Zanzibar Kumekucha

Mkuu.
Unaelewa kuwa kuna nchi ambazo ni visiwa kama Zanzibar?
Sychelles. Mauritius, Cape Verde..nchi hizi zipo Afrika.....je unaelewa vyanzo vyao vya mapato?

Lakini sisi Tanganyika aka Tanzania bara wenye vyanzo vya mapato....hayo mapato yako wapi? mapato yanayokusanywa yanamsaidia vipi mwananchi wa kawaida?

Nilipopitia historia nilijifunza kuwa Zanzibar walikuwa na uchumi bora kuliko wa Tanganyika kabla ya Muungano.

Wao uchumi wanao, na sisi uchumi tunao lakini "tumeukalia" kwa maneno ya Nyerere.

Tatizo ni viongozi tu.

Nonda at work, plz usipotoshe Nonda uchumi wa zanzibar ulikuwa mzuri sio kabla ya union bali sema kabla ya Mapinduzi, ni mapinduzi ambayo yaliwafukuza masettlers wengi wa kiarab na kupunguza imani ya wafanyabiashara hao kuwekeza zanzibar,kama ilivyokuwa huku bara na azimio la arusha-achana historia ya maskani. Karume akakuta pesa akatumia bila kuwekeza ktk return endelevu ili kuwa na revenue endelevu-zilipoisha kwisney. Kwanini kila falure yenu nyie zenj mnadai ni bcz Tanzania?(eh sory ni Darnyika)!
 
Wazanzibar wanataka uhuru wao sasa, wana bendera, nyimbo ya taifa na bunge. Sidhan kama kuna mtanganyika ana jua faida ya muungano kama wazanzibar.
Iitishwe kura ya maoni kuuvunja, nadhani matokeo ya watanganyika yatakuwa 98% uvunjike
 
Tatizo si muungano feki, bali ni viongozi wachache walioamua kujinufaisha wao na familia zao kupitia muungano na si wananchi. Wazanzibari navyowajua mimi, wakiamua jambo hawashindwi kumwaga damu kwao haoni shida, haki yo kama imepokonywa wapewe.
 
HILI NDILO TATIZO LA VIONGOZI KUTOWASHIRIKISHA WENYENCHI (wananchi) KATIKA MAAMUZI MAKUBWA YANAYOWAHUSU... SISHANGAI WALA SITOSHANGAA KWANI HATA TANGANYIKA HAINA FAIDA NA MUUNGANO HUO KIUCHUMI LABDA KISIASA!!!

makosa kama haya yanataka kujitokeza kwenye KATIBA mpya!! wanashirikishwa WANASIASA badala ya WANANCHI (kwa niaba ya...)
 
Nonda at work, plz usipotoshe Nonda uchumi wa zanzibar ulikuwa mzuri sio kabla ya union bali sema kabla ya Mapinduzi, ni mapinduzi ambayo yaliwafukuza masettlers wengi wa kiarab na kupunguza imani ya wafanyabiashara hao kuwekeza zanzibar,kama ilivyokuwa huku bara na azimio la arusha-achana historia ya maskani. Karume akakuta pesa akatumia bila kuwekeza ktk return endelevu ili kuwa na revenue endelevu-zilipoisha kwisney. Kwanini kila falure yenu nyie zenj mnadai ni bcz Tanzania?(eh sory ni Darnyika)!

Nonda at work?
Nonda mpotoshaji?
Nonda ana historia ya Maskani?
Nonda mzenj?
Tanzania....Darnnyika?

Mkuu.
Ningependa sana kuchangia juu ya mchango wako lakini naona umejaa jazba.

La msingi bila ya kuweka wazi ni kuwa umekubali kuwa tatizo ni viongozi, inatosha. Viongozi wa Tanzania, Tanganyika na Zanzibar. Wa Zanzibar siwalaumu sana kwani wamebanwa sana na Muungano.
 
