jerusalem ni ya waisrael tangu enzi ya Yesu. leo ndio iwe hivyo?
Ndiyo msimamo wa nchi nyingi duniani.Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora Bw. Phillip Marmo ametangaza kuwa ni msimamo wa serikali ya Tanzania kuwa Palestina lazima iwe na nchi yao na "Jerusalemu iwe makao makuu yake". Alizungumza hayo katika mkutano wa "Siku ya Mshikamano na Wapelestina" iliyoadhimishwa kwenye Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam...
Hawa nao wakikosaga vitu vya kuongea kwenye hotuba ndio huwa wanaweweseka namna hii!
Mkuu heshima mbele, haya mambo mengine mimi huwa ninasema bora kunyamaza tu, na kuwaachia wakubwa wa dunia waamue, I mean as if kuna mtu duniani anajali msimamo wetu kuhsu Palestina,
Hawa kina Marmo, hawa yaaani ni vichekesho tu basi si angemuachia tu Membe haya, angalau maana waziri wa ofisi ya rais na usalama, anahusika vipi Palestina!
Bongo bwana yaani huu ujiko wa siasa utatufikisha mbali sana!
Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora Bw. Phillip Marmo ametangaza kuwa ni msimamo wa serikali ya Tanzania kuwa Palestina lazima iwe na nchi yao na "Jerusalemu iwe makao makuu yake". Alizungumza hayo katika mkutano wa "Siku ya Mshikamano na Wapelestina" iliyoadhimishwa kwenye Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam...
Ndiyo msimamo wa nchi nyingi duniani.
jamani tuacheni kuchonga, huu m simamo wa Tanzania si wa leo wala jana.
huyu just kaukumbushia tu. ila msimamo huu toka wakati wa mwalimu. na ilikuwa mikutano mingi ya CCm viongozi wa palestina hasa PLO hualikwa hasa Hayati Yassir Arafat.
mkjj nnaamini unalijua hili sana tu. na kuna kipindi uhusiano wetu ulikuwa mbaya sana na waisrael kwa suala hili.
tuacheni upayakwaji usio na maana, na hapo palikuwa ni hafla ya palestina na ndio mahala pake kuonesha jinsi gani ss ndugu zao tunavyowaunga mkono ktk harakati za kujikomboa na kuundwa taifa lao.
Nchi nyingi zikichukua msimamo kuwa makao makuu ya Tanganyika yawe Singida tukubali kwa sababu ni "nchi nyingi"?