Papasa
JF-Expert Member
- Nov 2, 2018
- 1,947
- 4,131
Nimeona hili habari, isome kisha nami nitatoa maoni yangu...
Zahanati ya Mashati, Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro, iliyotajwa kujengwa zaidi ya miaka tisini iliyopita ipo hatarini kuanguka baada ya zahanati hiyo kuwa na nyufa hali ambayo inatishia usalama wa wagonjwa pamoja na watoa huduma katika zahanati hiyo.
Akizungumzia namna zahanati hiyo inavyotishia usalama wa wakazi wa maeneo hayo Diwani wa Kata ya Katangara Mrere, Venance Malle, amesema zahanati hiyo inahudumia wakazi wa Katangara Mrere na Kisare, hivyo ameiomba Serikali kufanya ukarabati wa zahanati hiyo.
Maoni yangu:
Serikali ilipaswa kumalizana na mambo ya Zahanati miaka 20 nyuma huko lakini bado ni tatizo hata sasa lakini cha ajabu wanajifia kujenga Zahanati katika Karne hii tena kwa hela mikopo hii ni aibu na umaskini wa akili, ukila na kipofu usimshike mkono.
Hizi ni dalili za uzembe na kukosekana kwa uwajibikaji kwa baadhi ya mamlaka ndani ya Serikali.