Mwl. aliwahi kusema "dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu". Hapa ni dhahiri watanganyika wanabaguliwa. Sidhani kama Mzee Karume alikuwa mjinga kiasi cha kuingia kwenye muungano ambao leo unaonekana FEKI. Yetu macho, kama sio kizazi hiki, basi vijavyo; endapo utavunjika, kuna siku tutatamani kurudi kwenye muungano lakini itakuwa "too late".

Kwani Zanzibar kama ni nchi ilidumu kwa miaka mingapi kabla ya huu Muungano? iweje leo eti ukivunjika Wazanzibar watajutia. Kwa mantiki gani hiyo? Tatizo la Tanzania ni uongozi mzuri wa nchi,hatuna uongozi wenye uwezo wa kuongoza nchi. Naamini Zanzibar bila Muungano watapiga hatua za kimaendeleo haraka. Mikakati inayotumiwa na serikali ya Muungano kuilazimisha Zanzibar iwe sehemu ya Tanganyika ,inalekea kugonga ukuta. Kwani kumekua na muamko wa hali ya juu kwa Vijana wa kizanzibar kudai nchi yao. Mifano ipo ,dunia ya sasa ni ya vijana. Huu muda unaotumiwa kuishikilia Zanzibar kama ungetumika kutatua matatizo ya kimaendeleo ya Tanganyika(Tanzania) basi taifa hili lingekua mbali sana.
 
Mwl. aliwahi kusema "dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu". Hapa ni dhahiri watanganyika wanabaguliwa. Sidhani kama Mzee Karume alikuwa mjinga kiasi cha kuingia kwenye muungano ambao leo unaonekana FEKI. Yetu macho, kama sio kizazi hiki, basi vijavyo; endapo utavunjika, kuna siku tutatamani kurudi kwenye muungano lakini itakuwa "too late".

sasa kwanini watanganyika wanabaguliwa Zanzibar? kwanini wazanzibar hawana furaha nu huu Muungano? there must be reasons as I know that Zanzibaris are very hospitable people on earth... just prove me wrong.
 
Sasa nawaogopa zaidi wanaoshabikia muungano kuvunjika. Ningeshukuru watu kulalamikia huduma nk. Sijui ni vipi muungano umezuia Pemba na Unguja kupendana na kuheshimiana. Sioni kivipi muungano unawafanya viongozi wanzanzibar na serikali yake kubagua kati ya Pemba na waunguja katika huduma za jamii na ni vipi kufa muungano kutabadili mila hizo. Lakin najua hili. Muungano haukuwahi kupendwa na hautalindwa na maadui wa Afrika. Zanzibar ikishafanikishiwa kujitenga na bara, waloitawala kale watarudi kwa nguvu zote bila kumhofia yeyote na kujigawia upya walojihalalishia kale sasa wakisaidiwa na vibaraka wao wengi. Hapo ndo mjue ugonvi na bara nako utaanza ni wapi mkondo wa mafuta waanzia na kuishia. Na ikiwa Bara kuna kinachohitajika na mabeberu, basi pa kupanga makombora yao waivaivamie Bar kama ilivo Libya pamepatikana. Nabaki kuwaogopa zaidi sasa wanaozungumzia muungano badala ya utawala bora na huduma za jamii.
 
Ipigwe kura ya maoni tu, kwa mujibu wa wazanzibari wengi nilioongea nao wao wana dhana kuwa bara inafaidika sana na maliasili za Zanzibar kuliko Zanzibar yenyewe (wananyonywa).

Serikali inatakiwa iwaulize wananchi wa pande zote mbili kama wanataka muungano uendelee (serikali moja au tatu) au uvunjike, tukiendelea kuikwepa kwepa hii issue itakuja kuwa out of hand tukaja kujuta.
 
