Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Kama wanamtandao wataguswa, hasa rostam na mwenzie hapo nitaona kuna maana! Na je hii haiwezi kumlipua JK mwenyewe? Sina uhakika kama mwenyewe kwa kwa dhamira yake ya dhati anakubaliana na haya.Natamani nimsikie akiyazungumzia

Calnde
Mwenyewe hatayazungumzia tena, atajidai yako mahakamani na yeye hawezi kuingilia mahakama wait and se...
 
"Suala la kuwa jambo hili ni usanii sikubaliani nalo kabisa. Hivi nani anaweza kukubali kufanywa kafara ionekane kuwa kazi imefanyika kweli.
Wote tumewaona kwa macho yetu wenyewe wako mahakani. wamesomewa mashtaka, waandishi walikuwepo waliotuhabarisha. Wamepewa nafasi ya kudhaminiwa kwa masharti yaliyowekwa na mahakama. Wameshindwa. Wako rumande. (Kama hujawahi kupelekwa rumande nakupa taarifa kuwa ukifika na kuingizwa ndani unaamriwa kuvua nguo zote, unabaki uchi wa mnyama na kukaguliwa sehemu zote mpaka ile ya haja kubwa ili usiingie na kitu kisichotakiwa) Je, yote hii ni cinema ya hollywood kweli????
Kesi itaendeshwa, watajitetea mwisho mahakama itatoa uamuzi. Sio lazima wafungwe, je muda wote huo watakao kuwa wamepoteza, heshima kuharibika, gharama za mawakili, muda wa kula raha. Je, vyote hivyo ni usanii kweli???? Tukubali kuwa walao hili la kuwafikisha mahakamani tu limewezekana. Wakishinda ni suala jingine.

Majambazi wanakamatwa "red handed" na bunduki wanajitetea na wanashinda, sembuse hawa. Something has been done bwana, sio hollywood cinema."


You are right on the money mkuu.

Kuna watu wanadhani kazi ya mahakama ni kufunga tu kila mtuhumiwa,... wanasahau kuwa mahakama inaweza kutowatia watu hatiani vilevile na ukawa bado ni utawala wa sheria. Sasa hii ya kusema midhali kuna possiblity ya hawa wakuu kushinda kesi basi ndio kigezo cha kusema the whole process is a sham inashangaza!.

Kazi iliyofanyika ni ya kupongezwa, si ndogo hata kidogo...halafu kuna mtu anaifananisha na kiula. Kiula utamfananisha na Mramba kwenye political circles za nchi hii?... You must be kidding!.. Someni CV ya mramba ndio mtajua kumlaza lupango mkulu kama huyu maana yake nini.

Tuiache Mahakama ifanye kazi yake, ikiwafunga au kuwaachia huru, yote ni matokeo ya utawala wa sheria... Mwenye macho haambiwi tazama.

Mkuu umesema kweli si unajua Hawa Chadema hawataki tuu mpaka DJ mbowe achukue nchi ndio wakubalil
 
"Suala la kuwa jambo hili ni usanii sikubaliani nalo kabisa. Hivi nani anaweza kukubali kufanywa kafara ionekane kuwa kazi imefanyika kweli.
Wote tumewaona kwa macho yetu wenyewe wako mahakani. wamesomewa mashtaka, waandishi walikuwepo waliotuhabarisha. Wamepewa nafasi ya kudhaminiwa kwa masharti yaliyowekwa na mahakama. Wameshindwa. Wako rumande. (Kama hujawahi kupelekwa rumande nakupa taarifa kuwa ukifika na kuingizwa ndani unaamriwa kuvua nguo zote, unabaki uchi wa mnyama na kukaguliwa sehemu zote mpaka ile ya haja kubwa ili usiingie na kitu kisichotakiwa) Je, yote hii ni cinema ya hollywood kweli????
Kesi itaendeshwa, watajitetea mwisho mahakama itatoa uamuzi. Sio lazima wafungwe, je muda wote huo watakao kuwa wamepoteza, heshima kuharibika, gharama za mawakili, muda wa kula raha. Je, vyote hivyo ni usanii kweli???? Tukubali kuwa walao hili la kuwafikisha mahakamani tu limewezekana. Wakishinda ni suala jingine.

Majambazi wanakamatwa "red handed" na bunduki wanajitetea na wanashinda, sembuse hawa. Something has been done bwana, sio hollywood cinema."


You are right on the money mkuu.

Kuna watu wanadhani kazi ya mahakama ni kufunga tu kila mtuhumiwa,... wanasahau kuwa mahakama inaweza kutowatia watu hatiani vilevile na ukawa bado ni utawala wa sheria. Sasa hii ya kusema midhali kuna possiblity ya hawa wakuu kushinda kesi basi ndio kigezo cha kusema the whole process is a sham inashangaza!.

Kazi iliyofanyika ni ya kupongezwa, si ndogo hata kidogo...halafu kuna mtu anaifananisha na kiula. Kiula utamfananisha na Mramba kwenye political circles za nchi hii?... You must be kidding!.. Someni CV ya mramba ndio mtajua kumlaza lupango mkulu kama huyu maana yake nini.

Tuiache Mahakama ifanye kazi yake, ikiwafunga au kuwaachia huru, yote ni matokeo ya utawala wa sheria... Mwenye macho haambiwi tazama.

Kwa wafuatiliaji wa sheria zetu za Tanzania tunajua fika kuna sheria za walalahoi walioiba baskeli au kuku kuozea keko na matajiri na vingunge walioiba mabilioni kuendelea kupeta uraiani wakati 'uchunguzi' unaendelea. Pia tumeshaona ya Marehemu Ukiwaona Mzuzuri pamoja na kuua aliachiwa huru katika mazingira ya kutatanisha, kama angekuwa ni mlalahoi angeozea rumande kwa kesi ya mauaji. Hivyo ni mapema mno kuanza kutoa pongezi kabla ya kuona mkondo wa kesi hizi.
 
Part 1

Wakuu jana na leo kuna yaliyojiri na kutokujiri, katika hatua mpya ya serikali ikiwa ni hatua ya awamu ya pili, yaani kuwafikisha viongozi wakuu wa serikali na wananchi waliohusika na shutuma mbali mbali za ubadhirifu wa mali ya umma, this is my take on all things considered:-

1. Kwanza ningependa kusema kwamba wananchi tunatakiwa kuwa waangalifu sana na yanayojiri, kwa sababu sio siri ni mengi mno na hakuna muongozo kamili, kwa hiyo kila kukicha kutakua na habari mbali mbali, za uongo na za kweli, lakini ninaamini kwamba wengi wetu tutakuwa tunajaribu tu kuhabarishana kwa nia njema as we get this very limited na sometimes impossible to get infos na dataz, zikiwa na mapungufu tusameheane sisi ni binadamu na wanaotupa pia ni bina-adam wenye mapungufu kama sisi kwa hiyo hata habari zinaweza kuwa na mapungufu, lakini haina maana zisichambuliwe kwa JF style.

- Ni lazima wananchi tuwe waangalifu na motives za serikali na wanasiasa wetu, yaani viongozi, ni lazima tuchambue ukweli na uongo wa yanayojiri, tujue sheria ilipo na isipokuwepo, tujue cinema na comedy zilipo, tuchambue wanashikwa kwa amri ya nani, kwa nini, na sheria inasema nini kuhusu suala zima la kushikwa kwao na kufika mahakamani, je mahakama waliyofikishwa ndiyo hasa inayotakiwa kisheria ya Jamhuri? Ili tusije tukawa tunachezewa Ze-Comedy za kampeni ya urais za 2010.

2. With all due respect kwa rais wa Jamhuri, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, ni kwamba yaliyokwisha fanyika yanatia moyo sana tena sana na hongera sana mkuu na Mungu akubariki, na mimi binafsi kama uchaguzi wa rais ukifanyika leo au kesho, nitakupatia kura yangu bila tatizo, kwa sababu never in my life nilitegemea kuona mawaziri wawili wa zamani, na marafiki wa karibu sana wa rais wa zamani wakifikishwa kwenye mkono wa sheria, na hasa mahakama ya Kisutu.

- Ninapafahamu sana pale mahakamani, kwa sababu nimekwenda sana kuwaangalia marafiki wakiwa katika state ya kutuhumiwa na kufikishwa pale kwa ajili ya kesi za mwanzo, ninasema hivi kule nyuma ambako mahabusu hupitia kabla ya kuingia rasmi kwenye mahakama, sio mahali hata pa kumpeleka adui wako usiyemtakia mema, kwanza ile harufu inayotoka kule ndani sijawahi isikia anywhere duniani, halafu najua for a fact kwamba mahabusu wanapokuwa wanasubiri kuingia mahakamani hufanyiana mambo mengi sana ya kinyama kwenye kile chumba bila ya kujali the next person anayeangalia ni nani maana ile opportunity huwa haitokei mara kwa mara, sasa kujua kwamba hawa mawaziri wa zamani na mmoja a sitting mbunge na huyo mwingine ni mbia wa kampuni moja na rais wetu mstaafu, kwa kweli ni un imaginable kwa Tanzania yetu.

- Sio nia yetu kufurahia misery ya kiongozi yoyote yule, lakini knowing kwamba huenda vitendo wanavytotuhumiwa navyo vikithibitishwa kisheria kua ni vya kweli, vinaweza kuwa viliwahi kusababisha vifo vya watoto wadogo, wazee na vilema kwa sababu mbali mbali kama za kukosa dawa, huku watuhumiwa wakizifanyia sherehe za kifisadi pesa hizo ambazo zingetumika kulipia hayo madawa, then inakuwa faraja kuwaona watuhumiwa hawa yaani mawaziri wa zamani wakiungana na wezi wa kuku, wezi wa mifukoni, wezi wa mbuzi, wabakaji na kadhalika pale kwenye chumba kile maalum cha mahabusu pale nyuma ya mahakama ya Kisutu, wenyewe hukiita chumba cha damu!
 
Kwa kuongezea analysis ya Mzee FMES,

Ndugu yetu Rais Kikwete, If you are playing a Political Game Mungu Atakulaani... Believe me!!!!!!

