Zaidi ya Sh307m hutumika kuwahifadhi samaki wa Magufuli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zaidi ya Sh307m hutumika kuwahifadhi samaki wa Magufuli!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mboka Manyema, Aug 15, 2009.

 1. Mboka Manyema

  Mboka Manyema Member

  #1
  Aug 15, 2009
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Date::8/15/2009

  Festo Polea


  WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli amesema samaki waliokamatwa katika meli iliyokuwa ikifanya uvuvi haramu hawajauzwa na akawataka kutojali gharama za kuhifadhi samaki hao ambazo zinafikia dola 1,184,000 za Kimarekani.

  Waziri Magufuli alisema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha Bahari Foods Ltd cha Mwenge jijini Dar es Salaam ambako samaki hao wanahifadhiwa tangu walipotolewa kwenye meli hiyo iliyokamatwa pwani ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.

  Magufuli alisema tani moja ya samaki hao huifadhiwa kwa gharama ya dola 800 za Kimarekani na samaki wote ni tani 296.32 na hivyo gharama za kuwahifadhi kwa mwezi niu dola 236,800 (sawa na Sh307.8 milioni).

  Kwa mantiki hiyo gharama za kuhifadhi samaki hao tangu walipokamatwa mwezi Machi sasa zimefikia dola 1,184,000.

  Kinachotakiwa kuangaliwa si gharama ya kuhifadhi samaki hao, bali ni kushukuru mafanikio ya kukamata maharamia hao pamoja na kuomba kesi hiyo iweze kuisha mapema na maamuzi kutolewa, alisema Magufuli.

  "Jukumu la serikali lilikuwa kukamata na kukabidhi maharamia hao wa samaki wetu kwa Jeshi la Polisi, na ndivyo tulivyofanya na leo (jana), nimekuja kuhakiki kama wapo na wote tunashuhudia kuwa wapo hivyo bado hawajauzwa hadi maamuzi ya mahakama yatakapotolewe."

  Magufuli alisema kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba maamuzi ya Mahakama Kuu yataheshimika, hata kama itaamua wagawiwe bure.

  "Sasa tumefikia hatua nzuri kwani upelelezi umekamilika na mahakama itakapoamua kama kuwauza tutawauza na kama kuwagawa kwa watu waliopatwa na misukosuko ya mabomu Mabagala, ama waandishi wa habari ama mashuleni na vyuo mbalimbali ama kokote tutafanya hivyo," alisema Magufuli.

  Magufuli alisema anapenda kesi iishe haraka ili wengine wanufaike kama zilivyo nchi nyingine ambako kesi za maharamia wa samaki husikilizwa kwa muda mfupi.

  "Nchini Msumbiji kesi kama hizo husikilizwa kwa wiki mbili, Afrika Kusini siku nne na Namibia husikilizwa kwa siku saba na maamuzi hutolewa wakati kwetu imefika miezi zaidi ya mitano. Kwa kuanzia siyo mbaya kwa kuwa tunajifunza," alisema Magufuli

  Pia Magufuli alisema anatarajia kufanya doria nyingine kwenye kwani ya Tanzania kusaka maharamia wengine kwa kuwa wameonekana kwenye rada wakiendelea na wizi wa samaki.

  Naye naibu kamishina, Peter Kivuyo alisema samaki hao bado wapo chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi kama kielelezo cha kesi na hawaguswi wala kuuzwa.

  Source Mwananchi
  FISADIS IN ACTION
   
 2. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wamekuwa samaki wa Magufuli?

  Tatizo mfumo wetu wa sheria una mizengwe, wewe mwizi anakamatwa na ushahidi upo basi kesi itazungushwa weee bila sababu za msingi. Sijui wanangija mtuhumiwa ajifikirie apele chochote?

  Sasa sijui watasema ni kosa la waziri aliyekama wezi? au polisi wanaochelewesha uchunguzi au labda mahakama hawana haraka kwa vile hawakupewa kidogodogo?

  Mbona kesi ya dhamana ya marehemu Ditto ilipelekwa chapchap?
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kulikuwa na ulazima wa kuwahifadhi wote (tani nzima) muda wote wa upelelezi wa kesi ukiendelea?
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.
   
 5. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kwa hili kweli akili ni nywele ndugu yangu.

  DUH!!!!

  Bring me my GUN!!
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu... nashukuru kwa kuuliza hilo swali!!! Roho inaniuma sana kwasababu a very good move by our minister has turned into his nightmare simply because the system wants to frustrate people with good deed... YES THEY DO IT KUVUNJA MOYO WENYE MAPENZI MEMA NA NCHI YETU

