Mboka Manyema
Member
- Nov 21, 2008
- 48
- 38
Date::8/15/2009
Festo Polea
WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli amesema samaki waliokamatwa katika meli iliyokuwa ikifanya uvuvi haramu hawajauzwa na akawataka kutojali gharama za kuhifadhi samaki hao ambazo zinafikia dola 1,184,000 za Kimarekani.
Waziri Magufuli alisema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha Bahari Foods Ltd cha Mwenge jijini Dar es Salaam ambako samaki hao wanahifadhiwa tangu walipotolewa kwenye meli hiyo iliyokamatwa pwani ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.
Magufuli alisema tani moja ya samaki hao huifadhiwa kwa gharama ya dola 800 za Kimarekani na samaki wote ni tani 296.32 na hivyo gharama za kuwahifadhi kwa mwezi niu dola 236,800 (sawa na Sh307.8 milioni).
Kwa mantiki hiyo gharama za kuhifadhi samaki hao tangu walipokamatwa mwezi Machi sasa zimefikia dola 1,184,000.
Kinachotakiwa kuangaliwa si gharama ya kuhifadhi samaki hao, bali ni kushukuru mafanikio ya kukamata maharamia hao pamoja na kuomba kesi hiyo iweze kuisha mapema na maamuzi kutolewa, alisema Magufuli.
"Jukumu la serikali lilikuwa kukamata na kukabidhi maharamia hao wa samaki wetu kwa Jeshi la Polisi, na ndivyo tulivyofanya na leo (jana), nimekuja kuhakiki kama wapo na wote tunashuhudia kuwa wapo hivyo bado hawajauzwa hadi maamuzi ya mahakama yatakapotolewe."
Magufuli alisema kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba maamuzi ya Mahakama Kuu yataheshimika, hata kama itaamua wagawiwe bure.
"Sasa tumefikia hatua nzuri kwani upelelezi umekamilika na mahakama itakapoamua kama kuwauza tutawauza na kama kuwagawa kwa watu waliopatwa na misukosuko ya mabomu Mabagala, ama waandishi wa habari ama mashuleni na vyuo mbalimbali ama kokote tutafanya hivyo," alisema Magufuli.
Magufuli alisema anapenda kesi iishe haraka ili wengine wanufaike kama zilivyo nchi nyingine ambako kesi za maharamia wa samaki husikilizwa kwa muda mfupi.
"Nchini Msumbiji kesi kama hizo husikilizwa kwa wiki mbili, Afrika Kusini siku nne na Namibia husikilizwa kwa siku saba na maamuzi hutolewa wakati kwetu imefika miezi zaidi ya mitano. Kwa kuanzia siyo mbaya kwa kuwa tunajifunza," alisema Magufuli
Pia Magufuli alisema anatarajia kufanya doria nyingine kwenye kwani ya Tanzania kusaka maharamia wengine kwa kuwa wameonekana kwenye rada wakiendelea na wizi wa samaki.
Naye naibu kamishina, Peter Kivuyo alisema samaki hao bado wapo chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi kama kielelezo cha kesi na hawaguswi wala kuuzwa.
Source Mwananchi
FISADIS IN ACTION