Zamani tulipanga foleni kupata huduma hizi

Zamani tulipanga foleni kupata huduma hizi

ila foleni ya kununa tiket ya sinema ni foleni bora kabisa, no stress bali unakuwa exited
 
Wakuu kwema…

Tuwape elimu ndogo vijana wa sasa kuhusu namna baadhi ya huduma zamani ilibidi upange foleni kwa kufika ofisi husika ili uhudumiwe.

1. Luku
Ili upate huduma ya kununua umeme (luku) ilikuwa lazma ufike kwenye ofisi za Tanesco. Baadae wakaongeza huduma kwenye baadhi ya vituo vya kuuzia mafuta (sheli).

Yaani unaenda kununua umeme jioni, unakuta foleni ndefu na hapo ombea network isisumbue mtalala giza kwenu.

2. Malipo ya DStv lazma uende ofisini kwao.

Miaka hiyo nakumbuka mzee akienda kulipa DStv kule Kinondoni Makaburini zilipokuwa ofisi pekee za Dstv kwa Tanzania nzima. Ikishalipiwa kule anapiga simu kuuliza vipi chaneli zimefunguka, kabla hajatoka ofisi zao.

3. Simu za TTCL za mezani
Malipo lazma uende ofisini kwao.
Nilichokuwa napenda kuhusu TTCL ni kuwa walikuwa wanatoa vitabu vyenye namba za simu zote nchi nzima. Ulikuwa ukiwa na shida na mtu unatafuta jina lake kwenye kitabu cha TTCL unakuta namba zake unampigia.

4. Malipo ya Maji NUA baadae
Ukiletewa ankara ya maji basi utalazimika kufunga safari kwenda ofisi zao zilipo ili uweze kufanya malipo.

Huduma gani imesahaulika? Ongeza
Unga
Mchele
Sukari
Nyama
Magazeti
Video za kuazima
Mafuta ya taa
Mafuta ya kula
Dizeli na petrol
Kushona uniforms
Kuingia cinema etc.

Tuliokulia 70s and 80s tunaona how ungrateful the gen zege is
 
Sio CCM ni teknolojia imekuwa..!!
Ingekuwa Tanzania peke yake sawa tungeipongeza veggies..!!

Ni wazungu wapewe maua yao, unafki haukupendezi 😹
CCM ndo iliruhusu hao wazungu kuleta teknolojia... wangeweza kuzuia
 
Kimbo mafuta ya kala.
Mie Nimetumia radio call zilikuwepo parokiani kanisa Catholic
Buluga
Mawingu nguo
Kilimbulini
Haaaaaaaah Hatari sana
 
images - 2025-09-03T204915.337.jpeg
 

Attachments

  • images - 2025-09-03T204849.386.jpeg
    images - 2025-09-03T204849.386.jpeg
    42.8 KB · Views: 11
Home tumeanza kutumia umeme kitambo ila hizo mambo za kununu unit toka tanesco hayakutufikia.

Sisi tulikua na mita za kulipa mwisho wa mwezi zile, mpaka hii system mpya ya kununua luku kwa simu/mawakala iliposambaa ndio wakaja kubadilisha.

Ilikua burudani sana zile mita, sometimes mnafanya uhuni mnatumia umeme bure.
 
Back
Top Bottom