Sirro: Watanzania wanaosemekana wameuawa, hakuna ushahidi labda walienda kutafuta maisha sehemu nyingine

Sir luta

Senior Member
Nov 28, 2022
148
209
Mkuu wa Jeshi la polisi Mstaafu, kamanda Saimoni Sirro katika mahojiano ya kipindi Cha dakika 45 Cha ITV akijibu swali la mtangazaji Fahria Middle ametoa majibu hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na Watanzania ambao wamepotea hawajulikani walipo hadi Leo.

Tukubaliane nae kuwa akina Ben Saanane wapo Marekani au Uturuki wanachimba migodi?

========

SEHEMU YA MAHOJIANO NA SIMON SIRRO - KIPINDI CHA DAKIKA 45

Kuhusu Matokeo ya Watu kupotea
Matukio ya kupotea kwa watu nimewahi kuyaeleza sana, kwamba unaweza kusema ndugu yako amepotea kumbe amekwenda maeneo mengine kutafuta riziki. Mpaka uje kufahamu kuwa huyu mtu inawezekana kafa, [ni] aidha umepata mwili wake, umefanya postmortem madaktari wakasema kwamba huyu mtu amekufa.

Lakini kama huoni mwili, hujafanya postmortem, unapeleleza upate Ushahidi kwamba kweli huyu mtu ameuawa. Anabakia kapotea. Lakini kama kapotea una-comfirm vipi kauawa? Inawezekana huyu mtu yupo hai anatafuta riziki.

Lakini niseme kuwa kuna matukio kweli kuna watu walipotea tukapepeleza. Kwa mfano kesi ya Mo, siyo? Mo alionekana kapotea, kafanya nini lakini baadaye tukampata na baadhi ya watu wakakamatwa, wakapelekwa mahakamani.

Watanzania wasitegemee Polisi ni kama waganga wa kienyeji. Sisi tunafanya kazi kutokana na taarifa ya wananchi. Mwananchi asipokupa taarifa ya kutosha unaweza usifanikiwe. Kwahiyo kuna matukio Polisi wanaweza kufanikiwa na kuna matukio wanaweza wasifanikiwe maana hawa ni binadamu, hata kama tuna vyombo.

We fikiria nchi kama Marekani, si ni nchi imeendelea sana? Lakini kuna tukio linaweza kufanyika na wasimpate mtuhumiwa.

Kwahiyo kujibu swali lako, naweza kulaumiwa na ninaweza nilsilaumiwe. Naweza kulaumiwa kwakuwa nilikuwa na ile nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini. Nina wajibu wa kuhakikisha kuwa watu wetu wanaishi kwa amani na utulivu, siyo? Ninaweza nisilaumiwe kwasababu sikupata Ushahidi. Kuonesha kuwa hao watu wamekufa au wapo hai – wamekwenda kutafuta maisha yao sehemu zingine."

Video ya CCTV kutekwa kwa Mo Dewji ilikuwa feki?
Ukitaka kupata ukweli, sikiliza pande zote. Picha zile hazikuwa feki. Na kwanini tulete feki kwa Watanzania? Jua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi siyo nafasi ndogo. Hawezi kuleta feki; akileta feki atakuwa na nafasi gani kwa Watanzania? Anayesema ni feki anataka kuwadanganya tu Watanzania.

Maamuzi yalikuwa ya utashi wa Kipolisi au kuna siasa ndani?
Kimsingi unapokuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Sheria ndiyo inatamka Mkuu wa Polisi – ukienda kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezungumzia habari za Mkuu wa Jeshi la Polisi. Kazi yake kubwa ni kusimamia Sheria. Maana yake nini? Maana yake huwezi kutoa maamuzi kinyume na sheria, taratibu zilizopo.

Kwa kujibu swali lako, Outright …. maamuzi yangu, maelekezo yangu yalikuwa yanafuata Sheria na kanuni zilizopo. Huwezi kwenda tofauti, ukienda tofauti utaliharibu Jeshi.

Jeshi la Polisi lilitumika kisiasa?
Hivi kila mtu akisema jambo fulani huwa ni kweli? Kama wanasema kwamba tulikuwa tunatumika kisiasa ni kweli? Unaweza kusema hivyo kumbe sivyo. Mimi nijibu tu swali lako, kama nilivyosema, maamuzi yangu, matendo yangu – kila kitu kilikuwa kinafanyika kwa mujibu wa sheria.

Ubadhirifu kwenye Mfuko wa Kufa na Kuzikana
Sihusiki na siwezi kuhusika. Jeshi la Polisi lina mifuko mingi, si mfuko mmoja. Na ile mifuko ukiangalia inaongozwa na Makamishna. Kuna Kamishna wa Utawala, ndiye anayehusika; kuna Kamanda anayehusika na hiyo mifuko. Na niwaambie watanzania, mtu aliyebaini kwamba kuna wizi ni IGP mwenyewe na wala siyo CAG.

Nilipokuwa nazunguka mikoani kwasababu ile ni fedha iliyokuwa inasaidia askari anapofiwa kukidhi mahitaji mbalimbali. Kwahiyo, nikiwa nazunguka kwenye mikoa ndiyo walinieleza kwamba ‘hatupati fedha sasa hivi’. Kwahiyo nikauliza, ‘ni kwanini hampati fedha?’ Majibu yalivyokuwa hayaeleweki kutoka kwa Kamishna, nikamwelekeza DCI ambaye sasa ni IGP afungue jalada tuchunguze tujue ni kitu gani.

Kimsingi ni kwamba askari waliohusika walikamatwa, wakakiri kufanya hayo matukio na askari wachache ambao waliweza kukimbia na kesi nasikia imeanza kusikilizwa. Kuna askari wapatao 12 Zanzibar na askari wengine wapatao 7 hapa Dar es Salaam… Tuache mahakama ichukue maamuzi yake.

IGP anayeweza kufanya wizi mkubwa hivyo kwa pesa ambazo wanakusanya wenyewe, huyo IGP atakuwa kichaa sana. Sasa kama mimi, yote niliyopitia, uchaguzi nimeletewa fedha – tena fedha nyingi. Haiwezekani ukaenda kuongea…, kwanza hiyo nafasi ya kuongea na askari mdogo inatoka wapi? Tuiachie mahakama ichukue hatua yake.

Sirro ni mtu wa namna gani?
Ni mtu mwadilifu sana. Kwanza makuzi yangu wanajua nimetoka wapi. Siwezi miaka yote hiyo nikafanya kazi vizuri nikaja kumaliza vibaya.

Nidhamu na weledi katika Jeshi la Polisi
Kwa kiasi kikubwa. Ukitaka kujua jeshi lina nidhamu kubwa angali uhalifu. Je, uhalifu uliongezeka au ulipungua wakati nikiwa Mkuu wa Jeshi? Kama jeshi lisipokuwa na nidhamu, uhalifu utakuwamkubwa sana kwasababu watakuwa wanashiriki na majambazi tu. Kwasababu watakuwa wanafanya mambo ya ajabu ajabu barabarani. Suala lingine ni weledi.

Kama jeshi halina weledi, uwezekano wa kupunguza uhalifu unakuwa ni mdogo kabisa. Kwahiyo kwa kujibu swali, jeshi tulihakisha jeshi lina weledi na nidhamu ya kutosha. Na ndiyo maana nyie wandishi wa habari mnaweza kuja kufanya kazi zenu kazini. Wewe uliza kule Congo kaskazini, kuna watu wanaenda kazini? Lakini si kila wakati we Farhia unakuja ofisini hapa?

 
Mkuu wa jeshi la polisi Mstaafu kamanda Saimoni Sirro katika mahojiano ya kipindi Cha dakika 45 Cha ITV akijibu swali la mtangazaji Fahria Middle ametoa majibu hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na watanzania ambao wamepotea hawajulikani walipo hadi Leo.
Tukubaliane nae kuwa akina Ben saanane wapo marekani au uturuki wanachimba migodi?

Mjinga Sana, kwa hivyo waliondoka kinyemela hata mpakani au uhamiaji hawakupita. Stupid mzee mzima hovyo.
 
Mkuu wa jeshi la polisi Mstaafu kamanda Saimoni Sirro katika mahojiano ya kipindi Cha dakika 45 Cha ITV akijibu swali la mtangazaji Fahria Middle ametoa majibu hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na watanzania ambao wamepotea hawajulikani walipo hadi Leo.
Tukubaliane nae kuwa akina Ben saanane wapo marekani au uturuki wanachimba migodi?
Wao kama polisi ndio wanabidi wathibitishe kuwa wako hai maana ndugu zao wanawatafuta na hawajui walipo.
 
Mkuu wa jeshi la polisi Mstaafu kamanda Saimoni Sirro katika mahojiano ya kipindi Cha dakika 45 Cha ITV akijibu swali la mtangazaji Fahria Middle ametoa majibu hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na watanzania ambao wamepotea hawajulikani walipo hadi Leo.
Tukubaliane nae kuwa akina Ben saanane wapo marekani au uturuki wanachimba migodi?
Huyo nae majununi tu! Anataka kutuaminisha kuwa vyombo vyetu vya usalama havina mafungamano na vyombo vingine ili vitusaidie kujua hawa raia wapo pande zipi! Ili sirikali yetu sikivu isiendelee kunyoshewa vidole kuwa iliua raia wake? Ye kama anataka ubunge huko ccm tumkumbushe tu aweke akiba ya maneno
 
Mkuu wa jeshi la polisi Mstaafu kamanda Saimoni Sirro katika mahojiano ya kipindi Cha dakika 45 Cha ITV akijibu swali la mtangazaji Fahria Middle ametoa majibu hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na watanzania ambao wamepotea hawajulikani walipo hadi Leo.
Tukubaliane nae kuwa akina Ben saanane wapo marekani au uturuki wanachimba migodi?
Majibu mepesi kwa swali lenye uzito.. #smh
 
Back
Top Bottom