Maishamapya
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,279
- 375
UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.
Dunia ya sasa ni juu ya umoja na ushirikiano. Tazama nchi za jumuiya ya Ulaya, wanazidi kuwa wamoja. Mifano ipo wazi, ni umoja wao katika kutafuta mafuta ya Afghan, Iraq, Kuwait, na sasa Libya kwa maendeleo ya watu wao na nchi zao. Zamu ijayo itakuwa ni Mafuta ya Unguja, Uranium ya Tanganyika, Mafuta ya Sudan ya Kusini, Mafuta ya Uganda, Angola n.k
Jumuiya ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki inategemea kumpata Sudani ya Kusini kama mwanachama mpya mwaka huu. Iweje sisi Watanzania tufurahie kuuvunja Muungano wetu? Mimi binafsi, ninadhani maeneo yote yenye utata kwenye Muungano wetu yanazungumzika, hivyo yawe wazi na tuyazungumze ili tupate muufaka kwa munufaa ya Nchi yetu Tanzania.
Muungano ukivunjika, sehemu zote za Tanganyika, Unguja na Pembe haizitakaa ziwe huru na salama. Tanganyika itajikita zaidi Magharibi, Pemba na Unguja wataegemea Middle East. Kihistoria, Magharibi (Ukristo) na Middle East(Uislamu), piga ua na garagaza sehemu hizi ni MAHISIMU.
Wito wangu: CHONDE CHONDE, tusidhubutu kuukaribisha uhasimu huo katika nchi yetu, maana utatumaliza.
Umoja ni nguvu ikiwa wote mnajenga kitu kimoja. Lakini kama mmoja anajenga kitu chake kwa kutumia fito za wote inakuwaje? Zenj hawatumii tu fito za wote ila wanachomoa fito zilizojengwa kwenye nyumba. Kwa mfano walidai wapeperushe bendera yao - wakapata; wakataka wimbo wao - wakapata. Walipobadili katiba ili wajitenge zaidi wakasema Znz ni nchi. Hapa wakavunja katiba ya muungano kwa waziwazi ila mkuu wa nchi amawanyamazia. Hapo kuna muungano?