Zanzibar Kumekucha

Zanzibar Kumekucha

Siku huu muungano ukivunjika nitafanya bonge la party. Sijawahi na wala sitegemei kuona faida za huu muungano miaka 10000 ijayo kwa upande wa tanganyika, zaidi ya sifa za kijinga, what a news, kama wanataka msaidizi wa kuvunja wanipm. Nitajitolea kwa taaluma yangu ya sheria kudraft article ya kuvunja muungano
 
UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.

Dunia ya sasa ni juu ya umoja na ushirikiano. Tazama nchi za jumuiya ya Ulaya, wanazidi kuwa wamoja. Mifano ipo wazi, ni umoja wao katika kutafuta mafuta ya Afghan, Iraq, Kuwait, na sasa Libya kwa maendeleo ya watu wao na nchi zao. Zamu ijayo itakuwa ni Mafuta ya Unguja, Uranium ya Tanganyika, Mafuta ya Sudan ya Kusini, Mafuta ya Uganda, Angola n.k

Jumuiya ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki inategemea kumpata Sudani ya Kusini kama mwanachama mpya mwaka huu. Iweje sisi Watanzania tufurahie kuuvunja Muungano wetu? Mimi binafsi, ninadhani maeneo yote yenye utata kwenye Muungano wetu yanazungumzika, hivyo yawe wazi na tuyazungumze ili tupate muufaka kwa munufaa ya Nchi yetu Tanzania.

Muungano ukivunjika, sehemu zote za Tanganyika, Unguja na Pembe haizitakaa ziwe huru na salama. Tanganyika itajikita zaidi Magharibi, Pemba na Unguja wataegemea Middle East. Kihistoria, Magharibi (Ukristo) na Middle East(Uislamu), piga ua na garagaza sehemu hizi ni MAHISIMU.

Wito wangu: CHONDE CHONDE, tusidhubutu kuukaribisha uhasimu huo katika nchi yetu, maana utatumaliza.
Sio hilo tu, lakini siku Muungano ukivunjika, Pemba nayo itajitenga na Unguja huku kukiwa na uwezekano wa Tanzania kugawanyika vipande vipande katika maeneo ya kanda.

Tatizo la Muungano kwanza ni vipengele vyake vyenye utatanishi na mgawanyo usio sawa wa mapato ya nchi. Hapa nakusudia kutokuwepo mipaka ya wazi inayotenganisha mamlaka ya Serikali ya TZ Bara ambapo kuna serikali mbili ndani ya moja, ile inayoshughulikia mambo ya TZ Bara na ile inayoshughulikia mambo ya Muungano. hili linatuudhi hata hapa bara.

Tatizo la pili na hili ndio kubwa zaidi, ni ugawanyaji mbaya wa utajiri wa nchi. Kama utaangalia, sehemu tajiri na mhimili wa uchumi wa nchi, ndio masikini kabisa. Suluhisho moja katika mengi, ni kuwa vipengele vyenye utatanishi vinazungumzika na kujaribu iwezekanavyo kuendeleza sehemu zenye utajiri na sio kuzifanya kama shamba la bibi.
 
mUUNGANO WETU SIO KWAMBA HAUNA FAIDA. wALA SI KWAMBA NI FEKI LA ASHA! Mkataba wa muungano ni halali ila kwa kuwa hauitajiki ni muda muafaka kuondokana nao. Bora tubaki na Tanganyika yetu ili tuondokane na dhana mbaya ya ukandamizaji. Nakuhakikishia kuwa hatuhitaji kura ya maoni kuwaacha watu wa visiwani wakjitawale. Wakae wakuba;iane wenyewe na kisha walete ombi bara la kujiondoa. Tanganyika ikiwa huru nod tuone Zanzibar ikijiendesha kwa uhuru. NAsikitika kusikia kuwa muunga o ulikuwa kwa ajili ya kulinda amani ya Tanganyika, swali ni je, vita ipi ingepigwa kutokea zanzibar na je nchi izo tuumiwa za kiarabu na nk zkiamua kuingia vitani au kuhatarisha amani hata bila kuptita zanzibar bara itaweza kudhiti. Fikiria hata mabomu yetu tayari ni chakavu. Iache zenji iwe huru.
 
wazanzibar kazi iko kwenu. Hamfikirii hata sheria zimevunjwe ili Shein arudi zanzibar kuutwaa urais! sheria zi wazi kuwa mtu ambaye kwa zaidi ya muda flani hatopiga kura,wala kuchaguliwa kwa ngazi za kisiasa z'bar, Shein amekaa magogoni miaka 5, hakuwahi hata kujiadikisha katika daftari la wapiga kura kwa zanziar bali jina lake liko Oysterbay dar es salaam na akampigia kura Jk,slaa au wengine kwa kuwa kura ni siri alafu akapanda boti au ndege kuwahi kusikiliza matokeo ya kura z'bar. Nakumbuka mtangazaji alimuuliza mh.mbona umepiga kura bara, hujajipaigia kura utashinda kweli? shein akamwambia 'nitashinda hata wewe utashangaa" Kwa kweli mi sioni kama z'bar iko huru. Ila tusitumie jazba,dola na mbinu chafu kuulinda muungano ambao raia wa tanganyika hatujui umuhimu wa muungano huu wenye nchi moja marais wawili na makamu watatu. na kwa kuwa makamu naye ni rais japo makamu, basi Tamnzania ina marais watawala watano! This is made in Tanzania and Tz alone.
 
Vunja muungano, nchi kubwa namna ile haiwezi kuwa na maendeleo nchi lazima ivunjwe vipandevipande.
 
****** ataki muungao uongelewe kwenye katiba mpya, hiyo ni dhairi muungano unamatatizo sana. Inakuwaje znz wanajibadilishia tu katiba wanavyotaka wao. kuwe na serikali moja na rais mmoja au muungano uvunjike tuwe na serikali mbili kila mtu kivyake
 
Hivi waBara wanahitaji kuungana na ZNZ? Kwana idadi kubwa ya wachochezi wa udini huku bara wana asili ya Zanzibar. Idadi kubwa ya wapinzani walioolewa na ccm wana asili ya Zanzibar. Uchumi na serikali ya Zanzibar zinapora rasilimali za bara. Ardhi na biashara za bara wamehodhi wazanzibar.

Wanajitenga lini tuwaandalie meli na mashua za kutosha? Hamadi Rashidi na genge lake la wabunge wachumia tumbo toka Zanzibar watakula wapi?
 
****** ataki muungao uongelewe kwenye katiba mpya, hiyo ni dhairi muungano unamatatizo sana. Inakuwaje znz wanajibadilishia tu katiba wanavyotaka wao. kuwe na serikali moja na rais mmoja au muungano uvunjike tuwe na serikali mbili kila mtu kivyake

Muungano ni wa kihuni na muundo wa serikali yetu ni wa kihuni.
 
Sio hilo tu, lakini siku Muungano ukivunjika, Pemba nayo itajitenga na Unguja huku kukiwa na uwezekano wa Tanzania kugawanyika vipande vipande katika maeneo ya kanda.

Tatizo la Muungano kwanza ni vipengele vyake vyenye utatanishi na mgawanyo usio sawa wa mapato ya nchi. Hapa nakusudia kutokuwepo mipaka ya wazi inayotenganisha mamlaka ya Serikali ya TZ Bara ambapo kuna serikali mbili ndani ya moja, ile inayoshughulikia mambo ya TZ Bara na ile inayoshughulikia mambo ya Muungano. hili linatuudhi hata hapa bara.

Tatizo la pili na hili ndio kubwa zaidi, ni ugawanyaji mbaya wa utajiri wa nchi. Kama utaangalia, sehemu tajiri na mhimili wa uchumi wa nchi, ndio masikini kabisa. Suluhisho moja katika mengi, ni kuwa vipengele vyenye utatanishi vinazungumzika na kujaribu iwezekanavyo kuendeleza sehemu zenye utajiri na sio kuzifanya kama shamba la bibi.

Mkuu.
Je hapo zamani ilitokea Pemba na Unguja kutaka kujitenga ?
Kwa nini ukivunjika watake kujitenga?

Tanganyika inaweza kupata msukosuko wa kidini kama hatutakua makini.
Na hapa sitaki kutoa lawama kwa upande wa dini fulani.Sote tuna jukumu la kuacha udini, kutochochea udini au kuendeleza udini.

Mkuu...Jina Tanzania halikuwepo hata pale ulipoundwa muungano...ok..lilikuja hilo Tanzania...sasa hili Tanzania bara ni nani alilitengeneza?
Tanzania lilitengenezwa na mhindi wa Tanga...Je hili Tanzania bara ni nani alilitengeneza?
Hivi ni kwa nini hatulitaki jina Tanganyika? Zanzibar kwa nini jina hili lipo?

Hata kama lipo jina Tanzania, sioni ni kwa nini tuone tabu kutumia Tanganyika kumaanisha sehemu iliyoungana na Zanzibar.

Hivi hatuwezi kuwa na dhana ya Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar... Tanganyika ikatumika kama sehemu moja ya Tanzania na Zanzibar kama sehemu nyengine ya Tanzania.

Katika huu utatanishi tunaouzungumzia basi kuacha kutumia Tanganyika na kuita Tanzania bara ni utatanishi mkubwa sana.

Lakini CDM ikichukua utawala, Tanganyika itagawiwa majimbo... how does it sound to you?
 
Muungano ni wa kihuni na muundo wa serikali yetu ni wa kihuni.

Unaweza kusema pia kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaendeshwa kihuni na kwa ubabe.
Kwa kifipi ni unafiki mtupu.

Hakuna mipaka ya kimamlaka kwa serikali ya Muungano inapojigeuza pia kuwa serikali ya Tanganyika.
wakati inakuwa rahisi kuwambia wazenj wanakiuka katiba wanapofanya mabadiliko ya katiba yao, la ajabu ni kuwa Tanganyika haina katiba yake.

Mimi nashindwa kuelewa vipi mamlaka tatu kisheria zinatumia Katiba mbili tu!
This is more than mkorogo wa kichina!

Na sisi tunapiga kelele tuwe na serikali moja badala ya kudai serikali ya Tanganyika pia iwepo!!!

Je na sisi pia ni wahuni?
 
Kama wazanzibar watawaacha waTanganyika basi watanganyika watabaki wamedumaa, lakini wazanzibar hawatabaki salama!!!!!!!!!
Nukuu isiyo rasmi
 
Mi Mtanganyika, naunga mkono Muungano uvunjike, Sijawahi, na wala sina mpango wa kufika Zanzibar... Break the Union Please!!
 
Nikifikiria vyanzo vya mapato Zenj kichwa kinauma. Mtauana sana. Tokeni sasa. Kura kama laki 2 za CCM zitapungua. Better

Mkuu.
Unaelewa kuwa kuna nchi ambazo ni visiwa kama Zanzibar?
Sychelles. Mauritius, Cape Verde..nchi hizi zipo Afrika.....je unaelewa vyanzo vyao vya mapato?

Lakini sisi Tanganyika aka Tanzania bara wenye vyanzo vya mapato....hayo mapato yako wapi? mapato yanayokusanywa yanamsaidia vipi mwananchi wa kawaida?

Nilipopitia historia nilijifunza kuwa Zanzibar walikuwa na uchumi bora kuliko wa Tanganyika kabla ya Muungano.

Wao uchumi wanao, na sisi uchumi tunao lakini "tumeukalia" kwa maneno ya Nyerere.

Tatizo ni viongozi tu.
 
UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.

Dunia ya sasa ni juu ya umoja na ushirikiano. Tazama nchi za jumuiya ya Ulaya, wanazidi kuwa wamoja. Mifano ipo wazi, ni umoja wao katika kutafuta mafuta ya Afghan, Iraq, Kuwait, na sasa Libya kwa maendeleo ya watu wao na nchi zao. Zamu ijayo itakuwa ni Mafuta ya Unguja, Uranium ya Tanganyika, Mafuta ya Sudan ya Kusini, Mafuta ya Uganda, Angola n.k

Jumuiya ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki inategemea kumpata Sudani ya Kusini kama mwanachama mpya mwaka huu. Iweje sisi Watanzania tufurahie kuuvunja Muungano wetu? Mimi binafsi, ninadhani maeneo yote yenye utata kwenye Muungano wetu yanazungumzika, hivyo yawe wazi na tuyazungumze ili tupate muufaka kwa munufaa ya Nchi yetu Tanzania.

Muungano ukivunjika, sehemu zote za Tanganyika, Unguja na Pembe haizitakaa ziwe huru na salama. Tanganyika itajikita zaidi Magharibi, Pemba na Unguja wataegemea Middle East. Kihistoria, Magharibi (Ukristo) na Middle East(Uislamu), piga ua na garagaza sehemu hizi ni MAHISIMU.

Wito wangu: CHONDE CHONDE, tusidhubutu kuukaribisha uhasimu huo katika nchi yetu, maana utatumaliza.
Tanganyika, kwanini iegemee magharibi?
 
Haíingii akilini kuwa huku tunajadili muungano wa nchi 5 za EA na huku tunajadili kuvunja muungano wa tanganyika na zanzibar

Mkuu.
Umesahau EAC pia tulipoona inakwenda kiujanja ujanja na haina faida tuliivunja.? Tulipoamua kuwa makini na kila member afaidi na anufaike tumeifufua tena...lakini pitia threads hapa Jf uone tunavyowaogopa Kenya.
 
Toka tokaa toka si mke wangu, kwanza ndoa ilikuwa ya mkeka, miaka yote huzai, kila kukicha kuchonga tu bla bla mwananke gani usietosheka jamani!
nikiona unapanda basi mie walahi nitashuka!
Kweli kima hafugiki.
 
Nikifikiria vyanzo vya mapato Zenj kichwa kinauma. Mtauana sana. Tokeni sasa. Kura kama laki 2 za CCM zitapungua. Better

Ukidhani unamkomoa kumbe unamfagilia. Zenj tukijitenga na Mwungano:-

1. Tunatangaza Islamic State
2. Tunajiunga na IOC
3. Biashara za mabaa zitafungwa.
4. Heri bwana ufe turudi kama zamani. Zanzibar ilikuwa swari. Husikii wizi wala vibaka. Mwizi akiiba tunakata mkono. Akifanya ufisadi tunakata kichwa.
 
Unaweza kusema pia kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaendeshwa kihuni na kwa ubabe.
Kwa kifipi ni unafiki mtupu.

Hakuna mipaka ya kimamlaka kwa serikali ya Muungano inapojigeuza pia kuwa serikali ya Tanganyika.
wakati inakuwa rahisi kuwambia wazenj wanakiuka katiba wanapofanya mabadiliko ya katiba yao, la ajabu ni kuwa Tanganyika haina katiba yake.

Mimi nashindwa kuelewa vipi mamlaka tatu kisheria zinatumia Katiba mbili tu!
This is more than mkorogo wa kichina!

Na sisi tunapiga kelele tuwe na serikali moja badala ya kudai serikali ya Tanganyika pia iwepo!!!

Je na sisi pia ni wahuni?

Hakuna haja , nafikiri hatua mhimu kwanza nikuuvunja muungano watu wafikirie kwanza. Kuendelea kuurekebisha huu uliopo kila siku kutakua na madai mapya yasioyoisha. Muungano wa kihuni unaendeshwa kihuni huni.
 
Kama wazanzibar watawaacha waTanganyika basi watanganyika watabaki wamedumaa, lakini wazanzibar hawatabaki salama!!!!!!!!!
Nukuu isiyo rasmi

Mkituletea unoko tunakwenda kuwasemea kwa kaka Obama tu. Mtakiona cha moto.
 
Back
Top Bottom