Kwa hali ilivyo Zanzibar, wakati umefika maamuzi juu ya kuvunjika muungano yafanyike haraka iwezekanavyo. Asilimia 90% ya wazanzibari hawataki muungano. Kwenye kongamno inayoendelea zanzibar imejitokeza wazi kabisa kuwa muungano hautakiwi. Ushahidi wa kutosha umejitokeza kuwawezesha wazanzibari kutamka hadharani kwenye majukwaa kuwa muungano ni FEKI. Ni uonevu uliopitika kutaka kuiua Zanzibar. Wakati umefika ndoa yetu ya haramu tuivunje. Kuna ushahidi wowote wa ndoa hii?.

Huh,siku hiyo nitafurahi sana!
Tume wabeba mno aisee,assume wabunge wengi zaidi ya 20 toka zenji tunawalisha huku na idadi ya watu wanao wakilisha haizidi ile ya watu wanao wakilishwa na mnyika ubungo,....ondokeni fasta bana
 
Hata mimi nina mawazo kama yako, hayo ya rangi nyekundu.
Set up ya Muungano kama ilivyo leo ni tatizo ambalo linafanya hata kushughulikia hizo zinazoitwa "kero za muungano" inakuwa haiwezekani.

Ugumu upo, nani ana-nigotiate na nani?
Viongozi wa Tanganyika hawaonekani kiwazi kuwakilisha matakwa ya Tanganyika....lakini hata kulipoteza jina lenyewe tu la Tanganyika ni uhuni. Yaani viongozi wetu hawana uchungu hata kidogo na nchi yetu.

Mkuu hivi kuna nchi zilizoingia katika Muungano, shirikisho au jumuiya na kuua majina na serikali zao?
What we have is not a Union, it is just a big mess!
 
Ng'ombe hajui thamani ya mkia mpaka siku umekatika na nzi wamemjaa mwilini ndo anapoukumbuka umuhimu wake
 
Kwanini wasiuvunje leo jamani kesho tukaamka na Tanganyika yetu na mamwinyi wakafia mbali kwao?
 
Ng'ombe hajui thamani ya mkia mpaka siku umekatika na nzi wamemjaa mwilini ndo anapoukumbuka umuhimu wake
Mkuu.
Pia kuficha uchafu chini ya zulia ni hatari kwa afya ya binadamu.

Ukipata maradhi mengine huwa umequalify kupata nafasi katika cemetry!

Viongozi wetu kwa jinsi wanavyouendesha Muungano wanacheza na uhai wa Watanganyika na Wazanzibar.

Watu hufurahia jambo,kitu chenye tija lakini pia wanahaki kulalamika au kuvunja kitu ambacho hakina faida au tija.
 
Mwl. aliwahi kusema "dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu". Hapa ni dhahiri watanganyika wanabaguliwa. Sidhani kama Mzee Karume alikuwa mjinga kiasi cha kuingia kwenye muungano ambao leo unaonekana FEKI. Yetu macho, kama sio kizazi hiki, basi vijavyo; endapo utavunjika, kuna siku tutatamani kurudi kwenye muungano lakini itakuwa "too late".

Hapo nilipoweka red naomba utafakari yafuatayo: Mapinduzi ya Zanzibar yametokea January 12 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulifanyika tarehe 22 April 1964 (siku rasmi uliposainiwa mkataba wa Muungano) - jee ni siku ngapi? Jibu 112!. Sasa kama umewahi kusoma historia ya Zanzibar utajua kabisa kwamba kwa kipindi hicho hata Zanzibar yenyewe ilikuwa haijakaa sawa. Na hata huku Tanganyika hakukuwa sawa baada ya mutiny iliyotokea January 19 (wiki moja baada ya mapinduzi). Kama kila kitu kilikuwa poa haraka zilikuwa za nini?
 
