Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,008
- 142,644
Huyu jamaa ana rekodi ya kuropoka ropoka tu mambo na wala huwa habanwi kuthibitisha ayasemayo.
Si mwingine, ni huyu Zito [ndiyo, naliandika jina lake bila ‘T’ mbili] Kabwe.
Pamoja na kauli zingine za ajabu ajabu, huko nyuma alishawahi kusema anawajua au ana orodha ya Watanzania walioficha pesa huko Uswisi.
Cha ajabu, hakuwahi kuwataja. Alisema tu wapo na anawajua.
Sawa, mdomo ni wake na anaweza sema lolote lile.
Uzuri ni kwamba, kusema tu kuwa jambo fulani lipo au kitu fulani kipo, hakufanyi hilo jambo liwepo au hicho kitu kiwepo.
Haya, sogeza siku mbele hadi hii leo, jamaa kaja na ingine.
Anadai eti mkuu wa polisi, Kamanda Sirro, anajua Mo Dewji alipo.
Yeye huyo Zito kajuaje kuwa Kamanda Sirro anajua?
Yeye Zito na Sirro walishirikiana kumteka huyo Mo?
Watu wengine bana. Kazi kuropoka ropoka ili mradi tu wasifike na wafuasi wao huku kwenye mitandao ya jamii.
Na hapo inatafutwa kila aina ya sababu kumhusisha Rais Magufuli!!!!
We Zito kama unajua kuwa Kamanda Sirro anajua alipo Mo, maana yake na wewe unajua alipo Mo.
Wasaidie familia yake kwa kuwafahamisha alipo. Siyo kushinda Twitter na kuropoka ropoka pasipo na ithibati.