Hatutaki kuja gundua baada ya miezi ama miaka michache mbeleni kwamba this was a political Game. Mungu mara zote husikiliza sauti za waja wake, na ingawa sio vizuri kumwombea mtu kitu kibaya, mimi nina uhakika kwamba something bad will happen to him kama ni kweli anatuchezea akili sasa hivi sisi watanzania milioni 42 ambao tumeanza kupata matumaini... I swear!!!!!

JF Please, don't forget to quote me maandiko haya yakija timia.
 
Ndugu yetu Rais Kikwete, If you are playing a Political Game Mungu Atakulaani... Believe me!!!!!!

- Tayari kuna habari za utatanishi sana kuhusiana na habari ya leo, according to the dataz inasadikiwa kwamba kuna minong'ono within the ranks za viongozi wa juu ndani ya CCM, kwamba so far hii kamata kamata bado haijashika Mtandao hata mmoja, WHY? na hatimaye habari zimemfikia mkulu.

- Inafahamika wazi huko ndani kwamba ile awamu ya kwanza ya kina Jeetu Patel, was never a Mtandao, na according to the more dataz Patel detested Mtandaos na made it known kwao. Na sio siri kwamba Yona na Mramba hawakuwa Mtandao je inaweza kuwa ndio the idea ya kuwashika waliotakiwa kushikwa leo ili kuleta balance? Au ndio sababu ya kushikwa kwao kina Yona anyways?

If all this are to be believed then je kweli kuna sheria hapa au ni Ze-Comedy?
 
- Tayari kuna habari za utatanishi sana kuhusiana na habari ya leo, according to the dataz inasadikiwa kwamba kuna minong'ono within the ranks za viongozi wa juu ndani ya CCM, kwamba so far hii kamata kamata bado haijashika Mtandao hata mmoja, WHY? na hatimaye habari zimemfikia mkulu.

- Inafahamika wazi huko ndani kwamba ile awamu ya kwanza ya kina Jeetu Patel, was never a Mtandao, na according to the more dataz Patel detested Mtandaos na made it known kwao. Na sio siri kwamba Yona na Mramba hawakuwa Mtandao je inaweza kuwa ndio the idea ya kuwashika waliotakiwa kushikwa leo ili kuleta balance? Au ndio sababu ya kushikwa kwao kina Yona anyways?

If all this are to be believed then je kweli kuna sheria hapa au ni Ze-Comedy?

Hili bomu lazima limlipukie Kikwete maana siasa ni mchezo mchafu. Kama alifikiri atakamata walio nje ya mtandao bila Watanzania na wale walio nje ya mtandao kumshtukia basi ameula wa chuya, labda kama yeye hakujihusisha na ufisadi kitu ambacho si rahisi maana waliombeba katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya mgombea wa CCM 2005 wote ni mafisadi ambao walimchangia mabilioni. Si dalili nzuri kwa JK hapo 2010.
 
- Another scenario according to the dataz, ni kwamba katika kikao cha mwisho cha cc kwa mara ya kwanza ever kulikuwa na shouting match between muungwana na b mbele ya wajumbe, kisa na mkasa mama Mamuya, aliyekataliwa kugombea uenyekiti wa uwt.

- Baada ya kukataliwa kugombea uwt, mamuya alifanya copy za ushahidi wake wote kuhusiana na wizi uliotokea uwt akiwa katibu na hata kumfukuzisha kazi, ushahidi unaomshika pia mwenyekiti wake mama msekwa, alipeleka ushaidi huu kwa wajumbe wote wa cc b akiwa mmojawapo.

- b ambaye hajawahi kuzungumza hata mara moja kwenye vikao hivyo, kwa mara ya kwanza this time aliomba kusema, akitaka kujua fate ya mamuya...." na alimtupia muungwana moja kwa moja swali kwamba anataka kujua ana mpango gani naye as far as kuruhusiwa kugombea, maana kwake aliona mamuya kuwa ana hoja nzito sana, kama anakataliwa basi na mama msekwa afukuzwe uenyekiti mara moja! na pia alitaka kujua exactly why mkono anakataliwa kugombea wazazi?

- muungwana was left in a shock, kwa sababu kwa wale tunaomjua vizuri this is one thing hapendi cha kuwa seriously challenged mbele ya watu wengine au public, akamjibu kwamba yeye kama mwenyekiti ameshaamua kwamba mamuya hafai kwa sababu ya kashfa nzito dhidi yake akiwa katibu, on this b became irritated na kudai kwamba uamuzi huo wa muungwana was unfair and unjustice kwa mamuya kama mwanachama wa ccm, hoja iliyopelekea mguno mzito toka wka wajumbe karibu wote ukumbini, kuashiria kushangaa kwao kwamba kumbe mkulu naye anajua haki na uonevu! Now muungwana was more upset kuliko mwanzo na kusema kwa ukali zaidi kuwa hakuna mjadala tena na on mkono alisema kwamba sio tu hamtaki mkono bali anafikiria kuivunja kabisa jumuiya hiyo ambayo alidai kwamba haina faida yoyote kwa chama baada ya shule zake zote kuchukuliwa na serikali hawana faida tena zaidi ya kua mzigo kwa chama.