  Tatizo la kwanza, sikumbuki kusikia wakulu wa juu zaidi kuonyesha total support kwa bwana Pombe Magufuli wakati wa tukio hadi leo hii... Something is wrong somewhere
  Baada ya kuamua kunadi wale samaki... Sielewi kwanini ule mnada uliongozwa kama mndana wa makochi au majokofu yaliyotumika. Naamini kuna namna ambayo ingetumika kuweza kupata international competitive process to auction wale samaki kwa mfumo wa kisasa
  Kuhusu suala la kuhifadhi wale samaki, bado sijaelewa kama napo proper procurement procedures zilifuatwa, hata kama ni emergency sourcing of storage facilities
  Nachanganyikiwa zaidi kuona kesi inarefushwa na siamini kwamba wale samaki wanahifadhiwa kwa ajili ya ushahidi, nahisi ni system yetu imekosa capacity ya kutengeneza fedha kwa kupitia samaki hawa waliobwa na wageni wezi!!!
  Cha mwisho kabisa ni jinsi baadhi ya waandishi wanapokosa uelewa wa mfumo na patriotism mpaka wanasema ni samaki wa magufuli.... LETS OWN OUR COUNTRY AND RESOURCES AND ADDRESS WALE SAMAKI KAMA "SAMAKI WA WETU WALIOIBIWA NA KUPATIKANA WANATUGHARIMU KIASI KADHAA" ILI WOTE TUBEBE OWNERSHIP YA RASILIMALI ZETU

  HAWA SI SAMAKI WA MAGUFULI, NI SAMAKI WETU

  WAHUSIKA, YULE MKUU WA TAASISI YA RESEARCH YA SAMAKI NA UVUVI AMESHAWAHI KUSHAURIWA NAMNA KADHAA ZA KUOKOA TAIFA LETU NA HASA HILI LA SAMAKI, JE KUNA MTU ANAMJUA AMUULIZE???
   
 7. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Soma vizuri! Gharama ni zaidi ya Billioni hadi sasa!

  Hao samaki ilitakiwa wapigwe mnada, hela zihifadhiwe hadi hukumu ya mahakama itakapopatikana.
  Huu ni upuuzi wa hali ya juu, tutajikuta tumepata loss mwisho wa kesi.
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mbaya zaidi, na kesi yenyewe tuje tushindwe!

  Amandla......
   
 9. i

  inawezekana Member

  #9
  Aug 17, 2009
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  something fishy inaendelea hapo, ndo maana orijino comedy waliigiza wakionyesha samaki hao walivyokonda, kumbe walilenga
   
 10. Maguma

  Maguma Member

  #10
  Aug 17, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na shidwa kuamini kuifazi pesa kesi pesa tukishidwa muda poteza kweli akili ninywele unaweza ukaazima kama wigi
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wazee, hapoa ndio natamani nishike kabunduki nikachape mtu mmoja pale uvuvi...

  Tumefikia wapi?

  Pinda bado uko na mavazi wakati hili lilikuwa muhimu sana kwa nji yetu na motivation kwa wale wanaopigania rasilimali zetu??
   
 12. C

  Chereko Member

  #12
  Oct 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Hizo pesa zinalipwa na walipa kodi? Makubwa! Hata kama tumekamata wezi sawa lakini kwa mtaji huu Mhh! Ok tumekamata ndio je ulinzi baharini vipi? Wale wasauzi sii washaondoka?
   
 13. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  kesi ni pesa na kuwahifadhi ni pesa!gharama juu kwa juu.wangezinadi hata kwa bei ya hasara kama kuwatunza ni gharama kubwa sana!
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mbona hamuulizi kama tukishinda kesi??

  The guy is smart!
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hata tukishinda kesi, bili ya kuwatrunza italipwa na kodi zetu kwa maana serikali ndio iliyokwenda kuhifadhi hao samaki kwa mtu binafsi
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,219
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  n yale yanayohifadhia samaki ya mwandosya na yeye anahusikaje jamani kw ahili???embu magufuli tuelezeni ama ndio dili ya mwandyosya kupata za campaign 2010...huu ni upuzi kabisa
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,219
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Hata tukishinda kesi

  washindie kwa masati??? wakati umeambiwa bado wanachunguza ;wameambiwa watafute kama hao samaki wa tanzania hakuna aliekuja na jibu mpaka leo
   
 18. C

  Chuma JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kuna tetesi wamepigwa biti na Ubalozi wa China hapa DSM...!!! Wachina sasa ni very powerfull....at the end Wachina watashinda.

  hizo pesa za kuhifadhi hawa samaki sijui zatoka wapi wakati wanashindwa kuwa na Boti za kisasa za Uvuvi au Kuwawezesha wa wa-TZ uvuvi wa kisasa. bei ya samaki locally ni kubwa sana kulinganisha na Bahari ilituzunguka from Znz,Tanga to Mtwara

  Kweli WaTz Bongo zetu Hazifanyi kazi ipasavyo.
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kushinda au kushindwa... kesi gani mwaka mzima??? Ile kesi ilikuwa ya vikao vitatu tu!! Mkiambiwa we have a corrupt legal system... mnakuwa wakali

  Mijitu inaangalia vouchers tu humu bongo

  mashuzi matupu!!

  Halafu wanawapa majembe sijui yono ndio waongoze mnada!!
   
 20. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuwe makini na kesi za kimataifa-mbona kesi hii imechukua muda mrefu walishinda fidia nahisi itakuwa kubwa sana.
   
Loading...