Wakati Tanzania na China zikielekea kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia ni vyema kutilia mkazo mawasiliano baina ya watu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
微信图片_20240111142831.png

Wakati Tanzania na China zikitarajiwa kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia mwaka 2024, huku zikikubaliana kufanya mwaka huu wa 2024 kuwa wa utalii na utamaduni, nchi hizi mbili kwa sasa zinajivunia kuwa na ushirikiano wa kimkakati, ambao umechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya watu wake. Bila shaka, iwapo zinataka uhusiano wa pande hizi mbili uimarike zaidi ya hapa ulipofikia, ni lazima pia kuweka mkazo kwenye mawasiliano baina ya watu na utamaduni.

Wakati rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alipotembelea China Novemba mwaka juzi baada ya kualikwa na rais Xi Jinping wa China, kwenye mazungumzo yao alisisitiza umuhimu wa mawasiliano baina ya watu na utamaduni na kuhimiza mawasiliano zaidi ya kielimu na vyombo vya habari kati ya nchi hizi mbili, pamoja na kuzidi kuendeleza urafiki kati ya watu wa pande mbili. Kwa nini mawasiliano baina ya watu na watu ni muhimu? Na nini kifanyike ili kuimarisha maelewano kati ya Wachina na Watanzania?

Wakati ushirikiano wa watu wa China na Tanzania unaendelea kukua siku hadi siku, ni muhimu kwa makampuni ya China, wafanyabiashara na wafanyakazi kupata uelewa mzuri wa hali za ndani, kama vile mila, desturi, utamaduni, kanuni na lugha. Hata hivyo, kinachoonekana ni kwamba baadhi ya wakati vizuizi vya lugha na tofauti za kitamaduni vinaweza kusababisha kutoelewana, na huenda vikaufanya uhusiano uendelee kuwa hatarini ikiwa pande zote mbili hazitafanya kazi kikamilifu ya kuvipunguza.

Ili kuondoa usumbufu wa namna hiyo, makampuni kadha wa kadha ya China yaliyopo katika nchi za Afrika, mbali na kupeleka wafanyakazi wanaozungumza Kiingereza ili kurahisisha mawasiliano, pia siku hizi yanajitahidi kuajiri Wachina wanaofahamu lugha za wenyeji. Mathalan makampuni ya China yaliyopo Tanzania yanaajiri japo Wachina wawili watatu wanaofahamu lugha ya Kiswahili. Mbali na hapo pia wafanyakazi wa China wanaokuwepo katika nchi za Afrika ambao hawajui lugha za wenyeji, wanajitahidi sana kujifunza kwa haraka ili kuondoa kizuizi cha lugha.

Kadhalika kwa sasa makampuni ya China yanayoandaa warsha za mafunzo, baadhi yao yanazingatia Kiswahili, huku mengine yakizingatia utamaduni wa Tanzania na sheria za kazi. Jumuiya ya Wachina na makampuni ya biashara nchini Tanzania pia yameshiriki kikamilifu katika mipango ya uwajibikaji wa kijamii ambayo inalenga kuboresha maisha ya watu wa kawaida katika jumuiya za mitaa. Juhudi kama hizi ni muhimu ili kupata uelewa wa kina wa wenyeji wao.

Kuimarisha mawasiliano kati ya watu na watu kuna umuhimu mkubwa wa kiutendaji hususan katika kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja. Chini ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), juhudi nyingi zimefanywa ili kubuni mbinu na njia mpya za kuhamisha teknolojia na kubadilishana maarifa. Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) kilizindua mradi wa "Teknolojia Rahisi, Mavuno Makubwa" mwaka 2011, ambao ni mradi wa ushirikiano wa kilimo unaotekelezwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, Serikali ya Tanzania na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro.

Mwaka 2018, kwa kushirikiana na mamlaka ya Morogoro, CAU ilianzisha mradi mwingine wa ushirikiano wa kilimo uitwao “Maharagwe Madogo na Lishe Kubwa” ukilenga kuhamasisha kilimo mseto cha mahindi na soya kwa wakulima wa huko na kuboresha muundo wao wa lishe. Miradi hii miwili ni mifano madhubuti ya mawasiliano ya watu na watu na ushirikiano kati ya China na Afrika kwa ajili ya usalama wa chakula.

Mawasiliano ya watu na watu, hasa ya wanafunzi, wataalam, wasomi na mashirika yasiyo ya kiserikali, yanaweza kuhamasisha juhudi za pamoja katika kutafuta maslahi makubwa zaidi na ya pamoja. Kupunguza umaskini na kubadilishana uzoefu wa maendeleo ni miongoni mwa maslahi ya pamoja kati ya nchi hizo mbili.

Ili kuunda mawasiliano ya hali ya juu kati ya watu na watu wa China na Tanzania, wafanyakazi wa vyombo vya habari lazima wabebe jukumu kubwa zaidi. Wasomi mara nyingi wamekuwa wakitaja changamoto na matatizo kadhaa hasa linapokuja suala la kuripoti uhusiano kati ya China na Afrika, ambazo ni pamoja na habari za uwongo, habari potofu, zinazogusa hisia na za kibaguzi. Utangazaji wa kina na unaofaa kuhusu Afrika pamoja na uhusiano kati ya China na Afrika unahitaji mawazo, tafakari na mawasiliano ya kina kati ya wataalamu wa vyombo vya habari kutoka mashirika ya China na Afrika.
 
Back
Top Bottom