- After this b was very upset that kwamba alipoulizwa maoni yake kwenye ishus zingine zilizofuata he would not even answer them, na mwishowe aliamua kuondoka, kitu ambacho kiliwashangaza sana wajumbe waliobaki, sasa kushikwa kwa mramba na yona wafuasi wa karibu sana wa b kuna anything to do na this incident?

Again my point again ni kwamba tuyaangalie haya yanayojiri kwa macho mawili!
 
-
- After this b was very upset that kwamba alipoulizwa maoni yake kwenye ishus zingine zilizofuata he would not even answer them, na mwishowe aliamua kuondoka, kitu ambacho kiliwashangaza sana wajumbe waliobaki, sasa kushikwa kwa mramba na yona wafuasi wa karibu sana wa b kuna anything to do na this incident?

Again my point again ni kwamba tuyaangalie haya yanayojiri kwa macho mawili!

Lazima fisadi Mkapa huko aliko ana wasi wasi wa hali ya juu. Kumbuka kauli ya Pesatatu Mramba kwamba, "Hata majani tutakula, lakini lazima rada inunuliwe" hii ni katika kuupigia debe uamuzi wa fisadi Mkapa kununua Rada ta $40 million ambao ulipingwa sana na Watanzania wengi pamoja na nchi za wafadhili, pia katika umiliki wenye utata wa Kiwira kuna ushahidi wa kutosha unonyesha kwamba fisadi Mkapa na Msabaha walitumia nyadhiza zao kutupora Watanzania mgodi wa Kiwira. Kwa hiyo anaona dalili za wale ambao aliwaamini sana na kuwa karibu nao wanaanza kuwekwa kiti moto (kama siyo usanii) hivyo anajua fika na yeye madudu aliyoyafanya akiwa Ikulu basi si muda mrefu wanaweza kumtolea aibu na kumuweka kiti moto, tusubiri tuone mwelekeo wa hili sakata.
 
-according to more dataz ni kwamba mtoto wa el na accountant mmoja wa ra wanatakiwa kukamatwa "very soon" kwa sababu as far as richimonduli hawa ndio waliokuwa wakienda dirishani kila mwisho wa mwezi kuchukua cheki ya dola laki moja na nusu kwa ajili ya malipo ya serikali kwa umeme hewa wa richimonduli.

- the more dataz ni kwamba makelele mengi ya warioba kuhusu rushwa na awamu ya nne ndio yamemponza, sasa kuna some mtandaos wako tayari kwa revenge ili apewe darasa japo kidogo tu kama alivyonidokezea mtandao mmoja, "....ili aache filimbi..". mwenyewe warioba anakubali kuwa it is only a matter of time kabla hawajaenda kumgongea anazo habari zote na he is ready.

- viongozi wengi wa juu wanaofuatilia kinachoendelea na kamata kamata, wana wasi wasi mkubwa kuwa hii kitu kuna siku itamfikia mstaafu wa idara ambaye ni an important player kwenye ma-deal yote machafu, sasa wanasema kua hapo kuna hatari kubwa sana unless muungwana ana uhakika na anayoyafanya sasa...ama sivyo wanadai huenda ukawa mwisho wake pia!

As usual tunaendelea kwa makini sana kufuatilia kwa karibu hii kamata kamata na the rest of the stories, weekend imefika tutagusa kila mahali kupata exactly kinachojiri!

Thanxs!
 
Field Marshall Es,
Unajua mkuu siku zote Terrorism huanzia ktk nafasi kama hivi. Najua uliwahi kuiona ile sinema ya Al Pacino - Scarface ambayo alisema kwanza unatakiwa upate fedha ambazo zinakupa Power, then The all world is in your hand!..
Hii ndio chimbuko la ma-terrorist wote..
Viongozi wetu wengi sana wameweza kujipatia fedha za nguvu kiujanja ujanja kisha wakajenga ngome zao (wafuasi) kuhakikisha kwamba wana power na kuwa respected sio tu kwa madaraka waliyokuwa nayo isipokuwa kwa yale wanayoweza kuyafanya nje ya Ubinadamu.
Sasa inapofikia watu kama hawa kukatwa ktk Utawala ndipo utaona wanaanzisha ugaidi..Tazama viongozi wote ktk Ugaidi (terrorists) ni watu ambao wamejikuta wakikatwa ktk Utawala na kwa sababu waliisha jijenga kwa fedha na wafuasi huunda majeshi dhidi ya utawala unaowatishia..Kumbuka Lowassa alivyopokelewa huko kwao kijijini kama shujaa.. Huyu ni Scarface in the making!..
Kikwete ana kazi kubwa sana sasa hivi na kama hataweza kumaliza mtandao sasa hivi basi ndivyo atakavyokuwa na wakati mgumu zaidi siku za mbele..Sababu zitakazo mshinda leo zitakuwa mara mbili mwakani..
Kuhusiana na Mkapa binafsi nadhani nitamsamehe mzee wangu isipokuwa huyo mkewe!... huyu first Lady bado anatumaliza, na kusema kweli ni sawa na yule first lady wa Manila, Ufilinipo aliyekuwa na pair sijui ngapi za viatu..huyu anakusanya tu majumba ya serikali karibu Upanga yote kauza yeye ati Real Estate agency!
 
Date::11/26/2008
Wananchi wafurahia vigogo kutinga mahakamani
Na Waandishi Wetu
Mwananchi

Idadi kubwa ya waanchi wamepongeza serikali kuwapandisha kizimbani mawaziri wawili wa zamani wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi, huku baadhi wakisema kuwa bado wengi zaidi wanatakiwa kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Wananchi wengi hawakuridhishwa na majina ya watuhumiwa 20 waliopandishwa kizimbani kwa makosa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malimbikizo ya Madeni ya Nje (EPA), wakidai kuwa hakukuwepo na vigogo, zaidi ya mfanyabiashara maarufu wa jijini, Jeetu Patel.

Lakini juzi mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona walipandishwa kizimbani na kusababisha maoni ya wengi kubadilika kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya tuhuma za vitendo vya ufisadi.

Mramba, waziri mkongwe aliyepata kushika wizara nyeti kwenye serikali za awamu zote nne, na Yona, aliyeshika wizara kwenye serikali za awamu mbili, walipandishwa kizimbani juzi kujibu tuhuma za kutumia vibaya ofisi kwa kuiruhusu kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza kuingia mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria. Kwa pamoja walisomewa jumla ya mashtaka 13.

Kesi hiyo ilivuta hisia za watu wengi waliofika Mahakama ya Kisutu juzi baada ya uvumi kuzagaa kuwa vigogo wangepandishwa kizimbani. Na baada ya vyombo vya habari kuripoti kwa kina kesi hiyo jana, watu wengi walioongea na Mwananchi walionekana kufurahishwa na hatua hiyo, wakisema sasa haki itachukua mkondo wake.

"Ndugu mhariri, nimefarijika sana baada ya kuona kwamba sheria inafuatwa katika kutetea maslahi ya wananchi, bila kujali majina, na nyadhifa walizokuwa nazo," anaandika mmoja wa wasomaji wa Mwananchi aliyetoa maoni yake kupitia anuani ya e-mail akijulikana kwa jina la Silumbe.

"Pamoja na sifa kubwa tunayoipa serikali yetu, napenda kutoa dukuduku langu kwamba, hii isiwe "changa la macho" kwetu sisi wapiga kura. Watanzania tumekuwa tukipewa utamu wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kwa ahadi mbalimbali, lakini mwisho wa siku, huwa hakuna kitu kipya.

"Waswahili walisema 'maji ukiyavulia nguo, lazima uyaoge'. Sasa tunataka tuone hawa

watu, na wengine kama hao, wanapata kile kinachotarajiwa na wananchi walio wengi. Muda wa kulindana umeshapitwa na wakati. Mtanzania anayeowaongoza wenzake katika wadhifa wowote ule, anapaswa kutambua kwamba hicho cheo ni dhamana tu."

Msomaji mwingine aliyeandika ujumbe wake kwa e-mail, Jeanet alisema "kweli nimefurahia sana kwa kukamatwa kwao ili sheria ifuate mkondo wake, Mungu ibariki Tanzania na mahakama ya Kisutu itoe haki, Amen."

Mkuu wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Jussa alisifu hatua hiyo akisema imeonyesha mabadiliko katika siasa.

"Kwa kweli haya ni mapinduzi makubwa katika uendeshaji wa siasa za nchi na demokrasia kutokana na ukweli kuwa watu hawa waliowahi kushika nyadhifa kubwa serikalini wamefikishwa mahakamani," alisema Jussa.

"Hatua hii itasaidia kupunguza vitendo vya viongozi nchini kutumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi na mali za umma zitaheshimika.

"Hii itasaidia angalau kujenga heshima ya mali za umma kwa viongozi na kupunguza matumizi mabaya ya madaraka."

Mwanasiasa mwingine aliyeungana na watu waliosifu kufikishwa mahakamani kwa vigogo hao, alikuwa mwenyekiti wa chama cha TLP, Agustine Mrema.

"Nitakuwa mnafiki kama sitampongeza Rais (Jakaya) Kikwete kwa kuanzisha vita ambavyo vilifumbiwa macho. Hakuna aliye jasiri hata wa kufungua mlango katika serikali za awamu ya pili na ya tatu dhidi ya mafisadi. Kikwete ameonyesha njia, sasa naomba rais anipe raha, apanue wigo wa mapambano bila woga aliokoe taifa," alisema Mrema aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani.

"Siyo Mramba na Yona pekee... wapo wengi. Mimi nawajua, wapo mawaziri na makatibu wakuu wa wizara, Watanzania waache kusherehekea mambo yasiyo na kichwa wala miguu."

Hata hivyo, alisema serikali imefungua mlango, kuonyesha ujasiri na njia ambayo serikali ya awamu ya pili ya Ali Hassan Mwinyi na awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa ilifumbia macho na kushindwa kuyaanzisha.


Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam nchini, Ramadhan Sanze alisema serikali imeonyesha ujasiri wa hali ya juu ambao ulikuwa unahitajika kwa muda mrefu na wananchi wa Tanzania.

Aliitaka serikali kuendeleza ujasiri huo na kuwafikisha mahakamani wale wote ambao wanatuhumiwa kwa upotevu wa fedha za umma.

Mbali na vigogo hao kufikishwa mahakamani, serikali imekuwa ikisema kuwa wengi zaidi wanakuja na kwamba hakuna atakayekwepa mkono wa sheria kama alihusika kwa njia yoyote ile na ufisadi, lakini bado kuna watu ambao wanaona bado juhudi kubwa hazijafanyika.

Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa alisema kuwa hata rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa hana budi kufikishwa mahakamani ili haki itendeke baada ya watendaji wake hao wawili kusomewa mashtaka juzi.

Dk. Slaa, ambaye amekuwa kinara kwenye kampeni dhidi ya ufisadi, alisema hadi sasa bado anasubiri kuona orodha yote ya watuhumiwa ambayo waliitaja kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwembe Yanga, mwezi Septemba mwaka jana ikifikishwa mbele ya vyombo vya haki.

"Hadi sasa siwezi kusema kwamba nimeridhika," alisema mbunge huyo wa Karatu. "Ninachotaka ni kuona orodha yote tuliyoitaja Mwembe Yanga inafikishwa mahakamani, akiwemo Mkapa," alisisitiza.

"Mkapa anapaswa kufikishwa mahakamani ili akishatikiwe na aeleze mahakama uhusiano wake na kampuni ya Tan Power Resources Limited, ambayo ilikuwa ikilipwa mamilioni ya shilingi na Tanesco.

"Mkapa pia anapaswa kueleza namna alivyojiingiza katika biashara kwenye mgodi wa makaa ya mawe Kiwira.

"Hivi ni vitu viwili tofauti, hapa Mkapa alifanyabiashara si kazi za urais, hivyo anapaswa kufikishwa mahakamani."


Habari hii imeandaliwa na Ramadhani Semtawa, Exuper Kachenje, Salim Said na Leon Bahati.
 
Very interesting observation. Bado naona ni tatizo ambalo kwa upande fulani limekuwa kama baraka. All out war between CCM mtandao na CCM asili, half war within Mtandao inaweza kufunua mengi zaidi ya tunayoyaona. Lakini naona kama kutulundikia yote kwa wakati mmoja ni kama kuna tiktak inataka kuchezwa, i hope JF as usual itakuwa on top na kufahamu jannja hiyo. I wonder mpaka sasa hakuna mtu aliyekufa kwa "ugonjwa wa moyo" au "shinikizo la damu", kutokana na "mshtuko" wa hali inavyoendelea, nasubiria habari ambayo naona ni matter of time sasa.
 
Tarime has proved that CCM with all its mighty can lose an election, unless they play the Kibaki game. They don't want to go there and they are conducting internal cleansing. That's what they want us to believe and really if that's the case we will see no stone unturned.

mkapa's regime, after death of Mwalimu, turned monstrous and if Kikwete's regime had proceeded on the same footprints, Just as Lowassa and co. seemed to believe, this country could be on a fast-track to a failed state. Believe me, 5 years down the road would have been enough to take us the Somalia way.

People still harbour some suspicions, especially because some sharks are still at large or on the loose. Kikwete has assured us that all is not well for the SHARKS and we want to believe him. If these are genuine and really committed efforts to cleanse CCM, then all sharks will be netted and we shall believe Kikwete was not among them and another landslide will be assured.

I know for sure, where we were, every concerned citizen must harbour some suspicions because we were really in a shit. The first leaders to rise against the coloinialist with all their mighty everybody thought they were on the loosing side. Some people are already raising the fears by saying if Kikwete continues, he will touch the untouchables, and that will be his end too! Let's fear the FEAR. It is our worst enemy.

Lowassa was the biggest mtandao player! If he was axed so unceremoniously then let's believe this is a real IRON BLOOM to cleanse CCM until otherwise proven. Let's rally our support behind the CCM chairman. Our support will fuel more actions. We want to see a respected government not a horde of thugs. Kikwete is on the way to prove his commitments to the electorate.

Ammandla!
 
Kumbuka bosi mwenyewe naye ana skeletons zake kwa mfano mkataba wa IPTL, si alianguka sahihi yeye mwenyewe JK
 
Mramba, Yona waenda Mahakama Kuu

NA MWANDISHI WETU
MAWAZIRI wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, wamewasilisha ombi Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba kupitiwa upya kwa uamuzi wa dhamana uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu.

Kupitia ombi namba 54/2008, lililowasilishwa mahakamani hapo jana mchana, Mramba na Yona wanaiomba mahakama kupitia upya uamuzi uliotolewa juzi na Hakimu Hezron Mwankenja.

Wanadai kifungu namba 148 (5) (e) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinaelekeza kutolewa dhamana ya nusu ya kiasi cha fedha kinachohusika kwenye shitaka au mali inayolingana na kiasi hicho.

Hakimu Mwankenja anadaiwa kukiuka kifungu hicho kwa kuamuru kuwasilishwa kwa fedha tu, bila ya kutoa nafasi mbadala inayotolewa kisheria ya kuwasilisha mali sawa na kiasi hicho cha fedha.

Katika uamuzi wa juzi, Hakimu Mwankenja aliamuru Mramba na Yona kudhaminiwa kwa fedha taslimu sh. bilioni 2.9.

Kupitia mawakili wao, washitakiwa hao wanadai kiasi hicho cha fedha ni kikubwa. Ombi hilo lilikuwa halijapangiwa Jaji wa kulisikiliza.

Jana asubuhi, Kampuni ya Mawakili ya Trust Mark, iliwasilisha ombi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuomba kupatiwa mwenendo wa kesi kwa ajili ya kuwasilisha ombi hilo Mahakama Kuu.

Mramba, aliyekuwa Waziri wa Fedha na Yona, Waziri wa Nishati na Madini, walifikishwa mahakamani juzi kujibu mashitaka 13, wakituhumiwa kutumia madaraka vibaya na kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 11.7.

Mramba, ambaye ni Mbunge wa Rombo na Yona walishindwa kutimiza masharti ya dhamana kwa kutokuwa na kiasi hicho cha fedha, hivyo walipelekwa rumande hadi Desemba 2, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.

Wakati huo huo, Joseph Burra anaripoti kuwa, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wamewataka Watanzania kuwa watulivu wakati vyombo vya sheria vikifanya kazi zake.

Pia wamepongeza hatua ya serikali ya kuwafikisha mahakamani washitakiwa hao, jambo linaloonyesha kuwapo kwa utawala bora.

Akizungumza na Uhuru kwa njia ya simu jana, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema wakati vyombo vya sheria vinafanya kazi, Watanzania wanapaswa kuwa watulivu na wavumilivu na kwamba, hilo lisivuruge amani ya nchi.

Alisema serikali imeonyesha hatua nzuri ya utawala wa sheria na kwamba, itafanya kila mmoja kuwajibika kwa nafasi yake kuitumikia nchi.

"Ni hatua nzuri ya utawala wa sheria itakayofanya kila mtu kuwajibika... tuwe watulivu, tuvute subira, tuachie vyombo vya sheria vifanye kazi," alisema.

Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ambaye ni Mbunge wa Karatu, alisema enzi za mfumo wa kulindana sasa umefika mwisho na ana imani kila kiongozi atawajibika kwa nafasi yake.

Mbunge wa Morogoro Mjini, Dk. Omary Mzeru, alisema huo ndio utawala bora unaofuata sheria.

"Ninachoweza kusema ni kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria, mtu yeyote anapotuhumiwa anafikishwa mahakamani bila kujali waziri au mbunge, tunachotakiwa kujifunza ni kwamba sheria haina macho, na ni msumeno," alisema Mzeru.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, alisema kuwa, Tanzania imetoa picha nzuri ya utawala bora, kwa kizazi cha sasa na kijacho, kwa kuwataka kuwa makini na madaraka watakayoyapata au waliokuwa nayo.
 
Kumbuka bosi mwenyewe naye ana skeletons zake kwa mfano mkataba wa IPTL, si alianguka sahihi yeye mwenyewe JK
 
Naomba mtu yeyote mwenye taarifa za uhakika atueleze kama hawa jamaa kweli wako Keko hadi sasa. Nina wasiwasi jamaa wanalala home na kutuzuga kwamba wako Keko. Bongo Darisalama kila kitu ni POSSIBLE!!
 
Imetolewa mara ya mwisho: 27.11.2008 0004 EAT
•
...Wabunge wamlilia Mramba, wampongeza Kikwete


Na Francis Godwin, Iringa



MWENYEKITI wa wabunge mkoa wa Iringa, Bw. Stephen Galinoma ambaye ni Mbunge wa Kalenga na Mbunge wa Mufindi Kusini, Bw. Benito Malangalila wamesema tuhuma dhidi ya mawaziri wawili wastaafu, Bw. Basil Mramba na Bw. Daniel Yona, si za kutisha.




Wabunge hao wanalinganisha tuhuma hizo za kutumia vibaya madaraka wakiwa watumishi wa Serikali na za wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), ambao wanasema walipaswa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhujumu uchumi ambazo kimsingi hazina dhamana.



Wamesema hata hivyo, Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, imevunja rekodi ya uongozi kwa hatua yake ya kutowafumbia macho viongozi 'wazembe' na kuwafikisha mbele ya sheria mawaziri na wabunge.



Bw. Mramba alikuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya Rais Benjamin Mkapa na Waziri wa Miundombinu na wa Biashara na Viwanda katika Serikali ya Rais Kikwete, wakati Bw. Yona alikuwa pia Waziri wa Fedha katika Serikali ya Rais Mkapa.



Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana kwa nyakati tofauti, Bw. Galinoma na Bw. Malangalila walisema wabunge wa mkoa wa Iringa wamepokea kwa masikitiko makubwa hasa kutokana na mbunge mwenzao, Bw. Mramba kufikishwa mahakamani huku pia wakiipongeza Serikali kujisafisha kutokana na uchafu uliosababishwa na tuhuma mbalimbali.



“Nafurahi, kuwa sheria imechukua mkondo wake, hivyo tutajua kama wana hatia au la ... tofauti na ilivyokuwa awali ambapo watu walikuwa wakiwatuhumu na kuichukia CCM kwa mambo yanayotendeka.Nasema awali tulikuwa gizani sasa tupo nuruni tuvute subira,” alisema Mwenyekiti Galinoma.



Lakini Bw. Galinoma alihoji sababu za Serikali kuchelewa kuwachukulia hatua za kisheria kwa muda wote huo, ambao walikuwa madarakani hadi leo ambapo mambo yameshaharibika.

Pia alisema pamoja na shauku kubwa ya Watanzania kutaka kujua hatima ya sakata la EPA, wanapongeza kwa kuibua sakata la matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi waliotangulia.



Walisema kwa sasa Watanzania wamefunikwa macho, kwa tuhuma wanazokabiliwa nazo za matumizi mabaya ya ofisi zao, ikiwa ni pamoja na kusamehe kodi na kusababisha hasara ya mabilioni ya fedha, ila bado haijajulikana kama walichukua rushwa au ni wahujumu uchumi.


“Ujue hawa si kama watuhumiwa wa EPA, ambao kimsingi kesi yao ilipaswa kuwa ya uhujumu uchumi na kunyimwa kabisa dhamana ... hawa wanatuhumiwa kutumia vibaya madaraka waliyopewa.



"Sasa hapa pia bado tupo gizani na kama hilo ndilo kubwa, kuna uhakika mkubwa wa watuhumiwa hao kushinda kesi zao, iwapo wataweka mawakili wazuri ... watuhumiwa wa EPA ndio wabaya wetu Watanzania, kwani hawatofautiani na wahujumu uchumi,” alisema Bw. Galinoma.



Aliongeza kuwa kufikishwa kwa mawaziri hao na wabunge mahakamani, heshima ya wabunge imepungua, lakini ni fundisho kwa viongozi wengine ambao wana tabia ya kutumia vibaya nafasi zao.

Bw. Malangalila alisema anasikitika kwa hatua ya Serikali kumfikisha mahakamani mbunge huyo, ingawa kufikishwa kwao ni ushindi kwa CCM mwaka 2010 hasa katika kuonesha mfano wa uwajibikaji kwa viongozi.



Alisema Serikali ya Kikwete imeonesha mfano, kwa kuibua uozo wa Serikali ya Awamu ya Tatu kwa hatua yake ya kuwafikisha mafisadi mahakamani bila kuwaogopa, hali ambayo inatoa matumaini makubwa kwa wananchi kwa Serikali yao.



“Kinachofanyika sasa ni kitimtim na kizaazaa kwa mawaziri waliopo madakarani na wastaafu ... kwani ukisikia ngoma imenoga, basi ndiyo sasa, lazima kila mmoja atacheza hata kama si kwa kuingia uwanjani basi kichwa kitatikisika,” alisema.

Bw. Malangalila na kuongeza kuwa hatua ya kufikishwa mahakamani vigogo hao ni mafanikio makubwa kwa CCM, wabunge na madiwani wa CCM, ambao walikuwa wamekatisha tamaa na masuala ya ufisadi na hata kuanza kujiandaa kutogombea mwaka 2010, sasa watabadilisha msimamo na kuendelea kugombea.



Pamoja na wabunge hao, baadhi ya wananchi mkoani hapa walipokea kwa shingo upande hatua ya kufikishwa mahakamani vigogo hao na kuwa Serikali inawapiga 'mchanga wa macho' kwani walitarajia mafisadi wa EPA wote wakifishwe mahakamani akiwemo mmiliki wa kampuni ya Kagoda Agricultural LTD, hapo ndipo wangepongeza kuwa kweli kazi imefanyika.



Bw. Abuu Changawa ambaye ni Mweka Hazina wa Vijana Taifa wa TLP alisema aliposikia vigogo hao wamefikishwa mahakamani, alidhani ni kwa tuhuma za EPA, lakini baada ya kusikia ni matumizi mabaya ya ofisi zao, alibaini kuwa ni 'mchezo mchafu' unaofanyika ili kupoteza Watanzania.



Lakini Bw. Denis Lupala wa Mgama, Iringa Vijijini na aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CCM wa Wilaya ya Iringa Mjini, Bw. Adamu Lameck, walisema hatua ya vigogo hao kukamatwa ni mafanikio ya ushindi kwa CCM 2010.

“Sisi tunaona ni sahihi kuchukuliwa hatua za kisheria mawaziri hao wastaafu kwa uzembe walioufanya wakiwa kazini na pia hii italeta heshima kwa chama chetu,” alisema Bw. Lameck.
 
Imetolewa mara ya mwisho: 27.11.2008 0004 EAT
•
...Wabunge wamlilia Mramba, wampongeza Kikwete


Na Francis Godwin, Iringa



MWENYEKITI wa wabunge mkoa wa Iringa, Bw. Stephen Galinoma ambaye ni Mbunge wa Kalenga na Mbunge wa Mufindi Kusini, Bw. Benito Malangalila wamesema tuhuma dhidi ya mawaziri wawili wastaafu, Bw. Basil Mramba na Bw. Daniel Yona, si za kutisha.

Wabunge hao wanalinganisha tuhuma hizo za kutumia vibaya madaraka wakiwa watumishi wa Serikali na za wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), ambao wanasema walipaswa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhujumu uchumi ambazo kimsingi hazina dhamana. .

hii kitu niliyo-bold Mzee Mwanakijiji amewahi kuiongelea, hawa jamaa ni wahujumu Uchumi na ndicho ambacho wangeshtakiwa nacho. Na kama story ilivyosema kimsingi haina dhamana.
 
Back
Top Bottom