Zambia Elections: Opposition (SATA) wins Presidential race!!!

hongera sana Sata kwa ushindi huo..zambia wame thubutu na wameweza sasa wasonge mbele..
 
Hivyo Zambia hakuna Usalama wa Taifa vile! Si wangemtangaza Rais wao magumashi kama nchi fulani ya "amani"!

Amani wapi?
Sema watanzania tu tumekua wavumilivu kupitiliza,
Hakuna cha amani yoyote!!
 
Kwa mujibu wa bbc kiongozi wa upinzani michael satta wa chama cha patriotic front ametangazwa mshindi kwa kumshinda Rupia Banda wa chama cha MMD. Michael Satta maarufu kama "king cobra" alijaribu kutafuta uraisi wa zambia kwa mara 4. Anafahamika sana zambia kwa sera zake za kupinga wawekezaji wa nje hasa wachina kuhodhi uchumi wa zambia. Ushindi wa Satta imeelezwa unatokana na hasira ya wazambia kwa chama tawala kufumbia macho ufisadi na uchumi mbovu. MMD wamevuna walichopanda. Ni fundisho zuri kwa magamba wa Tanzania.
 
Nimeshangazwa sana na vyombo vyetu vya habari,ushindi wa mgombea wa chama cha upinzani nchini Zambia umekuwa kama mshtuko kwa chama chetu tawala(CCM).Inavyoonekana kuna aina fulani ya mkakati ya kutotangazwa kwa matokeo hayo kwenye vyombo vyetu vya habari ili watu wasipate kuujua ukweli,ila kwa dunia yetu ya leo,vyanzo vya habari ni vingi sana.Siku hizi ukizuia hiki kwa hila,wengine wanafungua mlango kwingine kwa manufaa zaidi.Kweli,ukimuamsha aliyelala,utalala wewe.Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania.
 
Hii ni motisha kwetu na salamu kwa ccm. Tukazane tupate katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Yes Zambia upinzani wamechukua nchi, Jamaa wamezuga zuga sana kutangaza matokeo lkn ikawabidi. Ni kielelezo kwamba inawezekana kabisa hata Tanzania. Big up Zambians
 
Mbona MMD ni second generation, mwenzie na CCM kitambo hayupo katika ramani kama Zanu pf iliondoka na KK.
Manake afrika hata upinzani unang'ang'ania madaraka kama ilivyokuwa kenya hii ndio changamoto mpya hata bongo watu wanataka delivery na hakuna mwenye hati miliki
 
Msimu wa mabadiliko kwa Afrika,sasa ndugu zangu wa China waliojimilikisha karibu kila kitu na unyanyasaji wao wa watu ambao ulikithiri sijui utakuwaje,ni sawa na kumwaga chumvi kwenye jeraha bichi.Watajifunza kupitia Zambia.Tanzani ni 2015.Bila Mungu hatuwezi chochote,ila bila CCM tunaweza na zaidi ya kuwa washindi.
 
Vyama vya kiafrika wakati mwingine vinachosha kabisa. Huwezi kuamini mpaka dakika hii kwenye website ya PF hakuna breaking news juu ya kushinda kwa mgombea wao!

Lakini mkuu angalau zambia is now a 'real' democratic state. sidhani kama tz tume ya uchaguzi ingeweza kumtangaza. Hata kama ingekuwa wazi ameshinda wa upinzani na yule aliyemadarakani amekubali kushindwa NEC yetu inaweza kugoma kutangaza pia.
 
Nimeshangazwa sana na vyombo vyetu vya habari,ushindi wa mgombea wa chama cha upinzani nchini Zambia umekuwa kama mshtuko kwa chama chetu tawala(CCM).Inavyoonekana kuna aina fulani ya mkakati ya kutotangazwa kwa matokeo hayo kwenye vyombo vyetu vya habari ili watu wasipate kuujua ukweli,ila kwa dunia yetu ya leo,vyanzo vya habari ni vingi sana.Siku hizi ukizuia hiki kwa hila,wengine wanafungua mlango kwingine kwa manufaa zaidi.Kweli,ukimuamsha aliyelala,utalala wewe.Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania.

nimekatiza tunduma jana na tetesi zilizotapakaa ni kuwa rais huyu aliyeshinda moja ya ahadi zake ni kuchukua eneo la tunduma, kwani anadai mpaka ulitakiwa kuwa Mpemba km kama nane toka tunduma
 
H.E Sata ametamka wazi hawezi kuamini wachina wanaweza kuleta maendeleo Zambia
Wachina walikuwa wamejikita kila eneo nchini humo wakiwanyonya Wazambia kuiba Copper yao kwa bei ya kutupwa
habari zilizotufikia punde wachina wanahama kuelekea nchi za jirani,Angola,cONGO,Botwana
mwenye uchungu na nchi amekamata madaraka kazi kwao!
 
Dear members of the JF,
Opposition leader Michael Sata has won Zambia's presidential election after two days of vote counting following a tight race with incumbent Rupiah Banda.

Mr Sata was declared winner by Chief Justice Ernest Sakala after polling 43% of the vote with just seven constituencies left to be counted.
The election had been marred by riots in Zambia's northern mining region.
The anger had been prompted by a ban on the media announcing results not verified by the electoral commission.
The electoral commission said it had taken the step after its website was hacked to falsely record a landslide for 74-year-old Mr Sata.
Mr Banda's Movement for Multiparty Democracy (MMD) has ruled Zambia for 20 years and this was the fourth time Patriotic Front (PF) leader Mr Sata had run for the presidency.

He lost the last election, in 2008, by just 35,000 votes which sparked rioting by some opposition supporters in the party's urban strongholds

It is our turn tanzanians. What is happenning in same economically is the same as in our country why cant we change these regime as zambians did?

What is your opinion on this?

I wish to submit.
 
Upinzani kwa mara ya pili unashinda Zambia. Hili ni tukio zuri sana kwa sababu naamini change in government kunapunguza politicalisation katika Govt/Civil jobs. Kama Watanzania watajifunza hili, itakuwa kitu muhimu sana. Kazi kama kwenye Wizara, polisi, jeshi, nk zitafanyika kwa efficiency zaidi maana watakuwa hawana political support/affiliations. Badala yake, watu wenye uwezo wa kazi watajitokeza na kufanya kazi, na sio ndugu wa rais, nk watakao pata hizo kazi. Kwangu mimi, hii ndio sababu kubwa ya kuchagua upinzani katika nchi. Hii ni step kubwa sana katika kuleta maendeleo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom