Elections 2010 Zakia alipongeza Uhuru kufanikisha ushindi wa CCM....................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Zakia alipongeza Uhuru kufanikisha ushindi wa CCM

Thursday, 09 December 2010 20:14 newsroom
NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa kuteuliwa, Zakia Meghji amepongeza jitihada za magazeti ya Uhuru na Mzalendo katika kufanikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu uliopita.
zakia%20copy.jpg

Zakia alisema hayo alipozungumza na gazeti hili, kuhusu maadhimisho ya miaka 49 ya gazeti la uhuru, ambapo alisistiza magazeti hayo yamejijengea heshima kwa kuandika habari za kuaminika.
Alisema gazeti la Uhuru likilinganishwa na kipindi cha Uhuru lina mabadiliko makubwa, limeboreshwa na linaandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kutosha tofauti na magazeti mengine.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alisema tangu Uhuru gazeti limefanikisha uchaguzi mbalimbali kwa kuandika habari za kampeni na kuelimisha umma pale inapotokea CCM imeandikwa vibaya na vyombo vingine vya habari.
ìMiaka 49 si jambo dogo... magazeti ya Uhuru yameimarishwa zaidi, yamekuwa na msaada kwa Chama na kwa wananchi kwa kuwapasha habari mbalimbali mijini na vijijini,î alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu ambao uligubikwa na kampeni za kuchafuana baina ya vyama vya siasa, magazeti ya Uhuru na Mzalendo yalifanya kazi kubwa ya kuelimisha wananchi na kuhamasisha waichague CCM iendelee kuongoza nchi.
 
Kweli Mwanasiasa ni Mwana-Siasa tu......hivi kweli Uhuru iliandika ukweli wowote kwenye uchaguzi huu kama siyo kutumia muda wake mwingi kupotosha wananchi na ngebe za kiushabiki............Pia ushindi wa CCM wa mezani wa kuchakachua kura zetu kweli ni sahihi kuuhusisha na propoganda za Uhuru Publications........................................

Wako wapi HAbari Leo na Daily News katika kuzichakachua habari za uchaguzi?
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Zakia alipongeza Uhuru kufanikisha ushindi wa CCM

Thursday, 09 December 2010 20:14 newsroomKumbe ni gazeti maalum la kufanikisha ushindi kwa CCM na sio ku-foster uhuru wa Mtanzania???

Ahsante Zakia kwa kutsaidia kujua ukweli. Sasa sitahoji tena yanayoandikwa na UHURU, maana ni chombo muhimu kufanikisha ushindi CCM
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
24,954
19,273
Zakia alipongeza Uhuru kufanikisha ushindi wa CCM

Thursday, 09 December 2010 20:14 newsroomNA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa kuteuliwa, Zakia Meghji amepongeza jitihada za magazeti ya Uhuru na Mzalendo katika kufanikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu uliopita.
zakia%20copy.jpg

Zakia alisema hayo alipozungumza na gazeti hili, kuhusu maadhimisho ya miaka 49 ya gazeti la uhuru, ambapo alisistiza magazeti hayo yamejijengea heshima kwa kuandika habari za kuaminika.
Alisema gazeti la Uhuru likilinganishwa na kipindi cha Uhuru lina mabadiliko makubwa, limeboreshwa na linaandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kutosha tofauti na magazeti mengine.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alisema tangu Uhuru gazeti limefanikisha uchaguzi mbalimbali kwa kuandika habari za kampeni na kuelimisha umma pale inapotokea CCM imeandikwa vibaya na vyombo vingine vya habari.
ìMiaka 49 si jambo dogo... magazeti ya Uhuru yameimarishwa zaidi, yamekuwa na msaada kwa Chama na kwa wananchi kwa kuwapasha habari mbalimbali mijini na vijijini,î alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu ambao uligubikwa na kampeni za kuchafuana baina ya vyama vya siasa, magazeti ya Uhuru na Mzalendo yalifanya kazi kubwa ya kuelimisha wananchi na kuhamasisha waichague CCM iendelee kuongoza nchi.
Anazeeka vibaya............ MAMA NAONA UNALIPA FADHIRA KWA KUPEWA SHAVU
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
484
hapa dhana ya uzeee dawa naanza kuifuta kichwani sasa! huyo mama, sijui bibi karogwa?
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,162
10,292
QUOTE=mfarisayo;a.k.a Mzaa Chema cha Dr.( NONE PHD DR.)

Wewe mfarisayo nimeshakwambia sio PHD,bali ni PhD!
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,162
10,292
QUOTE=Rutashubanyuma; Zakia alisema hayo alipozungumza na gazeti hili, kuhusu maadhimisho ya miaka 49 ya gazeti la uhuru, ambapo alisistiza magazeti hayo yamejijengea heshima kwa kuandika habari za kuaminika.Duh! Hapa ni dhahiri huyu mama ana SANITY problems. Hayo makaratasi yanayoitwa magazeti,siku izi hata hayanunuliki. Hapa nilipo,makaratasi hayo hata ukipita jioni kwa wauzaji unayakuta yanauza sura. Mengine kama Mwananchi,Tanzania Daima,Raia Mwema,Mwanahalisi,Daily News (kutokana na kuwa na matangazo ya nafasi za ajira mbalimbali).
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,170
10,744
Confused! huyu mama juzi alichemka alivyowasifia gazeti la zamani la cheche, leo kajisafisha kwa style hii, you need to be crazy to practise hardcore politician!
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
8,204
3,532
wazee wa vijijini huwa wakianza kuzeeka wanakuwa si wazungumzaji sana, hivi wa mijini wana matatizo gani? hawajifunzi hata kwa mzee Kawawa?
 
ngoko

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
573
14
Zakia alipongeza Uhuru kufanikisha ushindi wa CCM

Thursday, 09 December 2010 20:14 newsroom
NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa kuteuliwa, Zakia Meghji amepongeza jitihada za magazeti ya Uhuru na Mzalendo katika kufanikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu uliopita.
zakia%20copy.jpg

Zakia alisema hayo alipozungumza na gazeti hili, kuhusu maadhimisho ya miaka 49 ya gazeti la uhuru, ambapo alisistiza magazeti hayo yamejijengea heshima kwa kuandika habari za kuaminika.
Alisema gazeti la Uhuru likilinganishwa na kipindi cha Uhuru lina mabadiliko makubwa, limeboreshwa na linaandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kutosha tofauti na magazeti mengine.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alisema tangu Uhuru gazeti limefanikisha uchaguzi mbalimbali kwa kuandika habari za kampeni na kuelimisha umma pale inapotokea CCM imeandikwa vibaya na vyombo vingine vya habari.
ìMiaka 49 si jambo dogo... magazeti ya Uhuru yameimarishwa zaidi, yamekuwa na msaada kwa Chama na kwa wananchi kwa kuwapasha habari mbalimbali mijini na vijijini,î alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu ambao uligubikwa na kampeni za kuchafuana baina ya vyama vya siasa, magazeti ya Uhuru na Mzalendo yalifanya kazi kubwa ya kuelimisha wananchi na kuhamasisha waichague CCM iendelee kuongoza nchi.

Ni njia ya kutoa shukurani kwa kuteuliwa ubunge
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
sasa sishangai kwanini alisainishwa cheki ya kagoda bila kusoma na baadaye
kudai amedanganywa na Balali kusaini cheki feki bila hata ya kumripoti polisi
mtu aliyemdanganya kusaini cheki hiyo.
 
Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
107
hivi kumbe hili gazeti lilikuwepo tangu uhuru?
Sasa ni mali ya ccm au serikali ingawa bongo kutofautisha chama na serikali ni ngumu?
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,631
8,445
Hapo hakuna kipya, mama ni mwanaCCM na gazeti ni la CCM... na gazeti ndo limeuliza, tulitegemea nini?

Nasubiri JK alisifie gazeti la habari leo kuhusu wale mapadre wanavyotenga waumini... he is capable of doing that!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom