Yerusalemu Iwe makao Makuu wa Palestina - Serikali ya Tanzania

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,485
40,014
Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora Bw. Phillip Marmo ametangaza kuwa ni msimamo wa serikali ya Tanzania kuwa Palestina lazima iwe na nchi yao na "Jerusalemu iwe makao makuu yake". Alizungumza hayo katika mkutano wa "Siku ya Mshikamano na Wapelestina" iliyoadhimishwa kwenye Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam...
 
Hawa nao wakikosaga vitu vya kuongea kwenye hotuba ndio huwa wanaweweseka namna hii!

Mkuu heshima mbele, haya mambo mengine mimi huwa ninasema bora kunyamaza tu, na kuwaachia wakubwa wa dunia waamue, I mean as if kuna mtu duniani anajali msimamo wetu kuhsu Palestina,

Hawa kina Marmo, hawa yaaani ni vichekesho tu basi si angemuachia tu Membe haya, angalau maana waziri wa ofisi ya rais na usalama, anahusika vipi Palestina!

Bongo bwana yaani huu ujiko wa siasa utatufikisha mbali sana!
 
Hapo Mazee FMES umeniacha hoi kweli kweli......siku nzima nilikuwa sijacheka...sasa siku yangu imekamilika
 
Bongo bwana, au hiyo ndio official statement ya Annapolis Summit toka kwa Serikali ya TZ?? Legacy ya "Mchonga Meno" hiyo, kujiingiza kwenye migogoro isiyotuhusu kichwa wala miguu. Kibaya zaidi ina-sound kama "Amjadi" wa Iran, maana katoa maelezo makali sana juu ya hiyo summit.......hivi suala la Jerusalem linaisaidia TZ kitu gani??! aaaaagh!!
 
Hapo Mazee FMES umeniacha hoi kweli kweli......siku nzima nilikuwa sijacheka...sasa siku yangu imekamilika

Mkuu hujasikia walivyotaka kutoana pua na meno, kisa ujumbe wa NEC tu, wewe ulifikiri uchaguzi wa NEC ukiihsa watatulia? Ndio hawa sasa wanaanza hata kuingilia mambo yasiyotuhusu, ndio maana huwa tunapigwa mabomu na Al-Qaeda, kutafuta ujiko tu wa siasa yaani sasa hatuna hata mipaka tena,

Hivi kweli hakukuwa na mtu wa kumshauri kuwa waziri, hebu yaache tu haya sio yetu, kihele hele tuuuu! ahh!
 
Labda aliandaliwa speech na wapelestina wenyewe waliomwalika kwenye hiyo shughuli. Lakini akiwa waziri hatakiwi kuongea mambo ambayo hayana manufaa kwa taifa letu. Rushwa, ufisadi, utovu wa maadili kwa viongozi wetu vimekithiri na yeye ndo mhusika mkuu na sijaona lolote la maana alilofanya, leo anakurukupa na swala migogoro ya mashariki ya kati. Hiyo ni dalili ya kukosa kazi au kutojua majukumu yake na mipaka yake ya kazi na aseme nini kwenye shughuli kama hizo! Lakini labda alitumwa akaseme hivyo au alimwakilisha Mkuu wa Kaya na kupewa spichi akaisome!!
 
Kwani tatizo liko wapi?

Je kuna mtu yuko tayari kujadili FOREIGN POLICY ya TANZANIA hu,u?

KAMA YUPO BASI APITIE POST YANGU niliyonyambua ile speech ya JK kule UN au bonyeza search ya FOREIGN POLICY kisha mtanielewa nazungumzia nini

otherwise tuendelee na zile episode zetu za kawaida humu
 
Na kwa kuendelea kujadili suala hili tuna prove either tunakubaliana na Marmo kuwa jambo hili ni muhimu kwa Tanzania na dunia kwa ujumla au na sisi pia ni vilaza tunapoteza muda kujadili irrelevant issues...

Take ur pick pls
 
..nime smile kidogo,maana nilikuwa nataka ku-post naona nimeshakuwa-discouraged!
 
Ni hatari kwa watu kujiamkia kutoa msimamo wa nchi kuhusu foreign policy. Inaweza kuathiri nchi, saa nyingine ni bora kukaa kimya. What happened to Non alligned Movement?
 
Kule hata hao wanaojiita Polisi wa Dunia hawawezi kuleta suluhisho.....

Kumehusisha sana masuala ya kiimani!

Vita ile kuisha mpaka Masihi arudi
 
jamani tuacheni kuchonga, huu m simamo wa Tanzania si wa leo wala jana.

huyu just kaukumbushia tu. ila msimamo huu toka wakati wa mwalimu. na ilikuwa mikutano mingi ya CCm viongozi wa palestina hasa PLO hualikwa hasa Hayati Yassir Arafat.

mkjj nnaamini unalijua hili sana tu. na kuna kipindi uhusiano wetu ulikuwa mbaya sana na waisrael kwa suala hili.

tuacheni upayakwaji usio na maana, na hapo palikuwa ni hafla ya palestina na ndio mahala pake kuonesha jinsi gani ss ndugu zao tunavyowaunga mkono ktk harakati za kujikomboa na kuundwa taifa lao.
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora Bw. Phillip Marmo ametangaza kuwa ni msimamo wa serikali ya Tanzania kuwa Palestina lazima iwe na nchi yao na "Jerusalemu iwe makao makuu yake". Alizungumza hayo katika mkutano wa "Siku ya Mshikamano na Wapelestina" iliyoadhimishwa kwenye Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam...

Wakati anakata hii speech alikuwa ameshakata mizinga mingapi ya Konyagi???
 
jerusalem ni ya waisrael tangu enzi ya Yesu. leo ndio iwe hivyo?
 
Watu wanangangania madaraka tukiwambia watoke wapishe wenye akili waongoze hawataki... sasa haya ndo matokeo yake,
 
Huyu amesema kwa upumbavu wake na unafiki wake. Mwehu na ndoto zza mchana.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora Bw. Phillip Marmo ametangaza kuwa ni msimamo wa serikali ya Tanzania kuwa Palestina lazima iwe na nchi yao na "Jerusalemu iwe makao makuu yake". Alizungumza hayo katika mkutano wa "Siku ya Mshikamano na Wapelestina" iliyoadhimishwa kwenye Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom