Zanzibar Kumekucha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar Kumekucha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Falconer, Apr 3, 2011.

 1. F

  Falconer JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Kwa hali ilivyo Zanzibar, wakati umefika maamuzi juu ya kuvunjika muungano yafanyike haraka iwezekanavyo. Asilimia 90% ya wazanzibari hawataki muungano. Kwenye kongamno inayoendelea zanzibar imejitokeza wazi kabisa kuwa muungano hautakiwi. Ushahidi wa kutosha umejitokeza kuwawezesha wazanzibari kutamka hadharani kwenye majukwaa kuwa muungano ni FEKI. Ni uonevu uliopitika kutaka kuiua Zanzibar. Wakati umefika ndoa yetu ya haramu tuivunje. Kuna ushahidi wowote wa ndoa hii?.
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,757
  Likes Received: 6,046
  Trophy Points: 280
  Mwl. aliwahi kusema "dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu". Hapa ni dhahiri watanganyika wanabaguliwa. Sidhani kama Mzee Karume alikuwa mjinga kiasi cha kuingia kwenye muungano ambao leo unaonekana FEKI. Yetu macho, kama sio kizazi hiki, basi vijavyo; endapo utavunjika, kuna siku tutatamani kurudi kwenye muungano lakini itakuwa "too late".
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Nikifikiria vyanzo vya mapato Zenj kichwa kinauma. Mtauana sana. Tokeni sasa. Kura kama laki 2 za CCM zitapungua. Better
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sivyo kabisa nilivyotarajia kuyakuta humu ndani
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  for your information karume alikuwa hautaki muungano kwa sababu alikuja kugundua kapigwa mchanga wa macho na nyerere..by the way hata mimi nataka muungano uvunjike hauna maana yoyote
   
 6. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Ukifa Muungano itakuwa poa maana kifo chake kitaambatana na kifo cha CCM bara na CUF Itakufa kabisa.
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  huu utafiti wako unaoonesha kuwa 90% ya wazanzibiri hawautaki muungano umeufanya lini ili tusije elezea hisia zetu kwa kuwabambika wananchi.
  na ukitazama vyema utaona kwamba nchi zakimbilia kuungana na sio kujitenga kama utakavyo wewe.
  kama kuna mapungufu kwenye muungano kwanini usipendekeze yafanyiwe kazi?
   
 8. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Hamtokaa salama!! luv this one please watch it all! its' amazing stuff!!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. M

  Mr zam Member

  #9
  Apr 3, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha wavunje maana hautusaidii chochote katika serekali ya tanzania bara iliyojificha, kama talaka juu ya ndoa haramu iliyofungwa sisi tutakuwa wa mwanzo kutoa talaka ya kuvunja muunguna
   
 10. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni ndoa ya hiari pekee itakayodumu. Kama mmoja akiwa na mawazo kuwa kadanganya kuingia katika ndoa husika basi ndoa haipo hata ulazimishe. Tutafakari na tuamue kwa busara.
   
 11. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Kidole kimoja hakivunji chawa
   
 12. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jk inabidi asikilize kilio chao mapema sana kabla mambo hayajaharibika.kukaa kimya bila kufanya lolote ni dalili ya dharau na ndio maana wenzetu wamechoka na muungano.nawahurumia wazenji kwani muungano ndio unawafanya wawe kitu kimoja na pemba sivyo wangekuwa nao wameshtengana siku nyingi kwani hawapendani kwa dhati hata kidogo.
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ipigwe kura ya maoni........ndio suluhisho
   
 14. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.

  Dunia ya sasa ni juu ya umoja na ushirikiano. Tazama nchi za jumuiya ya Ulaya, wanazidi kuwa wamoja. Mifano ipo wazi, ni umoja wao katika kutafuta mafuta ya Afghan, Iraq, Kuwait, na sasa Libya kwa maendeleo ya watu wao na nchi zao. Zamu ijayo itakuwa ni Mafuta ya Unguja, Uranium ya Tanganyika, Mafuta ya Sudan ya Kusini, Mafuta ya Uganda, Angola n.k

  Jumuiya ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki inategemea kumpata Sudani ya Kusini kama mwanachama mpya mwaka huu. Iweje sisi Watanzania tufurahie kuuvunja Muungano wetu? Mimi binafsi, ninadhani maeneo yote yenye utata kwenye Muungano wetu yanazungumzika, hivyo yawe wazi na tuyazungumze ili tupate muufaka kwa munufaa ya Nchi yetu Tanzania.

  Muungano ukivunjika, sehemu zote za Tanganyika, Unguja na Pembe haizitakaa ziwe huru na salama. Tanganyika itajikita zaidi Magharibi, Pemba na Unguja wataegemea Middle East. Kihistoria, Magharibi (Ukristo) na Middle East(Uislamu), piga ua na garagaza sehemu hizi ni MAHISIMU.

  Wito wangu: CHONDE CHONDE, tusidhubutu kuukaribisha uhasimu huo katika nchi yetu, maana utatumaliza.
   
 15. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Me nafikiri kero zitatuliwe bt hajifika kipindi cha kusema hauna faida
   
 16. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  HaĆ­ingii akilini kuwa huku tunajadili muungano wa nchi 5 za EA na huku tunajadili kuvunja muungano wa tanganyika na zanzibar
   
 17. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hao wanaosema hatutaki muungano ni wanafiki wakubwa ! Kama hamuutaki stand up and be counted kuliko kulia lia humu jf! Watangazieni walimwengu huko duniani kwamba muungano sasa basi! Kama hamtafanya hivyo mtaendelea kuwa wanafiki siku zote na kelele za chura hazitomzuia ng'ombe kunywa maji!
   
 18. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa kama hawataki muungano si wa uvunje wanapiga kelele tu kila siku za nini?? Mleta mada ni mnafiki kama mngekuwa hamna shida na muungano si mngepitisha tu sheria kwenye baraza lenu la wawakilishi, kila siku mnakuja na porojo tu!!!!:bored:
   
 19. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Wanasiasa ndio wachochezi sehemu zote
   
 20. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kama wanataka kuvunja muungano acha wavunje, nimezaliwa kwenye nchi inaitwa Tanzania hivyo basi mimi kwa umri wangu wa ujana najua Taifa langu ni TANZANIA, wakiondoka si tutabaki na Taifa letu Tanzania.Ila kama muasisi wa Taifa hili alivyopata kusema wakisha jitenga wataanza kusulubiwa na kanuni ya UBAGUZI, navojua mimi kwa uwelewa wangu japo mdogo nina hakika Ukiwachukua watanzania bara kumi [10] ukawauliza swala la kuvunja muungano na hakika watanzania bara nane [8] watakwambia awataki muungano uvunjwe japo awaoni faida yake wanasukumwa zaidi na jadi ya kitanzania ya kuthamini mgeni yoyote yule na hata kufikia hatua ya kuwa mwanafamilia. Swali hilo hilo ukilipeleka Tanzania visiwani na hakika kati ya watu kumi [10] watu nane [8] watakwambia wanataka uvunjwe.

  Dhambi ile mwalimu aliyosema tuwaache waijalibu TUSILAZIMISHE MUUNGANO kila jambo lina sababu, Muungano wetu na wao uwenda ulikua na sababu na sasa kwa kua wao ni wana na waja wasiotaka mahusiano hayo tuwaache yetu macho kuwaona wao na mbio zao zitaishia wapi.

  Na hakika wao wanaona kama wabara wanawanyonya sana wao, kwa lipi? na zile tuuma za mahusiano na ndugu zao uko ughaibuni zama hizi za technology jamani wabara msiogope zimekwisha angalia falme za kiarabu zilivyo matatani ni mjomba gani huyo atakuja kuwapa hiyo support wakati kwake kunaungua moto pindi wakianza kuchomana moto kumtafuta yupi mzanzibar pemba na yupi mzanzibar unguja.

  Tukioana wametafunana vya kutosha baada ya kuwa wameshajitoa kwenye muungano basi mfano mzuri tunao NJUANI. Moja ya vitu vizuri Mh JK alipata kufanya siku za awali za utawala wake kabla ya haya yanayoendlea sasa. Tutawaomba jamaa wa AU pls awa ni jamaa zetu tunawajua tunawaomba kuwaepusha na suluhu hii. Nafikilia mpaka hapo hakuna Taifa lolote Dunia litakata pindi Wantanzania watakapoamua kuomba KUINTERVINE, hata kama ni miaka kumi mpaka ishirini [10-20] hapo ndipo Wazanzibar wa kweli kwa moyo wa watataka muungano wa dhati na hiari kitu ambacho Karume [Brave Man] alikiona mapema ndio maana alimwomba Mwalimu [Intellectual] kuungana tukapata taifa ambalo mimi niyezaliwa chini ya mika sabini [1970s] najivunia.

  Give them chance to try, try and error nayo ni kanuni, let them. Tusiwalazimishe jamani dunia inabadilika leo hii ya Tunisa, Libya nani aliyategemea.

  Watanzania sie watuache na umoja wetu pwani na bara kama kawa,Ila kama wakijitoa rasmi kuvunja muungano mchakato mzima uanze wale wanzazibar wote walioko bara waamue kuchagua moja kati ya mawili kuludi ambako sasa wao wataita nchini kwao yani Zanzibar ama wabaki Tanzania na kujiandikisha rasmi kama watanzania wasio wazanzibar.

  Kwa wale wasukuma, waha, wangoni, wanyamwezi, wanyakyusa na wanyasa walioko zanzibar wakipenda ruksa waludi nyumbani Tanzania tuna ardhi kubwa sana, kuna watanzania waludi wakapewa ardhi huko Tanga leo hii wanaishi na ni raia wa Tanzania japo wamezaliwa nchi somalia, Kuna wakimbizi ngara huko wamepewa ardhi na uraia halali wa Kitanzania sembuse na ndugu wa damu.

  Give them a Chance, what goes around comes around, ifike time those who think big waanze kuwa na PLAN zenye VISION ya muda Mrefu kwa kua katika hili Watanzania Bara atutakua Guilt Concious, of what happen na hatutasutwa na dhamila na nafsi zetu na kutokea hapo ndio tutapata udgu wa kweli wa muungano wa dhati na wazi.

  KALUME alitangulia kuona japo wao awaamini, waacheni wachezee kiberiti cha gas kwenye tanki la gesi, wanaamini kuwa wao ni wamoja [Waswahili wa Wapemba ujuana kwa vilemba].
   
Loading...