Yupo wapi Mtulia wa Kinondoni?

Yupo wapi Mtulia wa Kinondoni?

Viongozi wangu wa CCM naombeni toeni kauli juu ya haya yanayo zungumzwa juu ya Mbuge wangu Mtulia au Mbuge wangu jitokeze hadharani tukuone tu ili watesi wako waaibike!.
 
Haya mambo siyo ya kuyadharau, kwani nimepata taarifa kuwa yule aliyekuwa mbunge wa Kilombero Abdul Mteketa yuko hoi bini tafani sio kifedha tu bali hata kiafya mpaka anashindwa kujitibu na anapitisha bakuli watu wamchangie!! Mteketa huko Kilombero alipokuwa anagombea ubunge mtakumbuka kuna binti mmoja mbunge wa viti maalum Chadema alifariki kwa ajali ya gari na yeye akahusishwa!! Damu ya binadamu haipotei bure hivi hivi!!

Mungu ana amri yake mmoja isemayo "Usimtendee mwenzio yale ambayo usingependa wewe utendewe" , hii amri ndio chanzo cha misemo kuwa " UKIUA kwa upanga ,utakufa kwa upanga "; " what goes around must come around"!! Kwahiyo namalizia kwa kusema kuwa viongozi lazima watambue kutokana na mifano hiyo kuwa malipo ni hapa hapa duniani kwani wakina GHABO wa Ivory Coast na James Taylor wa Liberia walitegemea yaliyowapata?

Kweli Abdul Mteketa alihusishwa na Jimbo la MORO enzi hizo Susanne Kiwanga na Regia Mtema walikuwa wanakimbiza sana wakiwa viti maalum Sasa Huyu Abdul ikadaiwa akamtenda hata hivyo haikusaidia Sana uchaguzi uliofuata aliangushwa na mwingine

Baba yake anaitwa Privatus Mtema ni mtu wa kusali Sana ,ni kiongozi wa Charismatic Katoliki
 
Acheni uzushi huo......

hivi mtajisikiaje siku mkimuona anaapishwa? mtakuja mfute huu uzi? ni vyema mkajikita kwenye hoja lakini sio gossips

AnaweZa kuapishwa akipona kama kweli anaumwa Mungu sio athumani
Watu wanahoji kwakua ni wiki Sasa wabunge wako Dodoma
 
Mbona kama haya mambo ya albadir yapo, mbona kwa tundu lisu hayakufanywa? Ili kuisaidia serikali ktk hao watu wasiojulikana
 
Sorry,
Huyu jamaa ndio yule wanaesema yuko Kijijini kwao huko Undengerekoni anaongea mwenyewe tu, muda wote anataja taja ovyo viungo vya uzazi?
Au nimemfananisha?
Hebu sema yuko kijiji gani huko Undengerekoni watu wamfuate kimya kimya.
 
Kama una HAMU naye nenda nyumbani kwake utamkuta,huku JF tuletee mada za maendeleo na ukosoaji wa kuchagiza maendeleo ,sio hoja za kitaarab taarab!
 
tulikuwa naye jana kinondoni, jamaa ni mzima wa afya, acheni kusambaza uongo , ehhhh
 
Acheni uzushi huo......

hivi mtajisikiaje siku mkimuona anaapishwa? mtakuja mfute huu uzi? ni vyema mkajikita kwenye hoja lakini sio gossips
Hapo atakuwa kashapona tayari
 
Back
Top Bottom