanya, mnaishia kuonekana wahaini au kupuuzwa tu na wenye nguvu halisi za kuamua haya mambo.
 
Serikali mbili au tatu hazitaweza kuimarisha muungano hata chembe.
Zanzibar yenye mamlaka yake kwenye mambo yanayoitwa yasiyo ya muungano itatamani kuwa na mamlaka kamili kwa mambo yote. Na hili linakwenda hatua kwa hatua. Linganisha mamlaka ya Zanzibar huko nyuma na sasa.
Tanganyika(Hii ipo kwa sababu Zanzibar ipo) kwa upande mwingine, kwa kadiri mamlaka ya Zanzibar yanavyozidi kujitanua, itaona kama yenyewe tu ndio iliyopoteza mamlaka yake tu.

Suluhisho ni serikali MOJA nchi MOJA TANZANIA.
Kiongozi akiwa katoka Zanzibar itakuwa sawa na aliyetoka Tabora tu maana ni Mtanzania. Hakutakuwa na Mzanzibari na Mzanzibara. Yaani mzanzibari amiliki ardhi nanjilinji sawasawa na muchari amiliki ardhi chakechake au matangatuani huko maana kote ni ardhi ya Tanzania.
Kama wewe ungekuwa Mzanzibari sababu gani hasa za msingi ungezikubali kuifanya nchi yako kuwa mkoa mmojawapo tu wa mikoa mingi ya Tanzania ?
 
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.

Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati huo sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.

Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.

1. Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.

2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.

3. Zanzibar ipewe 10% ya viti vya ubalozi.

4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.
Kwani hadi sasa Zanzibar haina hadhi maalum?
 
Tatizo mnaotaka kugawana mbao hamna chochote mnachoweza kufanya, mnaishia kuonekana wahaini au kupuuzwa tu na wenye nguvu halisi za kuamua haya mambo.
kama viongozi waliopo madarakani wameshindwa kuheshimu katiba ya Muungano unafikiri Muungano upo?
idea ya Nyerere ilikuwa watu wakishaona faida ya Muungano wadai serikali Moja na nchi Moja ila hayo mawazo hayapo ni Bora Kila mtu ajitegee kivyakevyake
 
Zanzibar ni ndogo sana kupewa 10pc ya Diplomatic Missions.

Wapewe Mamlaka Kamili, mambo ya kuogopa kuwa pako wazi sana ni ushamba, mbona hatulalamiki kuhusu Comoro?
 
Back
Top Bottom