Kwa hali ilivyo Zanzibar, wakati umefika maamuzi juu ya kuvunjika muungano yafanyike haraka iwezekanavyo. Asilimia 90% ya wazanzibari hawataki muungano. Kwenye kongamno inayoendelea zanzibar imejitokeza wazi kabisa kuwa muungano hautakiwi. Ushahidi wa kutosha umejitokeza kuwawezesha wazanzibari kutamka hadharani kwenye majukwaa kuwa muungano ni FEKI. Ni uonevu uliopitika kutaka kuiua Zanzibar. Wakati umefika ndoa yetu ya haramu tuivunje. Kuna ushahidi wowote wa ndoa hii?.
Hivi nani anayeuhitaji muungano zaidi ni Bara au Zenj,mi nafikiri Zenj wanahitaji zaidi huu muungano kwani kwa hali ilivyo wengi wao ni watu wanaotegemea bara kupata riziki zao ,tofauti na wabara ambao hawaitegemei Zenj hata kwa punje ya mtama,muungano ukivunjika watakaopata shida ni akina pangu pakavu kwani hawatakuwa na sehemu ya kusemea,na hao akina Hamadi itabidi waachie urua wanaopata bara na pia ina maana hao wapemba/wagunya waondoke bara au waishi kama wageni kwa kulipia vibali vya makazi ,sidhani kama mambo ya EAC kuwa muingiliano kuwa free kwa wanachama utaanza hivi karibuni,isitoshe ndugu zangu hao sijui watakaa wapi kwani Zenj imejaa na wanavyozaliana sijui itakuwaje hapo mbeleni kwani nyota ya kijani huko visiwani ni sawa na maji na mafuta
 
Wacha wavunje maana hautusaidii chochote katika serekali ya tanzania bara iliyojificha, kama talaka juu ya ndoa haramu iliyofungwa sisi tutakuwa wa mwanzo kutoa talaka ya kuvunja muunguna

HAWA wamanga tuwaacheni wajitenge! kwanza wamekuja bara kutuletea udini, ubaguzi majungu, nothing more!!
Wabaguzi, wadini wapenda majungu, wavivu yaani their just a chaos to us!!
 
haíingii akilini kuwa huku tunajadili muungano wa nchi 5 za ea na huku tunajadili kuvunja muungano wa tanganyika na zanzibar
tatizo sio kuwepo muungano.....tatizo ni muungano wenyewe haukupata kukubaliwa na wananchi....ulikuwa wa viongozi wawili..nyerere na karume...( ingawa hapa karume aliburuzwa -alilazimishwa...lakini wazanzibar walio wengi hawakuufarihia ....sijui tanganyika kama waliridhia as at that time hakuna wa kumpinga nyerere...
Unachoweza kuunusuru muungano huu ni viongozi waseme na kwa uwazi makosa yaliyofanywa na waasisi kuwa muungano hakua halali,mfumo wake haufai ni wa kiini macho( tanganyika imo ndani ya tanzania)nyerere hakua na nia njema juu ya zanzibar aliwahi kusema angeweza angevizamisha visiwa hivo baharini,lazima kumvalisha paka kengele
inachotakiwa ni kuitisha kura maoni..na kama kura itakubali basi pande zote zikae pamoja na kutengeneza muungano ambapo pande zote zinakuwa ni equal partners katika mambo ya muungano...lakini sio kama sasa ambapo muungano ni kama company na zanzibar wana hisa ndogo....
Kinyume cha hayo mustakabal wa muungano uko kwenye mashaka...
 
Huh,siku hiyo nitafurahi sana!
Tume wabeba mno aisee,assume wabunge wengi zaidi ya 20 toka zenji tunawalisha huku na idadi ya watu wanao wakilisha haizidi ile ya watu wanao wakilishwa na mnyika ubungo,....ondokeni fasta bana

Mkuu.
Unafahamu muundo wa bunge la EAC?
Kwa maoni yangu hivyo ndivyo ilipasa kuwa pia kwa bunge la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Hivyo basi tungekuwa na bunge la Tanganyika , Bunge dogo la Muungano na Bunge la Zanzibar.

Kuhusu idadi ya Wazanzibar kuwa ni ndogo,unasahau pia kuwa Zanzibar ni nchi ndogo, ingekuwa tuliungana na sychelles sijui tungesema nini?

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/country_profiles/1070461.stm#facts

BBC News - Seychelles country profile
 
Back
Top Bottom