Yericko Nyerere: Naziona Simba na Yanga nusu fainali

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Very interesting, @simbasctanzania vs @alahly hii game ni 50/50 hata Simba akitoa sare Kwa Mkapa bado game itabaki 50/50 na uamuzi utafanywa Cairo kwa mikwaju ya penati. Katika hili naiona bahati kwa Simba japo kuna marekebisho makubwa ya haraka yanatakiwa kufanywa kwa kikosi hiki safu ya ushamhuliaji na safu ya ulinzi. Kama Simba itacheza mechi zake kama ilivyocheza kwenye michuano ya AFL au Club Bingwa 2022/23 ilipotolewa na @wacofficiel basi naweka sarafu ya 55/% kwa Simba kwenda Nusu Fainali.

Very dramatic @yangasc vs @sundownsfc, hii ni mechi ya kipekee sana, kwa Yanga matumizi bora ya uwanja wa nyumbani wakishinda zaidi ya bao 2 bila basi wanakuwa na 51% ya kusonga mbele! Yanga kusonga mbele kunategemea zaidi mchezo wa kwa Mkapa, wakati Simba ina wastani mzuri wa kusonga mbele kwenye game ya mwisho Cairo bila kutegemea matokeo ya game ya Dar, Sijui kama naeleweka!

Kwa nadharia hiyo, nilivyoiona Yanga ikicheza na Al Ahaly Dar na kule Cairo na ilivyocheza na CR Belz, naipa Yanga nafasi ya kusonga mbele dhidi ya Memelod, Muhimu Yanga na viongozi wote hasa @caamil_88 wakitambua kuwa hii ni club bingwa, timu zote 8 ni bora Afrika, Wasijihisi wao wageni katika michuano hii.

Fainali ya Yanga iko Dar, Fainali ya Simba iko Cairo. Kwa gharama yoyote hata ikitakiwa @ahmedally_ na @alikamwe watolewe kafara timu zishinde basi wazee wa vilabu hivi msisite, Taifa liko vitani, ushindi ni muhimu kuliko uhai wa yeyote!😂 Tunataka wote Wazimie!

Vikosi vya kamati za ufundi vianze kazi leo sio kesho, Muhimu zaidi Viongozi wa Vilabu hivi Ndugu @salim_tryagain na @caamil_88 tambueni hela ya kamati za ufundi haipiti kwa mhasibu na haina ukaguzi wa mahesabu.

Narudia hela ya Kamati za ufundi haina CAG!

Mkileta ukora kuchungulia fuko tusilaumiane tukipigwa nje ndani!
 
1710263037788.png
 
TIMU ZENU ZINEISHIA HAPO

HIZI NDIO FAIDA ZA SIASA KWENYE MPIRA NA CHUPLI CHUPLI ZA UWEKAZAJI BANDIA WA AKINA MO......

SIMBA NA YANGA ZOTE OUT
 
Hela ya kamati za ufundi haipiti kwa mhasibu na haina ukaguzi wa mahesabu.
 
Fainali ya Yanga iko Dar, Fainali ya Simba iko Cairo. Kwa gharama yoyote hata ikitakiwa @ahmedally_ na @alikamwe watolewe kafara timu zishinde basi wazee wa vilabu hivi msisite, Taifa liko vitani, ushindi ni muhimu kuliko uhai wa yeyote! Tunataka wote Wazimie!

Vikosi vya kamati za ufundi vianze kazi leo sio kesho, Muhimu zaidi Viongozi wa Vilabu hivi Ndugu @salim_tryagain na @caamil_88 tambueni hela ya kamati za ufundi haipiti kwa mhasibu na haina ukaguzi wa mahesabu.

Narudia hela ya Kamati za ufundi haina CAG!

Mkileta ukora kuchungulia fuko tusilaumiane tukipigwa nje ndani!

Hi ni kwa mujibu wa mizimu?
 
Asijali, atayeanza kucheza kwa Mkapa, atarogela dozi ya wiki nzima...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom