Majukumu ya Serikali na walichofanikiwa kwa miaka 60 ya Uhuru

Mnyunguli

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
1,570
3,906
Tangu nijitambue nikiwa kidato cha 3 na miaka 17 mpaka leo na miaka yangu 26 sijaona Serikali imefanikiwa kwenye lipi katika kazi zifuatazo za serikali au kipaumbele chao zaidi ya upigaji wa mali za umma.

Yafuatayo ndiyo mambo muhimu na ya lazima serikali yoyote inatakiwa ifanye kwa wananchi wake kuleta maendeleo

1. Huduma za afya: Serikali inapaswa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wake kwa bei ya chini sana.Taifa lenye wagonjwa wengi haliwezi kuendelea

2. Elimu bora: Serikali inapaswa kuwekeza katika elimu bora, kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu hii inaenda pamoja na kuboresha miundombinu na mitaala bora.Huwezi amini awamu ya mwendazake shule za hizi mbovu za serikali zilikuwa zinaongoza kitaifa hahahaha.

3. Upatikanaji wa ajira: Serikali inapaswa kuweka mazingira rafiki kwa ukuaji wa uchumi na kuunda fursa za ajira ajabu ni kuwa Hili jukumu serikali wanalikwepa kama haliwahusu

4. Usalama na haki: Serikali ina jukumu la kuhakikisha usalama wa raia na mali zake na ulinzi wa haki za binadamu ila kwa Police wetu hawa wenye tamaa kila mtu anawajua.

5. Miundombinu na huduma za msingi:kama barabara, umeme, mawasiliano ,maji safi na salama.Ninavyo andika uzi huu umeme hakuna maji hakuna na hapa nipo jijini Daslamu huko vijijin sijui hali ikoje.

6. Ulinzi wa mazingira: Serikali ina jukumu la kulinda mazingira na kusimamia rasilimali za asili,nasikia Bandari na ngorongoro zimeuzwa huko.

7. Kuimarisha usawa kiuchumi na kijamii: Hapa ni kupunguza pengo la kipato walio nacho na wasio nacho pia kupigania haki za wanawake na watoto pamoja kuwawezesha kundi la walemavu na makundi mengine yaliyotengwa

8. Uongozi bora na uwajibikaji: lazima kuwepo mfumo wa uongozi bora, uwazi, na uwajibikaji. Inapaswa kusimamia rasilimali za umma kwa uaminifu, kushirikisha wananchi katika mchakato wa maamuzi, na kuwawajibisha viongozi wanaokiuka maadili na sheria.Hapa ndio kiini cha Tatizo na kama hatutafikia hatua hii basi Maendeleo Tanzania tusahau.

The Good thing is that this CCM government has remained unchanged for over 60 years, but it is unclear what their priorities are if they have not successfully achieved even 40% of their governmental duties.
 
Back
Top Bottom