Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Zakia alipongeza Uhuru kufanikisha ushindi wa CCM
Thursday, 09 December 2010 20:14 newsroom
NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa kuteuliwa, Zakia Meghji amepongeza jitihada za magazeti ya Uhuru na Mzalendo katika kufanikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu uliopita.
Zakia alisema hayo alipozungumza na gazeti hili, kuhusu maadhimisho ya miaka 49 ya gazeti la uhuru, ambapo alisistiza magazeti hayo yamejijengea heshima kwa kuandika habari za kuaminika.
Alisema gazeti la Uhuru likilinganishwa na kipindi cha Uhuru lina mabadiliko makubwa, limeboreshwa na linaandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kutosha tofauti na magazeti mengine.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alisema tangu Uhuru gazeti limefanikisha uchaguzi mbalimbali kwa kuandika habari za kampeni na kuelimisha umma pale inapotokea CCM imeandikwa vibaya na vyombo vingine vya habari.
ìMiaka 49 si jambo dogo... magazeti ya Uhuru yameimarishwa zaidi, yamekuwa na msaada kwa Chama na kwa wananchi kwa kuwapasha habari mbalimbali mijini na vijijini,î alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu ambao uligubikwa na kampeni za kuchafuana baina ya vyama vya siasa, magazeti ya Uhuru na Mzalendo yalifanya kazi kubwa ya kuelimisha wananchi na kuhamasisha waichague CCM iendelee kuongoza nchi.