KERO Foleni kubwa katika kupata huduma katika Mabenki

KERO Foleni kubwa katika kupata huduma katika Mabenki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Technologiest

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2017
Posts
3,728
Reaction score
4,058
Habari wakuu.

Bila kuwapotezea muda, kwa kila ambaye amewahi kutumia huduma za kibenki hapa Nchini kwetu Tanzania kuna tabia ya uchelewevu wa huduma na upotevu wa muda sana hasa ukifika Matawini na ATM.

Leo nataka tuangazie hili la huduma za kwenye matawi hasa zile za kufuata ndani ambazo kwa namna moja ama nyingine zinakulazimu upate kutoka branch moja kwa moja ndani ya tawi la benki na si kwa wakala ama kupitia Wakala.

Benki nyingi (Matawi) unaenda kutafuta huduma unajikuta unakaa benki kama nawe umeenda kufanya kazi pale, huduma inakulazimu kuchukua hata saa moja ama mawili wakati ukisubiri huduma, binafsi naona hii haiko sawa.
Wakati huo unaona Madirisha mengine ya huduma (teller) yako temporary closed na hiyo temporarily unakuta ni kuanzia asubuhi hadi jioni na kesho ukija hali hiyo hiyo.

1. Hawa watu huwa wanawaza nini juu ya majukumu mengine ya watu?
Hivi huduma ya kibenki ni ya kungoja dakika 30,saa 1 ama mawili kwa dunia ya leo kweli?
2. Je, wanatafakari juu ya masuala ya Kiusalama?

Kuna mtu ametoka amejilinda njia nzima huko barabarani afikishe mzigo benki bila kukwapuliwa huko barabarani unafika unamuweka saa zima kwa foleni, what if ikatokea akiwa hapo tawini wazee wa kazi wakaingia wakalaza raia wote chini na wakatoka na pesa za wateja ambazo walikuwa bado hawajamkabidhi teller.

Benki itawajibika kwa uzembe maana huyu mteja angefika na kuhudumiwa dakika chache baada ya kufika huenda maafa hayo yakitokea yasingemkuta?
Hebu wahusika wajirekebishe.
 
Back
Top Bottom